Elections 2010 Baada ya Kuzomewa Kikwete apanda Hasira; Atamka Atashinda kwa Kishindo

chanzo cha habari yako ni nini? Kama huna source huna haki ya kuandika!!! Kama wewe ni msomi utanielewa lakini kama wewe ni mfurukutwa au vinginevyoo ruksa!!!

Usikariri hata yeye personally anaweza kuwa source!!!!
Unajua maana ya usomi wewe?
 
USHABIKI MWINNGINE UNAONDOA HATA MAANA YA HABARI

tulivyosoma kwenye vynazo husika (kama ni bukombe) ni kwamba walimwambia watampa kura za rais na diwani lakini si ubunge... sasa sielewi haya mengine yanatoka wapi
 
kikwete kesha panga kuiba kura? mbona sishangai! alafu mbona anatetemeka ivyo? majini yanapanda au vipi?
 
hiyo kauli kaitoa kwa kujua kuwa ni lazima tu wataiba kura hata kwa kumwaga damu, si ndio zao ccm
 
Niliwahi kuuliza hawa CCM wanategemea kura za nani ili washinde wakati wafanyakazi walipoambiwa kuwa kura zao mwenyekiti wao hazihitaji na sasa kwenye midahalo ambako wananchi wanataka kujua nini watafanyiwa hawataki kwenda sasa nani atawapigia kura za kushinda kwa kishindo?

FAMILIA YAKE itampigia kura kwa KISHINDO maana hiyo ndiyo inayo msaport
 
Hivi nani huwa anatumika kuchakachua matokeo! maana hawa washashi wameshashindwa,nani huwa anachakachua abanwe,tutaendelea hivi mpaka lini?
 
Naombeni tusubiri wana JF kwa nini kubishana na mtu aliyechanganyikiwa??utaonekana na wewe umechanganyikiwa kama yeye.Mwamuzi wa haya ni October 31.kwa wale watakaobahatika kufika maana yule mlinzi wao 'sheikh" alishatabiri mengine.
 
Source: Habari leo

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia CCM, Emmanuel Luhahula ameonja joto ya jiwe baada ya wananchi kumkataa mbele ya Mwenyekiti wake wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa kampeni.

Luhahula anayeomba tena ridhaa ya kuongoza jimbo hilo la wilayani Bukombe mkoani Shinyanga, alijikuta akizungumza huku akizomewa kwa kupigiwa miluzi na wananchi juzi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Igulwa Mjini Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Shinyanga.

Kwanza alikutwa na dhahama hiyo wakati akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2005-2010 na hata alipotambulishwa kwa wananchi hao na Rais Kikwete, bado hakukubalika.

Kwa kusoma hali ilivyokuwa uwanjani hapo, Rais Kikwete aliwauliza wananchi hao kama wanamkubali awe Rais wao, walimjibu "Ndiyo", lakini wakasema "Hapana" kwa Luhahula aliyeongoza katika kura za maoni ndani ya CCM.

Hata hivyo, mshindi wa pili katika kura hizo za Agosti mosi, mwaka huu, Profesa Kulikoyela Kaige, aliihama CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ndiye mgombea wao wa ubunge.

Wakati wote akisoma utekelezaji huo wa Ilani ya CCM, Luhahula alikumbana na kelele za wananchi hao zilizotokana na kuzomea na kupiga miluzi huku wakionesha ishara ya vidole viwili hewani, alama inayotumiwa na Chadema.

Hata Luhahula alipopewa fursa ya kuwasalimia wananchi baada ya Rais Kikwete kumaliza kuzungumza, hali ilikuwa ile ile ya kumkataa mbunge huyo aliyeingia madarakani mwaka 2005.

Alitumia muda huo kuwatambia wananchi hao waliomkataa kwa kusema, "najua wanaoninyooshea mikono, watakuwa wa pili, Luhahula atakuwa wa kwanza katika uchaguzi.

Ushindi wa CCM ni lazima."
Awali, katika hotuba yake, Rais Kikwete aliwaponda wanachama wa CCM ambao baadhi yao baada ya kushindwa kura za maoni hukimbilia vyama vya upinzani, akiwafanan isha na wanafiki.

"Maisha yako yote uko CCM, siku ulipokosa uteuzi unakuwa kada wa chama kingine, unafiki mtupu," alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa CCM bado ni chama imara kuliko vya upinzani.

Alifafanua kuwa CCM haisumbuliwi na kuwepo kwa vyama vya upinzani, kwa sababu ni Serikali ya CCM iliyoamua kupitisha uamuzi wa kuwa na mfumo wa vyama vingi nchini, licha ya asilimia 80 ya Watanzania kukataa.

"Hawa waliopo leo wasingekuwepo kama siyo CCM, serikali inayoheshimu haki za raia kuchagua chama unachokitaka. Uhuru huo ni CCM ilitoa. "Hiyo ni hekima ya CCM.

Asilimia 80 wana imani na Chama Cha Mapinduzi. Asilimia 20 ndio wapinzani.

Wala msihangaike, hilo halitusumbui, tuliamua wenyewe muwepo, kwa hiyo mkiwepo, haitushangazi," alisema Rais Kikwete na kushangiliwa na maelfu ya wakazi wa Bukombe mkutanoni hapo.

Hata hivyo, aliwaomba kuendesha siasa bila fujo akisema, "hata kama una mbunge wako, kwa sasa Mbunge ni Luhahula, na tarehe 31 atashinda na kitakachomfanya ashinde ni mafanikio aliyoyaeleza hapa."

"Tumeanza mipango ya kuhakikisha umeme unafika Bukombe, mchakato wake unaanza Novemba, hakuna wasiwasi.

Tupeni miaka mitano tufanye vizuri zaidi. Wananchi wa Bukombe wasihangaike, hivi vyama vingine vinapita," alisema mgombea huyo wa urais wa CCM.


Kwa mujibu wa duru za siasa wilayani Bukombe, kuna mgawanyiko miongoni mwa wananchi kuhusu wagombea ubunge uliojikita katika suala la ukabila miongoni mwa wagombea hao wawili; Luhahula na Profesa Kaige.

Salma Kikwete aifananisha CCM na mwembe Na Mwandishi Wetu MWEYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, amekifananisha Chama Cha Mapinduzi na mwembe ambao hurushiwa mawe kutokana na matunda yake.

Amesema wapinzani wanaisema CCM kwa sababu imefanya mambo mazuri kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na taifa baada ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005-2010.

"Ukiona wapinzani wanaisema sana CCM, ujue imefanya mambo mazuri, ni sawa na mwembe wenye matunda hupigwa mawe, kwani umeshaona mwembe usio na matunda ukipigwa mawe?" Alihoji.

Mama Salma alisema hayo jana na juzi kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Mkoa wa Mtwara.

Kuhusu uchumi, alisema uuzaji wa mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ni ukombozi kwa wakulima dhidi ya walanguzi.

Taarifa iliyowasilishwa kwake ilieleza kwamba, uuzaji korosho kwa mfumo huo umewanufaisha wakulima ambapo hulipwa malipo kwa awamu mbili hadi tatu kulingana na bei ya soko.

Ilieleza kwamba, wakati Serikali ya Awamu ya Nne inaingia madarakani, kilo moja ya korosho ilikuwa ikiuzwa kwa kati ya Sh 150 hadi Sh 300 na kwa sasa ni Sh 800 hadi Sh 1,000 baada ya uanzishwaji wa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani.

Mama Salma alisema wanaoupinga mfumo huo, wanataka kuendelea kujitajirisha kwa jasho la wakulima kama ilivyokuwa huko nyuma.

"Msidanganyike, uuzaji wa mazao kwa stakabadhi ya mazao ghalani ni ukombozi kwa wakulima, na Serikali ya CCM inawapenda haiwezi kuwadhulumu ndio maana inasisitiza na kusimamia mazao kuuzwa kwa vyama vya ushirika," alisema na kupigiwa makofi na vigelegele.

 
Kaimu Raisi Wa jamhuri ya serikali ya tanzania bara Mh RIZIWANI JAKAYA MRISHO KIKWETE
Amenusurika kupigwa kichapo pale alipoingizwa mkenge kutaka kutumia ukumbi wa shule kwa manufaa ya kampeni za ccm hali ikipingana na sheria za NEC

Hali hiyo iliotokea pale vidume wa chadema waliposikia hilo dili na kwenda moja kwa moja shulen huku wakishangaa magari yakiingia na bendera zikipeperuka kama kunguru wa zanziba ndipo ilipofika wakati mh sana riziwani alipowasili na hapo kkundi la vijana wakiwa kama 70 TU wakamfwata mkuu wa shule na kumuuliza RIZIWANI KIKWETE NI NANI kaja kama nani na anakuja kufanya nini shulen...na kwa nini umeamuru watoto wetu ikifika muda fulan waondoke mapema kisa upuuzi wa CCM

Sasa kama walikudanganya leo mkutano aufanyiki semina aipo...labda watafute jina lingine la kutufanya tuwaachie..ndipo akashuka mtu mmoja kutoka kwenye gari la mh KAIMU RAIS WETU RIZIWAN KIKWETE NA KWENDA KUELEZA awakuja kwenye kampen bali ni kikao cha kusuluisha ugomvi kati ya MWAKALEBELA NA MGOMBEA MBUNGE B MBEGA...lOH waliposikia mbega wakahisi kichefu chefu kama wamekunywa VALUE na kumuamuru mwalimu mkuu asiwardushe watoto kabla ya wakati na Hakuna kikao wala kampeni wala usuluhisho wowote utakaofanyika hapa wakasuluhishane makao makuu sio hapa...

Ilikuwa ni aibu ya ajabu ndipo kwa upole msafara ukiongozwa na mgombea ubunge bi mbega ukaanza kuondioka kwa masikitiko na kushukuru mungu huku akiangalia nyuma kweli wamesalimika ama macho yake

WAZO LA BURE

RIZIWAN HESHIMU MAMLAKA NA SHERIA YA NCHI..BABA MWENYEWE AYUKO JUU YA SHERIA ..HATA KAMA ANAFANYA KAMPEN MPAKA SAA MOJA USIKU KINYUME NA MAELEKEZO YA NEC..SO USIMWONE MZEE KACHEMSHA NA WEWE UNAAMUA KUMFWATA..LEO HII KA SIO CHULE HAYOYOTE USINGEYAJUAA..UNA MAMLKA GANI KUWAAMRISHA WATOTO WETU WAACHE SHULE MAPEM KUJA KUKUSIKILIZA NARUDIA ACHA KWA MSISITIZO KOMA...TUACHIE NCHI YETU MSITUARIBIE VIJANA WETU HATA KIDOGO
 
jinsi ccm wanavyoendesha mikutano yao ya kampeni wanastahili more than kuzomewa. Kukusanya watoto wa primary ambao hata hawana umri wa kupiga kura!!! Means wao hawajui umuhimu wa elimu. Lol!

Mikutano imejaa ubabe, ulaghai, ufedhuli, unafki, wizi wa fedha za wtz (ufujaji) uongo, hila, point less na upupu mwingiiiii. Wamezomewa ila kwa mimi nikiwaona i am sure nitachemsha maji ya moto niwamwagie cause wanaboa sanaaaaaaaaa!!! Ole wao wapitie anga zangu..
mimi ni mtetezi wa haki za watoto .nipeni data nimburuze kizimbani kabla ya 31 oct
 
USHABIKI MWINNGINE UNAONDOA HATA MAANA YA HABARI

tulivyosoma kwenye vynazo husika (kama ni bukombe) ni kwamba walimwambia watampa kura za rais na diwani lakini si ubunge... sasa sielewi haya mengine yanatoka wapi
acid, siku ile bukombe alipanda jukwaani, mgombea ubunge wa ccm , wakamzome, akapanda mwenyekiti akamkaribisha jk, jk akamwita yule mgombea ubunge, ili amkapenie tena, ndipo wananchi wakaaanza kumzomea huku wakionyesha ishara ya chadema.
 
Yaani ingekuwa mimi ndio JK nisingepanda jukwani kwenye kampeni ninge mwachia balali afanye
 
lakini jana aliongeza kuwa "wachache wape?!":mad2:
So mwaka huu hata mkimchagua Slaa, CCM watapata kura chache lakini ndio wanataka watangazwe. Mwenyewe anajua kuwa hawezi kushinda.

Kwa wageni wengi ambao wamejiunga JF wiki hii ambao ni wengi, jueni kuwa Watanzania wako tayari kufanya mabadiliko. Ninyi msibaki nyuma.

Mafanikio ya Jk haya hapa chini kwa wageni ambao hawamjui





CHAGUO LA MUNGU: "Mafanikio" ya Kikwete 2005-2010 Katika Picha.

1689bp1.jpg
UBISHI TUUU: HUU UTITIRI WA MASHANGINGI SIO UTHIBITISHO WA MAISHA BORA?SASA HIYO NI AWAMU YA KWANZA.AWAMU IJAYO NI BAJAJ KWA WAJAWAZITO NCHI NZIMA

Maji+1%5B1%5D.jpg
MAJI BWERERE

MAISHA+BORA.jpg
MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YAMEWEZEKANA

HURUMA.jpg
USHAHIDI WA MAISHA BORA UNAONEKANA HATA KWA WATOTO WADOGO

ADHA+YA+MAJI.JPG
YOU SEE, TATIZO LA MAJI MIJINI NA VIJIJINI LIMEPATIWA UFUMBUZI WA KUDUMU

USAFIRI+WA+WANAFUNZI.jpg
TATIZO LA USAFIRI KWA WANAFUNZI MIJINI LIMEMALIZWA.MNATAKA MAISHA BORA YAPI ZAIDI YA HAYA?

POLISI+MSIMBAZI.jpg
MNAONA?POLISI WENYE MAKAZI DUNI SASA WANA SWIMMING POOL HAPO MSIMBAZI POLICE FLATS.MAISHA BORA KWA POLISI YAMEPELEKEA WAACHE KUDAI RUSHWA NA KUBAMBIKIZA KESI KWA WALALAHOI

zjgfo4.jpg
KURA ZA ALBINO ZIMEZAA MATUNDA.HUYO MGOMBEA WA CCM WANAYEDAI NI MTUHUMIWA WA BIASHARA YA VIUNGO VYA ALBINO NI SIASA ZA MAJITAKA TU

25p4yv6.jpg
HATA SUPAMODO NAOMI CAMPBELL ALIPOTEMBELEZA TANZANIA ALIRIDHISHWA NA HALI ALIYOKUTA WODI YA AKINAMAMA.NA AKATOA MACHOZI YA FURAHA

MATREKTA+KILIMO+KWANZA.JPG
BARABARA ZETU NI MARIDADI.TUMELETEWA MATREKTA MENGI MNO KWA KILIMO KWANZA HADI INABIDI YAFANYE KAZI YA KUVUTA MALORI.EBO!KWANI CHA AJABU NINI TREKTA KUVUTA LORI?NI FERI ZA NCHI KAVU HIZO

MATOPE.JPG
CHAGUA KIKWETE NA CCM KWA BARABARA BORA.NA 2010-2015 BARABARA KAMA HIYO HAPO JUU ZITAKUWA UPGRADED TO FLYOVER.

ELIMU+CHINI+TENA.jpg
SERIKALI YA KIKWETE IMEWAJALI SANA WANAFUNZI NA KUWANUNULIA MADAWATI BORA MNO HADI YANAWACHOSHA KUYAKALIA NA KUAMUA KUKAA SAKAFUNI

KIBANO+UDSM.jpg
HAPANA.KOSA LA MSOMI HUYO WA CHUO KIKUU ANAYEFUKUZWA NA FFU NI KUGOMA KUCHUKUA HELA ZA KUJIKIMU ZILIZOINGIZWA KWENYE AKAUNTI YAKE KABLA HAJAWASILI CHUONI.HAPO ASKARI WA FFU ANAMHAMASISHA MSOMI HUYO AENDE BENKI.CHAGUA KIKWETE USOME KWA RAHA MUSTAREHE

elimu+chini+.jpg
NDIO MAANA RAIS MPENDWA JAKAYA KIKWETE ALISEMA MIMBA ZA WANAFUNZI NI KIMBELEMBELE CHAO TU.ANGALIA MWENYEWE MAZINGIRA BORA KABISA YA NAMNA VIJANA WETU WANAVYOPATA ELIMU.KIKWETE OYEEE

kikwete+na+pipi.JPG
BAADA YA MABILIONI YA KIKWETE,NA KAGODA KUREJESHA MABILIONI,SASA MAISHA BORA NI KWA MWENDO WA PIPI KWA KILA MTOTO.YAH,PIPI KWANZA KISHA LAPTOP KWA KILA MWANAFUNZI.HALAFU HUYO SLAA ANAPOSEMA ATATOA ELIMU YA BURE KWANI MIE NAUZA HIZI PIPI?

Jakaya-safarini-218x300.jpg
SAFARI MOJA HUANZISHA NYINGINE.KWANI MLIPONICHAGUA MLITAKA NIOTE MATENDE IKULU?

rostam_1.jpg
MFANO HAI WA AMANI NA UTULIVU

SAFARI+MOJA.JPG
ZAPATERO ANAELEKEA KUSHANGAA: HIVI KAMA HUYO JAMAA ANA MAWAZO YA HALI YA JUU KIASI HIKI KWANINI BADO NCHI YAKE NI MASIKINI?NO,HAPO KIKWETE ANAHUBIRI KUHUSU CHANZO CHA UMASIKINI WA AFRIKA JAPO HAFAHAMU KWANINI TANZANIA NI MASIKINI

AKINAMAMA.JPG
AKINAMAMA WAMEPEWA KIPAUMBELE CHA HALI YA JUU KATIKA MIPANGO YA SERIKALI YA KIKWETE.PICHA INAWAONYESHA KAMA WANA MAJONZI LAKINI UKWELI NI KUWA WAMESHIKWA NA BUTWAA KUTOKANA NA KAZI NZURI YA CHAGUO LA MUNGU KIKWETE



TwinTowers.jpg
MMENG'ANG'ANIA TU SUALA LA EPA NA KAGODA NA KUSAHAU MINARA PACHA.BY THE WAY,FEDHA ZA EPA HAZIKUIBWA BALI ZILIAZIMWA TU,NDIO MAANA NILIWASIHI TULIOWAAZIMA WAZIREJESHE.WALIOAZIMWA WANAREJESHA IN KIND KWA KUCHANGIA KAMPENI ZA CCM

Richmond.jpg
TEH TEH TEH,NICHEKE MIE.KIKWETE MTU BOMBA SANA.SIE TUMEKUJA NA KABRASHA TUPU LEO HII TUNA MABILIONI KWENYE AKAUNTI.ASANTE DOWANS KWA KUTURITHI,ASANTE KARAMAGI NA MSABAHA.ASANTE WATANZANIA KWA KUMWAMINI KIKWETE.SI MNAONA SASA TATIZO LA UMEME NI HISTORIA KAMA ALIVYOAHIDI CHAGUO LA MUNGU KIKWETE?

regina.jpg
MWAKYEMBE NA TUME YAKE NI ROHO MBAYA TU.KAMA MUME WANGU LOWASSA ALIHUSIKA NA UFISADI WA RICHMOND MBONA KIKWETE AMEKUJA JIMBONI KUMPIGIA DEBE?

lowassa.jpg
TATIZO LENU WATANZANIA MNA KUMBUKUMBU HAFIFU.MMESAHAU ENZI ZA Boyz II Men?MIE NA JAKAYA HATUJAFAHAMIANA MTAANI.MNABISHA?SI MMEONA JINSI MAJUZI ALIVYOMWAGIA SIFA JIMBONI MONDULI?


SAFARI+ZAIDI.JPG
MNASEMA NASAFIRI SANA?KWANI MLIPONICHAGUA MLIKUWA HAMFAHAMU KUWA NILIPOKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NILIKUWA NASAFIRI SANA?ACHENI UZUSHI,SAFARI ZANGU ZITAILETEA TANZANIA SIFA YA KUVUNJA REKODI YA VASCO DA GAMA.

Bartlett+with+Jakaya+Mrisho+Kikwete+and+wife+at+Mystic+Mountain.jpg
MTAJIJU....ACHE MIE NIBEMBEE

KIKWETE+MWANAE.jpg
JIJENGE HUKO UVCCM.SI UMEONA FAMILIA YA BUSH ILITOA MARAIS WAWILI KAMA YA KABILA HUKO DRC?BASI NA WEWE JIANDAE.MIE NAITWA CHAGUO LA MUNGU,WEWE UTAITWA CHAGUO LA BABA

JK+RIZI+WANI+CLASS.jpg
WE KATUNI HUELEWI SOMO LIPI TENA?YANI UNAKUWA KAMAMIE NISIYEELEWA KWANINI TANZANIA NI MASIKINI!

dance+kikwete.jpg
PICHA YA JUU NA YA CHINI: CHAGUO LA MUNGU DANCING.BY THE WAY "Never Trust a Spiritual Leader who cannot Dance".-Mr Miyagi,The Next Karate Kid,1994


MAKAMBA.jpg
HUYU SLAA ANATAKA KUNIWEKEA MCHANGA BADALA YA UBWABWA KWENYE SAHANI HII.HIZI HABARI ZA MIE KUFUKUZWA UALIMU ZA NINI TENA MUDA HUU?

Makamba+(1).jpg
WANAKUJA NA USHAHIDI NINI?WANATOKEA HUKU AU KULE?ANYWAY,HAWAWEZI KUTHIBITISHA LOLOTE

makamb.jpg
MGOSI,UNAKUMBUKA SIKU ZILEEEE KATIKA SHULE ILEEE...BASI SLAA KAINYAKA HIYO ISHU.







 
Kaka taratibu! Naelewa unavyojisikia ila wahenga walisema hasira hasara! Ushauri wangu kwako na kwa wengine wenye hasira: tuwahamasishe ndugu zetu, rafiki zetu, jirani zetu na wote WENYE MAPENZI MEMA, Tarehe 31/10/2010 tukamalizie HASIRA ZETU kwenye masanduku ya kupigia kura! Cha muhimu TUZILINDE KURA ZETU KABLA HAWAJAZICHAKACHUA hao mabazazi!!

Jinsi CCM wanavyoendesha mikutano yao ya kampeni wanastahili more than kuzomewa. Kukusanya watoto wa primary ambao hata hawana umri wa kupiga kura!!! Means wao hawajui umuhimu wa elimu. Lol!

Mikutano imejaa ubabe, ulaghai, ufedhuli, unafki, wizi wa fedha za Wtz (ufujaji) uongo, hila, point less na upupu mwingiiiii. Wamezomewa ila kwa mimi nikiwaona I am sure nitachemsha maji ya moto niwamwagie cause wanaboa sanaaaaaaaaa!!! Ole wao wapitie anga zangu..
 
Katika moja ya Mikutano yake kanda ya Ziwa, Rais anayeondoka madarakani Bwana Jakaya Kikwete alijikuta katika hali ngumu baada ya kuzomewa na wananchi pale alipotoa ahadi iliyotafsirika kama upupu kwa Watanzania.

Ninashauri kuwatendea CCM haki haya mapungufu ya kutojua eneo kwani JK amendea maeneo mengi kanda ya ziwa sasa hili ni lipi na ni lini. Maswali haya hayakujibiwa humu hivyo ni vyema ikaondolewa namhusika ajipange upya ila ajulishwe
 
Hivi ni kweli Makamba alibaka Mwanamke huko Kigoma? Sina habari za kuhakiki hii skandali.

Kama alibaka, je kuna utaratibu gani wa kumpa Dozi zake kwa mabaya aliyoyafanya huko kwa kina Zitto?
 
Back
Top Bottom