Elections 2010 Baada ya Membe kugomewa; JK kuzungumza na Viongozi wa dini Usiku

Huyu jamaa bana!!! Anahaha tu!!!

Nilikuwa na kamanda mmoja wa JWTZ ananiambia wana uhakika JK atapita!!!

Nikasema hata wanajeshi wamekuwa wanasiasa!!!
 
Jamani si aje hata kwangu nimuombee, mi sihitaji hata miadi...pole kaka
 
Hao wakuu wa dini sijui wataupokeaje ujumbe wa JK, maana je watamsikiliza JK au Mungu. anyway vyovyote iwavyo changes is still there,
DR. Slaaaaaaaaa hazuiliki, sasa hivi tunampango mkakati wa kumwomba jk atupe kura yake.
 
afadhali maaskofu wamekuwa wawazi zaidi, wasikubali hawa jamaa kutugawa wananchi! Kumbukeni 2005 walim-endorse kama chaguo la Mungu!
This time, wamemuona amekengeuka.
Long live Tz
 
Madhebu ya mengine ya Kikristo yalishaamua kutosali Jpili, mengine watasali misa moja kuanzia saa 12 asubuhi na zitakua fupi kadri inavyowezekana! ili wawahi wakatoe hukumu kwenye masanduku ya kura, wangeendelea tu na kampeni zao wamechelewa sana!
 
Well my dear friend JK ...it is too late to catch the departed plane....just go home and have a piece of mind................it is a case of too little too late.

Mkuu inawezekana vipi awe na peace of mind? Jana kuna mdau amesema alienda kwa Sheikh Yahya na kuondoka na furushi lisilojulikana, na sasa anataka kwenda kwa maaskofu na wachungaji, can 2 real work together in one persons mind? si rahisi naona itakuwa ni pieces of mind na sio Peace of mind.
 
Ukisoma habari hii unaweza kuelewa ni kwa nini anakutana nao!

Membe atetea serikali kwa maaskofu

Saturday, 23 October 2010
Source: Mwnanchi

Frederick Katulanda, Mwanza


WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema CCM imegawanyika makundi mawili, moja likiwa ni lile la viongozi walioshindwa kuupata urais na lingine likiwa ni lile la Kikwete na serikali yake.

Alisema kundi lililoshindwa na Kikwete kupata urais ndilo limekuwa likisambaza ujumbe na taarifa za kumchafua Kikwete na serikali yake kuwa ameshindwa kuwashughulikia mafisadi na kuigeuza nchi hii kuwa ya kidini kwa kuteua viongozi wengi wa ngazi za juu nchini waislamu.


Membe alijikuta akieleza hayo wakati alipokuwa akijibu maswali ya viongozi wa dini na madhehebu ya kikristo kuhusu masuala mbalimbali aliyoyazungumzia kuhusu ufisadi, udini na serikali kujiunga na IOC .


Alisema kutokana na uvumi huo kuenezwa zaidi wakati huu wa kampeni ameanza ziara ya kupita mikoani nchini kuzungumza na viongozi wa dini kusafisha hali hiyo ya hewa.


Katika kikao hicho kilichofanyika Hoteli ya G and G jijini Mwanza juzi na kuhudhuriwa viongozi wa madhehebu ya kikristo zaidi ya 100, Membe alisema alikuwa na mambo manne ya kufafanua ambayo ni tuhuma za kuwepo kwa udini, ufisadi, suala la Tanzania kutaka kujiunga na OIC na pamoja na kuanzishwa ka mahakama ya Kadhi nchini.


"Wakristo wanaonekana kujitenga wakidai kuwa Kikwete kaonyesha mpasuko kwa kupendela waislamu katika serikali yake na kuwa ifikapo mwaka 2015 Tanzania itakuwa imejiunga na OIC na kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi na mengine yakidai kuwa ameshindwa kushuhgulikia ufisadi hapa nchini, mambo haya siyo kweli." alisema


Ingawa Membe alikanusha Tanzania haijafikia uamuzi wa kujiunga na OIC
aliwataka viongozi hao kukubaliana na suala hilo kwa vile zipo faida nyingi ambazo nchi itapata na kutaja mojawapo kuwa jumuiya hiyo inazo fedha nyingi hivyo itawasaidia kutatua matatizo waliyonayo.

Membe alizitaza baadhi ya nchi akidai kuwa zimenufaika na OIC na kusisitiza kuwa kujiunga nayo hakuna masharti ya kuigeuza nchi kuwa ya Kiislamu bali ni kuwa na idadi ya waislamu wasiopungua asilimia 60.

Alikaririwa akidai kuwa serikali haina udini na kwamba kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi hakutaibadili nchi kuwa ya kidini na kubainisha kwamba katika utawala wa Kikwete amekuwa akipambana na ufisadi kinyume na inavyoelezwa na watu.


Kutokana na maelezo hayo ya Membe, kilifika kipindi cha viongozi hao kueleza ya kwao ambapo mchungaji mmoja alianza kuzungumza kwa kutumia msemo wa Biblia kuwa kauli anayoitoa Membe kumsemea Kikwete wakati huu wa uchaguzi ni sawa na ‘Sauti iliayo nyikani' na kutoboa kuwa Membe hakupaswa kuyaeleza yeye bali Kikwete.

"Hapa tunasikia sauti inalia nyikani, sasa hatumuoni mtu anayelia, wakristo tunataka kumsikia yeye mwenyewe na siyo kutuma mtu bali aseme yeye kwa kinywa chake hadharani kuwa Tanzania hakuna udini na nchi haitajiunga na OIC." alisema mchungaji mmoja akimueleza Membe.


Kwa upande wa mafisadi mmoja wa viongozi hao wa dini walikaririwa akimuuliza iwapo ana dhamira ya kupambana na ufisadi ni kwa nini ameweza kusimama hadharani na kuwashika mkono akiwaombea kura baadhi ya watuhumiwa, ambao serikali yake imewafikisha mahakamani huku akitolewa mfano wa nchi ya Malawi ambako waziri mmoja amefilisiwa na kukamatwa kutokana na ufisadi.


Mmoja wa viongozi hao wa dini alimtahadharisha Membe kuwa anapaswa kutambua kuwa Watanzania wa sasa siyo sawa na wale wa zamani na kwamba sasa anapaswa kuwajibu vyema wapouuliza.


Walisema iwapo anasema faida ya kujiunga OIC ni kwa ajili ya kupata fedha za kusaidia taifa na kuhoji taifa limeshindwa vipi kunifaika na raslimali zake kama madini kiasi cha kuhitaji fedha za OIC.

"Membe alisema mambo yote ambayo ameyazungumzia na kwao yamezushwa wakati huu wa uchaguzi na kubainisha kuwa wanaozusha ni kundi la waliokosa uongozi ndani ya CCM.

Hata hivyo, nje ya hoteli hiyo Membe alipotakiwa na waandishi wa habari kuzungumzia kikao chake na viongozi wa dini, alikataa na kuwakimbia ambapo alijikuta akiliacha gari lake na kuingia gari la mkuu wa mkoa wa Mwanza ambaye alimkumbusha kuwa hilo halikuwa gari lake na kurudi kuingia gari lake na kuondoka.


Naye Mwenyekiti wa Umoja wa dini na Madhehebu ya Kikristo, Charles Sekelo ambaye ni Askofu wa Kanisa la CECT, alipoulizwa kuhusuna na kikao hicho alikiri kuzungumza kwa mambo hayo na kueleza kwamba Membe alidai alikuwa akimsafisha Kikwete kutokana na kuvuma kwa mambo machafu.

"Kwa maneno yake Membe alisema maduhumuni ya kikao chake nasi ilikuwa ni kusafisha juu ya mambo hayo, alidai yameuwapo mambo mengi mchafu ya kumchafua Kikwete na CCM, na kumbe alikuja kusafisha." alieleza Askofu Sekelo.


Kwa upande wake Mwakilishi wa Kanisa la Anglikana katika kikao hicho, Geoffrey Salum alisema, Membe alikuwa akijaribu kuwashawishi viongozi hao kujenga imani na serikali.


"Membe hajafanikiwa kutokana na msimamo wa viongozi wa dini ulivyokuwa ndani ya ukumbi huo, kwani ameshindwa kukidhi haja ya maswali yao na diyo maana wengi wamemweleza wazi kuwa wanataka Kikwete mwenyewe akiri hakuna udini nchini," alieleza Salum.

Hata hivyo, Mchungaji David Emanuel wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, alisema katika kikao hicho wametoa dukuduku lao na kueleza wazi kuwa hawaafikiani na serikali yake.
 
U
Ingawa Membe alikanusha Tanzania haijafikia uamuzi wa kujiunga na OIC aliwataka viongozi hao kukubaliana na suala hilo kwa vile zipo faida nyingi ambazo nchi itapata na kutaja mojawapo kuwa jumuiya hiyo inazo fedha nyingi hivyo itawasaidia kutatua matatizo waliyonayo.

Membe alizitaza baadhi ya nchi akidai kuwa zimenufaika na OIC na kusisitiza kuwa kujiunga nayo hakuna masharti ya kuigeuza nchi kuwa ya Kiislamu bali ni kuwa na idadi ya waislamu wasiopungua asilimia 60.

Alikaririwa akidai kuwa serikali haina udini na kwamba kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi hakutaibadili nchi kuwa ya kidini na kubainisha kwamba katika utawala wa Kikwete amekuwa akipambana na ufisadi kinyume na inavyoelezwa na watu.


Kutokana na maelezo hayo ya Membe, kilifika kipindi cha viongozi hao kueleza ya kwao ambapo mchungaji mmoja alianza kuzungumza kwa kutumia msemo wa Biblia kuwa kauli anayoitoa Membe kumsemea Kikwete wakati huu wa uchaguzi ni sawa na ‘Sauti iliayo nyikani' na kutoboa kuwa Membe hakupaswa kuyaeleza yeye bali Kikwete.

"Hapa tunasikia sauti inalia nyikani, sasa hatumuoni mtu anayelia, wakristo tunataka kumsikia yeye mwenyewe na siyo kutuma mtu bali aseme yeye kwa kinywa chake hadharani kuwa Tanzania hakuna udini na nchi haitajiunga na OIC." alisema mchungaji mmoja akimueleza Membe.
Hivi hata baada ya miaka mitano kupita bado Dk Salim A Salim anaandamwa! Dhambi hii hukumu yake itakuwa mbaya sana. Membe ni mnafiki na tena ni mdhaifu mno,kadanganywa na ahadi ya urais 2015. Kama amenukuliwa sawasawa,basi yeye ndo mchochezi wa hicho kinachoitwa udini,anajaribu kutafuta huruma kwa kuleta uchonganishi.

Issue ya udini hajui kuwa ni planted na inapata back up ya Ngombale,ili iwasaidie kurudi madarakani! Sioni wasiwasi wao uko wapi kwa vile sijasikia viongozi wa dini wakitaja rais anayetakiwa anatakiwa awe wa dini fulani,ila wao waliainisha kwenye waraka ambao haukutaja dini,huu wasiwasi uliopo wa kutokubali mabadiliko ndo hatari kwetu kuliko hata huo udini.
 
HABARI za Uhakika ambazo nimepokea Punde kutoka kwa viongozi wa Dini jijini Mwanza ni kuwa Baada ya Bernaed Membe kujaribu kuzungumza na viongozi wa dini na madhehebu ya Kikristu na kushindwa kuwabadili, leo Usiku saa 5:00 Kikwete atakutana na viongozi hao kwa siri na kuwabembeleza kumchagua na kumpigia kampeni kwa waumini wao.

Eneo la kikao hicho mpaka sasa hawajaambiwa, lakini Utaratibu uliopangwa watakutana kwa makundi ambapo kundi la kwanza litakuwa ni;
1. Maaskofu tu
2. Wachungaji

Maendelea kukatuma Ka INZI kufuatilia kwa ukaribu zaidi na kujua jinsi ambavyo mzee atajitetea kwao kuomba wamchague na wakawaambie waumini wao.

Amechelewa. maana hakuna ibada tena mpaka Jpili. Wengine wameahirisha ibada. hapo amechemsha. hata timing hajui
 
Kwa taarifa yako maaskofu wengi hawapo kanda ya ziwa wako Mbeya leo wanaadhimisha jubilee ya askofu wa RC JIMBO LA mbeya misa ndo imekwisha sasa hivi.Wale wako bussy na mambo ya kichungaji wanaokoa kondoo wao.Hawadanganyiki

Bwana mzee unatakiwa kutoa data zisizo na mashakamashaka. Askofu wa Jimbo Katoliki Mbeya ni Evaristo Chengula. Amezaliwa mwaka 1941 na hadi sasa ametimiza miaka 69. Amepata upadri mwaka 1970 na hivyo leo anatimiza miaka 40.03 ya upadri. Amepata uaskofu February 1997 hivyo hadi leo ana miaka 13.73 ya uaskofu.

Diocese ya Mbeya ina hadhi ya jimbo tangu mwaka 1953 na hivyo hadi sasa ina miaka 57. Popular Jubilee ni Silver, Golden na Diamond ambayo huchukua interval ya miaka 25.

HIvyo tulitegemea iwe ni Jubilee ya miaka 25, 50 au 75 ya kitu chochote kati ya nilivyotaja. Je, hiyo jubilee yako ni ya nini?

Kwa taarifa yako askofu wa D'Salaam yaani Polycarp Pengo hayuko huko Mbeya kwani ana mwezi mzima yuko Vatican.

Hebu tupe usahihi kama ulikosea kwa kuwahi kutuhabarisha.
 
Mbona amechelewa kukutana nao, ibada c huwa inakuwa J'pili, sasa anategemea watakutana na waumini lini kabla ya uchaguzi? Ni vyema angekutana na wale wa Ijumaa manake ndio watapata muda wa kutafakari kwa kina...

Umenifurahisha sana ndugu yangu. Ni kweli kabisa akutane na ma-bishop na wachungaji leo ili ndio iweje, Na hiyo siku yakukutana na waumini ndo siku ya kumtia JK kwenye kikaango wale nyama:)
 
Dah... huu ndio udini sasa!!! Keshamalizana na waislamu sasa ananunua wakristu

halafu analaani udini

Tutafanya zaidi... mkinipa rishaa yenu

Ana wasiwasi wa nini mbona Moses Kulola alishamfanyia kazi yake. Awahi kusikilizia Bagamoyo
 
Mkuu inawezekana vipi awe na peace of mind? Jana kuna mdau amesema alienda kwa Sheikh Yahya na kuondoka na furushi lisilojulikana, na sasa anataka kwenda kwa maaskofu na wachungaji, can 2 real work together in one persons mind? si rahisi naona itakuwa ni pieces of mind na sio Peace of mind.

Mimi namshangaa sana JK na timu yake wanapowalaumu viongozi wa dini kwa kuwa tu wametumia haki yao ya kikatiba kutoa maoni ya kutofautiana naye ...kama WALIVYOTUMIA HAKI YAO YA KIKATIBA KUMUUNGA MKONO MWAKA 2005...MKUKI KWA NGURUWE???

MYTAKE IS :- JK ALIFANYA KOSA SANA KUTUMIA VIONGOZI WA DINI MWAKA 2005 WAMFANYIE KAMPENI...NI WAZI INAWEZEKANA KUNA MAKUBALIANO ALIFANYA NAO AMBAYO HAKUYATEKELEZA NDIO MAANA WAMEMTUPA MKONO SAFARI HII..................TUWAACHE VIONGOZI WA DINI MAKANISANI NA MISIKITINI!!!
 
Dah... huu ndio udini sasa!!! Keshamalizana na waislamu sasa ananunua wakristu

halafu analaani udini

Tutafanya zaidi... mkinipa rishaa yenu

Hapo kwenye bold mkuu inanikumbusha pale jangwani japo inatia huruma........ Tutafanya zaidi .... mkinipa rishaa yenu ........ aiseeeee....tutafanya zaidi....tutafanya zaidi.........

Hakika Mungu hapendi unafiki.

 
Back
Top Bottom