Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
Chama cha Wananchi CUF, kinawiwa na wanachama wake tamko mahsusi kuwa ni nini hatma yake kwa sasa. Uchaguzi wa Igunga unafanyika katika mkoa ambao anatokea mwenyekiti wa chama, pamoja na mbunge wake wa viti maalumu. Kwa nguvu waliyoiweka CUF ikiwemo kumleta makamu wa raisi wa SMZ, wabunge, viongozi waandamizi na bila kusahau kutumia helicopter, naamini matokeo ya leo is the best thay can expect kwa uchaguzi wowote utakaofanyika Tanzania bara.
Vipo vyama vilivyowahi kuvuma na kuporomoka kikiwemo NCCR-mageuzi. Tofauti na CUF, sababu za kuporomoka kwa vyama hivi ilikuwa wazi, hususani migogoro ya uongozi na ukata. Ila kwa CUF, sababu ya kuporomoka kwake haiko wazi; uongozi ni ule ule, ruzuku imeongezeka, tena wamepewa na sehemu ya serikali kule Zanzibar. Tulitegemea CUF kionyeshe kuaminika zaidi na wananchi, hivyo kiwe chama kikuu cha upinzani!!!
Sio siri, ni halali yao wanachama na wapenzi wote wa CUF kupata maelezo ya kina, ni kwa nini chama hakifanyi vizuri...
Kwa heshima na taadhima, namwomba ndugu Julius Mtatiro pia atoe maoni yake juu ya matokeo ya Igunga, na juu ya mustakabali wake kisiasa. (Ingekuwa heri leo asikie sauti ya wananchi, asifanye mgumu moyo wake).