Baada ya kumkataa Rais

Kwenye red: nini tofauti kati ya National Assembly na Parliament? Tuwe tunasoma na kuelewa kwanza kabla ya kukosoa hoja ya mtu. Parliament kikao akiwemo na Rais na national assembly kikao bila Rais. Soma ibara ya 62 (1) na 63 (1) ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania (toleo la 2005).

akiwepo rais ni nani anakuwa kiongozi wa bunge kwa wakati huo?
Nafahamu kuna wakati bunge hukaa kama kamati ambapo kiongozi wake anakuwa termed kama m/kiti. Je rais anaweza kuwa kiongozi wa bunge kwa namna yoyote?
 
kwanza kabla ya yote rais wa Tanzania siyo mbunge, kwa kenya sawa, pili ili kuthibitisha hilo rais ataruhusiwa kuingia bungeni pindi tu katiba au mwongozo wa bunge utakapo vunjwa na kuafikiwa na wabunge wote,
hoja yako ya pili ninadhani huelewi vizuri siasa nahujui kuhusu bunge na wabunge, nani anaruhusiwa kuunda kambi ya upinzani, jaribu kwanza kusoma katiba na miongozo yake ndio uwasilishe hoja. wabunge wa chadema hawajachaguliwa na kikwete, wamechaguliwa na wananchi na wapo pale kutetea maslahi ya wananchi,
Tatu nimetambua uwezowako ni mdogo kweli kama ulivyotangulia kusema wewe unadhani siasa ni uadui sisi kama CHADEMA hatuendeshi siasa za uhasama na kusalimiana kwa Dr Slaa na pinda ndo kielelezo tosha kwamba tupo katika kutetea maslahi ya nchi ukijumlisha na pinda kwani naye ni mwananchi.
ANGALIZO:
kama ubongo wako ni wa mgando kimawazo usitumie kuwadanganya hata wale walioelimika, kaa kimya tuachie sisi tunayohitaji mabadiliko na tutayapata yatakusaidia wewe na watoto wako.

Ume-m-maliza!!!Kwishne!!

Akafie mbali huko.

Chadema kimejaa 'vichwa' baba.

Chadema hatufanyi mambo kwa kuunga-unga.
 
Bwana Sokomoko,mtu kupinga matokeo ya uchaguzi au kura alizopata Rais katika Tanzania kwa kutumia public forum au kutoa kauli kama aliyoitoa hakuna ubaya wowote kwa chadema kwani hiyo ndiyo option pekee waliobakiwa nayo,ingekuwa kama katiba inaruhusu kupinga mahakamani Dr.Slaa angeenda,ila kwa kuwa katiba yetu inasema kwamba MATOKEO YA URAIS YAKISHATANGAZWA HAYATAHOJIWA KATIKA MAHAKAMA AU CHOMBO CHOCHOTE KILE cha sheria. Kwa kipengele hicho hata kama mtu anayehsinda Urais awe alishinda kwa kuwalazimisha watu kumpigia kura au kuwakata mikono wote wanaompinga kama ilivyowahi kutokea Sierra Leone,bado kwa kipengele hicho cha katiba Rais huyo ni halali na ushindi wake huwezi kuupinga kokote.
Lakini je,tujiulize Rais huyo atakuwa ameshinda kihalali within the meaning ya uchaguzi huru na wa haki? Je, katika mazingira ya namna hiyo mtu ambaye anadhani ameonewa remedy yake ni nini? je,ajikunyate tu na kukaa kimya as if ameridhika au walau atoe KAULI inayyonesha kwamba JAPOKUWA MTU X AMETANGAZWA MSHINDI ushindi huo sio halali,kwa hiyo alichofanya SLAA ni kuprotest,kwani hata mahakamani ,mtu unaruhusiwa kuappear under protest. Yaani unajua kabisa kwamba wewe si muhusika katika hiyo kesi lakini unatii wito wa mahakama wa kuja mahakamani na kujibu maswali na unaiambia wazi mahakama kuwa unakwenda tu lakini wewe huhusiki hiyo wajue kabisa.
KWA hiyo hata kusema watafanya kazi na kikwete ni sawa tu lakini msg zent kwamba BWANA MKUBWA japokuwa umetangazwa mshindi lakini ujue ushindi wako si halali na kwakuwa hatuna cha kukufanya,hatuna jinsi isipokuwa kushirikiana na wewe na kukuheshimu ili kuepusha umwagaji damu. Pale ambapo ni lazima kushirikiana nawe itatubidi, mf.kusikiliza hotuba zako,kufanya kazi na bunge lenye mawaziri wako nk,ila mengineyo hatutakuja,hasira zetu zikiisha kabisa basi utaona tunashirikiana nawe tu bado kooni kwetu bado kuna vidonda.
HII ndio maana halisi ya kauli ya Dr.Slaa ama chadema kwa ujumla
 
siasa ni mchezo mchafu...............ktiba imewekwa ili kuwalinda ccm na wizi waliopanga kuufanya
 

Jamani,
Ni kweli hili tangazo la Chadema kuwa hawamtambui Rais, ambaye amechaguliwa na ametangazwa kikatiba, ni kichekesho cha mwaka na ni jambo la kitoto! Wabunge wenyewe wa Chadema wameapa kulinda Katiba ya Nchi, kama alivyoapa Rais ambaye Chadema wanasema hawamtambui. Je, wakati Rais msiyemmtambua anapokuja Bungeni, kikatiba, kuhutubia, Chadema mtakuwepo au mtatoka nje? Rais akileta jina la Waziri Mkuu ili athibitishwe na Wabunge, Chadema, watatambua kitendo hicho cha Rais wasiyemtambua anayetaka apate msaidizi wake, ambaye ni Waziri Mkuu? Waziri Mkuu mwenyewe, aliyeteuliwa na Rais (ambaye Chadema hawamtambui) na kuthibitishwa na Bunge, ndiye atakayekuwa kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni, je Chadema watamtambua? Watamuuliza maswali ya Papo kwa Papo? Mimi nadhani Chadema wangefanya vema kutomtambua Rais na kutotambua matokeo ya kura za Ubunge pia na wakatoka Bungeni! Humtambui Rais, lakini unatambua Bunge, ambalo sehemu yake, kikatiba, ni Rais. Acheni danganya toto! Na hawa waaandishi wetu wa Habari, akina Saed Kubenea, wameshindwa hata kumuuliza Mbowe na Slaa, "the legal implications and interpretation of this move". Wanaandika tu na kutuletea, kama kasuku! Slaa akisema, wanatuandikia tu, Mbowe akisema, wanatuaandikia tu, Mtikila akisema, wanatuandikia tu! Hamuulizi hata maswali? Jamani?
Bwassa

Katiba imelazimishwa kumtambua Jk.. Maana hata na yenyewe inamtambua raisi aliyetokana na wananchi na si vinginevyo... JK hayuko pale kwa mujibu wa sheria bali de facto(kwa kutumia nguvu na kubaka demokrasia)...
CHADEMA wana haki ya kutambua baadhi ya matokeo ya ubunge ndio maana mengine yako mahakamani tayari... Mimi nadhani kipengele cha kutotambua matokeo ya uraisi ndio kero hapa kifutwe halafu mengine tutaongea baadae... Kule jamaa wanachakachua lakini muhimili mmoja yaani serikali wamebaka mamlaka ya mahakama kwa kusema matokeo ya uraisi hayawezi kupelekwa mahakamani... Mimi nadhani siku raisi anasoma hotuba pale bungeni ni lazma CHADEMA watoke kuonyesha nia yao ya dhati... Lakini kama watakuwepo basi lazma watakuwa na njia yao mbadala ya kukataa haya matokeo kama walivyodai watatupa msimamo mzima wa ligi ulivyokuwa...

Watu wengi hawaelewi maana ya mtu anaposema hamtambui raisi maana wengine wanafikiri anakiuka sheria ya treason... Lakini La hasha CHADEMA wamekuwa wastaarabu saana maana maeneo mengine watu walishaanza kutembea barabarani kudai haki tumeona Shinyanga, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kigoma ujiji kusema kwelli CHADEMA wametumia utaratib mzuri sana na kufuta ile dhana ya kuwa wanapenda fujo... Huu ni ustaarabu mwenye akili atafikiri ila aliyenyimwa akaombewe tuu!!!
 
Kwani BWASSA labda nikuulize Baraza la kwanza la kutunga sheria liliundwa mwaka 1926 wakati huo Tanzania haikuwa huru,na hili ndo lilikuwa bunge la wakati huo mchini ya Gavana,Nyerere na wenzake wanne walikuwa miongoni mwa wabunge wa kwanza wa baraza hilo. Je, waliwezaje kukaa kwenye bunge hilo la muingereza japokuwa serikali ya kikoloni walikuwa hawaitaki? Jibu ni moja tu kwamba,walikuwa wanawakilisha wananchi bila kujali nani analiongoza bunge,wangetoka maslahi ya wananchi yasingetetewa, so huwezi sema kuwepo kwao mle ilikuwa na maana wameikubali serikali ya muingereza. The same to CHADEMA kuwepo kwao bungeni hakuna maana wameikubali serikali ya kikwete lazima wawepo mule ili kutetea maslahi ya wananchi dhidi ya tabaka hilo hilo kandamizi linaloshikilia bunge
 

Jamani,

Mnapotoa michango humu, muwe mnaelewa mambo, siyo mnapiga porojo tu! Kuna mtu humu amesema Bunge ni Bunge na Rais ni Rais. Angalieni Katiba ya Jamhuri ya Muungano inavyosema:-

Ibara 62.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge;

Ibara 63. – (1) Rais kama sehemu moja ya Bunge, atatekeleza madaraka aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.[/FONT]


Je, haya Dk. Slaa, ambaye aligombea Urais, hayajui? Je, aliyejipachika Mkuu wa Upinzani katika Bunge, Freeman Mbowe, kwa uroho na uchoyo wa madaraka bila ya kuvishirikisha vyama vingine mashuhuri kama CUF, hayajui haya? Unamkataaje Rais, lakini unakubali kuwa Mbunge? Na hawa ndiyo watu waliotaka waongoze Dola! Wanaapa kwa Katiba ambayo hawaijui? Bora wameshindwa! Tungepta taabu sana nchi hii!
Suala Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya, halihusiki sasa hivi hivi baada ya matokeo! Dk. Slaa na Chadema, walitakiwa wakatae tangu mapema kushiriki uchaguzi kwa kuwa “Tume siyo huru” na “Katiba haifai”. Mnaingia mashindanoni, mnashinda Viti vya Ubunge ili kuogeza ruzuku, mnakubali matokeo na kuapa kuilinda Katiba mkiwa Wabunge (Tume ni ile ile na Katiba ni ile ile); mnashindwa Urais mnasema: “Tume mbovu…Katiba haifai… kura zimechakachuliwa…! Ni sawa na mechi ya mpira, unafungwa mabao, unasema Sheria 17 za FIFA hazifai tena; Refa ametuuma! Tena anayeyasema hayo siyo Kamisaa wa Mchezo bali Kapteni wa Timu iliyoshindwa! Jamani!

Bwassa


Jamani naona haya mambo yananichanganya. Naomba anayeelewa vizuri atoe tafsiri ya hiyo sehemu niliyoweka red. Manake ukisoma kama ilivyo utaona Bunge la Jamhuri ya Muungano limeundwa na vitu 2 ambavyo ni raisi na wabunge.
Manake kama bunge limeundwa na vitu 2 halafu kimoja hukitambui manake hata hilo bunge hulitambui. Labda mniambie bunge limeundwa na kitu kimoja na sio viwili.
 
We Lorah,
Ndiyo hujui chochote, ni mlalamishi tu! Rais ana uwezo wa kulivunja Bunge, kikatiba! Usiseme tu kuwa Bunge linaweza likampigia kura ya kutokuwa na imani na Rais, bali Rais pia anaweza kulivunja Bunge, kwa uwezo aliopewa na Katiba hiyo hiyo waliyoapia kina Mbowe!
Bwassa
 
Jamani naona haya mambo yananichanganya. Naomba anayeelewa vizuri atoe tafsiri ya hiyo sehemu niliyoweka red. Manake ukisoma kama ilivyo utaona Bunge la Jamhuri ya Muungano limeundwa na vitu 2 ambavyo ni raisi na wabunge.
Manake kama bunge limeundwa na vitu 2 halafu kimoja hukitambui manake hata hilo bunge hulitambui. Labda mniambie bunge limeundwa na kitu kimoja na sio viwili.

Bwasa una hasira CUF aka CCM b kutounda upinzani ndo maana unataka utafsiri katiba kulingana na mawazo yako.
Kuna National Asembly ndo ambayo ina wabunge na executive. Ndiyo maana ya hivo vitu vinavokukanganya. Parliament + Executive= National Asembly. Ndio maana ya tafsiri ya hicho kifungu.
Sasa Chadema na wabunge wao wako parliament na rais kamwe is not a member of perliament but a member of national assembly. Tatizo hapa ni uwezo mdogo wa Lugha ya Kiswahili kutafsiri national asembly na perliament kama vitu tofauti. Utaona maneno yanafanana kote ikitumia neno bunge.
CHADEMA kumkataa rais si kwamba wanajichanganya kwamba wanamkataa rais kama rais wakati ndio mkuu wa bunge hivo ni vitu viwili tofauti.
Kwa lugha nyepesi kwa kuwa serikali na bunge ni mihimili inayohusika zaidi kwa huduma za jamii na utendaji zinakuja pamoja katika kitu kinachoitwa National Asembly ili kufanya kazi lakini ni vitu viwli tofauti.
 
With all do respect and my admiration to Dr. Slaa nafikiri hapa kakosea, lakini pia ni uhuru wake wa kikatiba kusema mawazo yake. Hapa naona ni Uselfish zaidi alioutumia, maana sijui what next atafanya au mipango ya CHADEMA baada ya kutomtambua Rais. Kwa kiongozi aliyeweka Kampeni zake kwa kuwatetea Watanzania sijui kwa kutomtambua Raisi atasaidia vipi ktk utetezi. Raisi ni muhimili wa utawala wa Serikali maana ni kama anasema hatatambua kazi yoyote ya serikali, na since hao wabunge wake watalipwa na serikali asiyoitambua watasusia mshiko? Tuache ushabiki na tuchambue hoja ya Sokomoko kwa makini kuwa what next? Na since Number dont lie, am curious kama Slaa ameshataja total number ya kura zake according to calculation zake na kura za Kikwete according to their calculation. Nafikiri sasa angetumia nguvu zaidi na ushawishi wake kuibua mjadala wa kurekebisha tume ya uchaguzi na katiba kwa ajili ya next election, otherwise hizi kelele zake kwangu binafsi naona ni za Kisiasa tuu. Na Mwl Nyerere ambaye Slaa ameshamrejea sana alishasema "IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA'.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hii ni point nzuri tunayojadili mwelewesheni tu sokomoko bila jazba ingawa tumemwelewa katoka wapi la msingi sasa ameelewa. Na kama haelewi ameshasema yeye ana uelewa mdogo inatosha. Ila jibu limeleweka.
 
kwanza kabla ya yote rais wa Tanzania siyo mbunge, kwa kenya sawa, pili ili kuthibitisha hilo rais ataruhusiwa kuingia bungeni pindi tu katiba au mwongozo wa bunge utakapo vunjwa na kuafikiwa na wabunge wote,
hoja yako ya pili ninadhani huelewi vizuri siasa nahujui kuhusu bunge na wabunge, nani anaruhusiwa kuunda kambi ya upinzani, jaribu kwanza kusoma katiba na miongozo yake ndio uwasilishe hoja. wabunge wa chadema hawajachaguliwa na kikwete, wamechaguliwa na wananchi na wapo pale kutetea maslahi ya wananchi,
Tatu nimetambua uwezowako ni mdogo kweli kama ulivyotangulia kusema wewe unadhani siasa ni uadui sisi kama CHADEMA hatuendeshi siasa za uhasama na kusalimiana kwa Dr Slaa na pinda ndo kielelezo tosha kwamba tupo katika kutetea maslahi ya nchi ukijumlisha na pinda kwani naye ni mwananchi.
ANGALIZO:
kama ubongo wako ni wa mgando kimawazo usitumie kuwadanganya hata wale walioelimika, kaa kimya tuachie sisi tunayohitaji mabadiliko na tutayapata yatakusaidia wewe na watoto wako.

Kweli kaka ngau wewe una akili sana;

kumbuka kama umefuatilia siasa physically sio za kwenye keyboard, kuna sehemu watu wamakufa, ofisi za ccm kuchomwa moto, nyumba za wanachama kuchomwa moto n.k, wounds that have been caused by recently election in some areas you can heal!

kwa layman wa kawaida kabisa, kama mimi ukiacha wewe mwenzetu mwenye akili ni ngumu sana ku-comprehend the reality. nashangaa hata muansiha maada alijishusha ili ngau usitumie maneno yale yale, lakinikama ilivyozoeleka umepokea defensive hili swala

Rais aliteua jina la PM, Tundu Lissu ndiyo aliyeenda kuhesabu kura, na same president hatambuliwi, kukataa matokeo ni kesi kubwa na I am telling you, wananchi wengi wangekuwa nyuma ya chadem kuipa support for any move, kama hauamini nenda segerea, uone mahanha asivyokuwa kwenye amani!!

Huu ukondoo ,ndio unaosababisha watu wasipige kura next elections! tusijione tumefika na hawa wabunge, wananchi hawa hawa huwa wanabadilika msisahau hili na issue ya RUZUKU inazumngumzwa sana, kuwa jamaa wamepata walichokuwa wanataka na wale walioumia na kubaki na makovu yatabaki hivyo hivyo huku nguvu yao ikiwa imepotea bire, mwaka 2015 mtamtaka tena huyu mtu awapigi ekura! my foot!

Guys hii issue ni serious kuliko mnavyodhani, the very applausible move ya kusema hawatambuai matokeo was excellent and supportive, lakini kinachoendela baada ya hapo ni confusion, watu wakiuliza wanaambiwa una uelwa mdogo! yuko wapi Rais Mteule Slaa?

hivi siasa za amani zikoje, wakisema wanasusia bunge ngau kutikisa kiberiti sio faraja tosha kwa walioumia? ili hali wakitengeneza na kufanya cheap and sel-explanatory campaigns za mwaka 2015, turnout ya watu itakuwa kubwa wakiamini na KUJISEMA LETS SEE THIS TIME AGAIN!!! lakini hali ya sasa ina warudisha nyuma wengi na they will evenetually forget Chadema soon!

This is forum, hakuna sifa wala kujuana humu, hizi defensive and 'shatap' comments hazitusaidii kwenye ukombozi, it hurts us, really!, usije shangaa mwaka 2015 cahdema inapata wabunge 4?? in poltics is possible, just do what voters need!
 
Naomba nikusahihishe Sokomoko,tofautisha kati ya kuwakilisha na kuwasilisha. Unamuwakilisha nani? I think the correct word is "NAWASILISHA"
 
Back
Top Bottom