Baada ya matokeo ya Igunga, CUF itoe tamko rasmi kwa wanachama wake

Umeandika hii article bila ya uchambuzi wa ukweli. CUF ina mafanikio zaidi ktk vyama vya upinzani. Angalia Wabunge waliokuwa nao, na sasa hivi wanayr Makamu wa Rais.

Sasa huoni kama hiyo ni progress?
mkuu nahisi una faili lako pale milembe hospital
 
Napenda sana demokrasia na sina chama chochote hadi sasa,hakuna aibu kubwa iliyowahi kuvunwa na CUF kama uchaguzi wa Igunga,kama viongozi wake wangekuwa na maon wasingeshiriki uchaguzi huo,ni biashara gani kama sio ya ukichaa inayokula mtaji wote?mtaji wao wa kura elfu 10 umeota mbawa.Kwa maoni yangu kuna mambo kadhaa ambayo yamechangia: CUF ni chama chenye muonekano wa kidini-Wabunge na viongozi wote wa CUF kasoro Mtatiro ambaye naye ana SIJIDA wote ni waislamu,CUF kwa bara kinaonekana kama ni cha Kizanzibar na kitendo cha wabunge wa CUF wa ZANZIBAR kuja Igunga pia kimeipunguzia kura.CUF hawana sera zenye mvuto zaidi wanaonekana kama wapo kwa ajili ya kuisupport CCM yaani ni dhahiri wao ni CCM-B,
Ni bora CUF wajiondoe bara kwani wanapoteza muda wao bure ,pamoja na gharama zote na helicopter bado wwameumbuka hivi,ni bora CUF kibaki kuwa chama cha Zanzibar.
 
Umeandika hii article bila ya uchambuzi wa ukweli. CUF ina mafanikio zaidi ktk vyama vya upinzani. Angalia Wabunge waliokuwa nao, na sasa hivi wanayr Makamu wa Rais.

Sasa huoni kama hiyo ni progress?

swala sio wabunge walionao,,point ni kuwa:CUF ile ya 1995;2000;2005 sio sawa na hii ya leo kwani haiko pinzani kwa chama tawala kama awali,inashuka umaarufu na pia namba ya viti bungeni inapungua kila kukicha.
Ili kukinusuru chama,,ni lazima kufanyike mageuzi makubwa kwenye uongozi wake,,sisemi nani aondoke,maana chama chenyewe kinajua wazi ni akina nani inabidi wang'atuke kwa manufaa ya chama.
 
Cuf, ilipojitangaza kipindi kile kuwa ni ngangari kilionyesha ni chama mbadala kinachoweza kusimamia utajiri wetu, kumbe walikuwa ngangari kwa tamaa, haikuwa na haja ya kukubali ndoa na ccm kisa watapata nafasi ya pili, matokeo ni kusababisha baraza kubwa la mawaziri na gharama kubwa katika uendeshaji wa zanzibar. Wale waliopigwa january 27 2001, wale wananchi walioandamana ili kutafuta haki na usawa damu iliyomwagika ni kwaajili ya seif apate umakamu na baadhi wapate uwaziri.

Hiki sio chama na hii yote ni kutokana na chama kuwa na sura ya kumuangalia mtu mmoja kwa matumaini, seif alisha sema kama ccm watanipa uenyekiti wa chama nipo tayari kurudi !, sasa prof lipumba anachokifanya cuf sikielewi anatakiwa asome alama za nyakati other wise atafulia kama mrema ila chdema tuna watu makini wengi na wenye uwezo zaidi na wanakubalika na wananchi wengi. Yaani 2015 ni raaaaaha

Lipumba hatumtaki hata bure!!!
 
Kisa cha Majuha wawili wanawake! Akili za kushikiwa utazijua.
Tumepata mbunge wa 49 Mheshimwa Kashindye!
Chadema hoyeee!!
 
CUF ilishapoteza nafasi yake kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya kukubali kuvishwa pete ya ndoa na ccm huko Z'bar! Pia suala la kuendekeza udini nalo linaitafuna CUF! Watanzania kwa ujumla wao sio wadini na wala hawabaguani kwa misingi ya kidini maana katika koo na jamii zetu tumechanganyikana katika dini zote. Unakuta mama mkristu, mjomba muislamu, baba muislamu lakini shangazi ni mkristu! Udini unaletwa na wanasiasa!
 
Back
Top Bottom