Baada ya kuimaliza NCCR, Marando sasa aanza na CHADEMA

TandaleOne alichosema Marando ni kweli tupu hasa ukizingatia zile meseji zilizokuwa zinatumwa mwaka jana wakati wa uchaguzi za uchochezi juu ya Dr Slaa! meseji zilikuwa zinaonekana zinatumwa toka Malasia, baada ya malalamiko mengi sana na baada ya mamlaka ya mawasiliano kufuatilia waligundua kuwa zile meseji zilikuwa zintumwa toka hapa hapa nchini na kuna watu walienda mbali na kuja na ushahidi kuwa zilikuwa zikitumwa kutoka karibu na jengo moja liko pale karibu na hotel iliyokuwa sheraton zamani, na kama vile mgongano inasemekana pia ndani ya jengi hilo hilo kuwakuwa na ofisi zisizo rasmi zilizokuwa zikiratibu kampeni za JK zikiongozwa na mtoto wake aliyesomea mambo ya IT kule nchini India akishirikiana na rafiki zake! so kama lile liliwezekana hili linashindikana vipi?
 
JUMAMOSI iliyopita, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando alinukuliwa akiwatetea wabunge wa chama hicho John Mnyika na Tundu Lissu, kwa kusema hawakutishia kumuua Mbunge wa Iramba Magharibi mkoani Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba.

Marando ambaye pia ni wakili wa kujitegemea na afisa wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa (NSS), alisema siyo kweli kwamba wabunge hao walimtumia Nchemba meseji zenye ujumbe wa mauaji dhidi yake, vinginevyo aache kukifuatafuata chama chao katika harakati zake za kutaka kutawala mwaka 2015.

Alisema badala yake, meseji hizo zimetumwa kwa mbunge huyo na mtoto wa kigogo wa CCM anayemiliki mtambo wa kuingilia mawasiliano ya watu kwa mbinu za kijasusi, lakini akashindwa kumtaja jina wala kuzungumza chochote juu yake.

Huku akijitambulisha kuwa ni Kiongozi wa Idara ya Usalama na Upelelezi ya Chadema, alisema mtambo huo umenunuliwa nchini Israel, na kwamba umetumika kuandaa maneno na kuingilia mawasiliano ya simu za wabunge hao.

"Nchini Israel kuna kampuni mbili; Verinty na Nice Systems, hizi zimegundua mtambo wenye uwezo wa kuingilia mawasiliano ya watu kwenye mitandao yao iwe intaneti au simu", alisema.

Nilibahatika kumfahamu vizuri Marando alipokuwa Katibu Mkuu wa chama cha NCCR – Mageuzi kati ya mwaka 1995 – 1999, wakati huo nikiwa mwandishi wa habari wa magazeti kadhaa nchini, hivyo nina mengi ninayoweza kuyaainisha juu yake ingawa sitaki kufanya hivyo katika makala hii kwa sababu siyo mahali pake.

Ninachotaka kusema ni kwamba kama ni taaluma ya ushushushu aliyonayo basi amehitimu kwa mafanikio sana. Ana uwezo wa kumwibulia tuhuma mtu yeyote na kuziweka wazi hata mbele ya halaiki, akazungumza kwa makini na uhakika mdomoni mwake, lakini ukifuatilia baadaye unagundua bila mashaka yoyote kuwa ni uzushi.

Ujuzi wake huo niliweza kuujua vizuri kati ya mwaka 1997 – 1999 alipokuwa akigombana kwa nguvu kubwa na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR – Mageuzi, wakati huo, yule ambaye hivi sasa ni Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema.

Lakini kwa vile naye ni shushushu na amewahi kuwa mpaka Afisa Usalama wa Taifa wa Wilaya (DSO) kule Kahama mkoani Shinyanga, fitina za Marando kisiasa kwa Mrema ziligonga mwamba hadi akakimbia yeye mwenyewe kutoka Makao Makuu ya NCCR – Mageuzi, Manzese Argentina jijini Dar es Salaam.

Ukimwacha Mrema, viongozi wengine waliowahi kupandikiziwa chuki katika chama hicho na Ofisi ya Katibu Mkuu chini ya Marando ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Kitengo cha Vijana, Msafiri Metemelwa ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Taifa wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Prince Bagenda.

Wakati ambapo Mtemelwa alizushiwa kwamba anaongoza kikundi cha kigaidi cha Black Mamba ili kuwadhuru viongozi wanaompinga Mrema katika upande wa kwanza, Bagenda katika upande wa pili aling'olewa kutoka Kamati Kuu ya Chama, lengo likiwa ni kupunguza nguvu za mbunge huyo wa sasa wa Vunjo katika chombo hicho cha uongozi wa kisiasa.

Inawezekana Mtemelwa na Marando katika kipindi hiki hawavutani wala kugombania tena jambo lolote la kisiasa na uongozi wakiwa wote Chadema, lakini mwanasiasa huyo kamwe hawezi kusahau yaliyomkuta ikiwemo kufukuzwa kwenye vikao muhimu vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya NCCR – Mageuzi, vyote vikifanyika kwa vurugu za kijinga kwenye Ukumbi wa Raskazone Hotel mjini Tanga kuanzia Mei 21, 1997.

Mwingine ambaye hawezi kusahau vurugu za Marando za kisiasa ukiwemo uzushi, uongo na fitina kwa wapinzani wake ni pamoja na Harold Jaffu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya NCCR – Mageuzi aliyekuja kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho na hatimaye TLP chini ya Mrema baada ya Bagenda kuachia nafasi hiyo.

Wengine ni pamoja na Thomas Ngawaiya aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa Taifa wa NCCR – Mageuzi na TLP, Hamduni Marcel aliyekuwa Mkurugenzi wa Taifa wa Kampeni na Uchaguzi wa NCCR – Mageuzi iliyokimbiwa na kina Marando na Cosmas Chenyenge, yule ambaye naye alikuwa Mwenyekiti wa vyama hivyo kwa nyakati tofauti wa Mkoa wa Mwanza.

Hao wote na wengineo wanamjua vizuri Marando kuwa kwenye siasa ni mzushi kiasi gani, mfitini wa daraja gani na rafiki namna gani, yule ambaye ana sura na rangi tofauti na yupo radhi na tayari wakati wowote na mahali popote kusema vyovyote, kuanzisha chochote na kung'ang'ania jambo lolote ili mradi tu anakidhi matakwa yake ya muda huo bila kujali kutatokea nini baadaye.

Kama ni kazi ya kutengeneza maneno mezani, kuyamwaga hadharani na kufanana na ukweli basi Marando amefuzu. Aliweza kumfitini Mrema na kila kiongozi aliyekuwa akimuunga mkono walipokuwa wote NCCR – Mageuzi, lakini dhambi hiyo ilikwenda naye sambamba hadi chama hicho kikasambaratika kama kishada kilichokwenda harijojo!

Kilikufa kama kibudu hadi mwenyewe akapoteza mvuto hata kwa wanachama, marafiki na viongozi aliokimbia nao kutoka Manzese Argentina, wakahamia Kisutu ambako walifungua ofisi mpya ya Makao Makuu ya NCCR – Mageuzi huku wakikomba ruzuku yote ya chama.

Ushahidi wa suala hili ni pale alipotaka kurudi tena kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR – Mageuzi kupitia uchaguzi mkuu wa chama hicho wa mwaka 1999. Katika zoezi hilo ambalo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam, Marando na aliyekuwa rafiki yake wa karibu, Dk. Masumbuko Lamwai walitupiliwa mbali na nafasi hiyo ikachukuliwa na James Mbatia ambaye bado anaendelea nayo hadi sasa.

Katika kutaka kwake kuwatetea Mnyika na Lissu kwamba hawahusiki na vitisho vya mauaji dhidi ya Nchemba, hakika shushushu huyo wa zamani wa serikali anajaribu kutwanga maji kwenye kinu, kazi ambayo kwa vyovyote siku ya mwisho itakuja iwe tasa.

Anajaribu kuogelea kwenye bahari yenye kina kirefu cha maji huku mawimbi makali na tena usiku wa manane yakimpiga usoni. Anataka kuwaokoa kutoka kwenye korongo lenye giza nene, lile ambalo bila kutumia umeme hata akikesha anamulika kwa tochi ya betri 10 hawezi kuona mlango wa kuweza kuwatolea.

Kama alivyoshindwa kumng'oa Mrema kutoka katika uongozi wa juu wa NCCR – Mageuzi, akajaribu kumvuruga mpaka kisaikolojia wakiwa kwenye kikao cha NEC kule Tanga, lakini akakimbia yeye mwenyewe usiku wa manane, akahamishia ofisi uchochoroni kutoka Makao Makuu yaliyoandikishwa kisheria; hakika hata juhudi hizi za kutaka kuwaokoa kina Mnyika na Tundu Lissu nazo zitakwama.

Anataka kuitumia nafasi hiyo kusaka umaarufu kwa kudai kuwa ametumia ushushushu wake akiwa ni Kiongozi wa Idara ya Intelijensia ya Chadema, akazichunguza tuhuma hizo kwa siku tatu tu na kugundua kwamba kuna mtoto wa kigogo wa CCM anayemiliki mtambo wa kufanyia ujasusi dhidi ya watu wengine.

Sitaki kuaminishwa uongo na kielelezo siyo kutaja majina ya makampuni yanayotengeneza mitambo hiyo kwa sababu hata kompyuta inafahamika wapi zinatengenezwa duniani, halafu hata Marando mwenyewe anazijua ni kampuni gani zinatengeneza na kuuza ndege za aina zote za Gulf Stream, Air Bus, Boeing, Fokker Friendship, Twin Otter na kadhalika, hivyo anaweza pia kusema chochote akitaka kuibua uzushi wowote kwa kutumia makapmuni hayo kama kigezo cha kuhalalishia uongo wake.

Kama hawadanganyi Watanzania basi atutajie majina kamili ya mtoto huyo wa kigogo wa CCM aliyenunua mtambo huo, aseme ilikuwa lini kwa maana ya tarehe, mwezi na mwaka gani, saa ngapi na atuonyeshe pia risiti ya mauzo hayo na ikiwezekana atuambie hata jina la afisa aliyehusika katika kuuza mtambo huo kule Israel.

Ataje mtoto huyo wa kigogo wa CCM aliondoka Tanzania tarehe ngapi, mwezi gani, mwaka gani na alitumia usafiri gani kama ni wa anga au meli na shirika lake, linamilikiwa na nani na kutoka nchi gani, alianzia wapi safari yake, saa ngapi, alipitia wapi na Israel alifika muda gani.

Aseme alifikia uwanja upi wa ndege au bandari gani nchini humo, akaishi huko kwa muda gani akiwa hoteli gani kabla ya kurudi Tanzania. Ataje pia usafiri aliotumia kwa safari hiyo na takwimu nyingine zote kwa wasafiri wa kigeni wanaokwenda na kutoka nchi nyingine.

Bila kufanya hivyo atakuwa anajaribu tena kurudia kazi iliyomshinda kwa Mrema, halafu akashindwa pia kurejea madarakani kama Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR – Mageuzi kwa awamu ya pili. Akagaragazwa vibaya na Mbatia hadi akatimka kutoka chama hicho na kujisalimisha mwenyewe Chadema.

Endapo amebobea katika uzushi wa kisiasa, majungu na fitina zake sasa namuomba asidhani Watanzania wote ni zezeta wa kufikiri au kutafakari vichwani mwao. Inabidi atafute namna mpya inayoweza kuwaokoa Mnyika na Tundu Lissu kama anataka aendelee kuaminiwa kuwa Kiongozi wa Idara ya Intelijensia ya Chadema.

Kubaki ameng'ang'ania uongo huo hatimaye ataaibika na kama alivyosema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye, shushushu huyo ni mzushi aliyewahi kumsingizia hata yeye, lakini alipombana akaomba radhi kwa maandishi kuwa alishinikizwa kufanya hivyo…"Hata haijapita angalau miezi mitano tu hivi anatoa uzushi mwingine", anasema.

Huyo ndiye Mabere Marando, Katibu Mkuu wa zamani wa NCCR – Mageuzi aliyeongoza harakati za kukimaliza kisiasa chama hicho kuanzia mwaka 1997 – 1999, yule ambaye sasa anatetea uozo utakaoisambaratisha Chadema kwa kutumia uzushi mwingine!

One mistake does not define who you are, but don't repeat and let the past mistakes to define who you are!!!

Jamani, baada ya hayo yote alikuwa kimya kwenye siasa inaonyesha kama yeye ni Msomi alijiangalia, akaona Makosa

Yake akaona ni bora kujirekebisha sidhani CHADEMA walimpokea bila kumgusia story zake za zamani; sio vizuri

kumbagua mtu kwa story za zamani kama hajaua hiyo ndio historia yetu ya uchanga wetu wa vyama vingi vya

kisiasa - democracy in it's youngest stage; Angalia Kenya wanavyokanyagana lakini kesho Wanaungana...
 
pamoja na kwamba sikubaliani nacdm kumpa marando ujumbe wa kamati kuu kutokana na yeye kuwatetea baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi hoja zako bado ni dhaifu kwani huyo Mrema unayemsifia naye alikuwa usalama wa taifa na hata alipoamia TLP wote pamoja na Thomas Ngawaiya waliishia kugombana siku nyingine unapoleta mada inabidi ujipange vizuri
 
aliyekutuma mkae naye kisha mje kivingine hii single haijatuzibua masikio
 
:A S 465:alichoongea marando ni UKWELI mtupu, mtambo huo unamilikiwa na Mdogo wa rizmoko aliesoma India...ndio waliutumia wakati wa uchaguz wa uraisi uliopita kuwachafua upinzani wakishirikiana na kigogo mmoja wa vodacom ambae alikua ndo head wa IT pale voda kabla ya kuhamia NBC pia alikuwepo jamaa mmoja anaemiliki hizi kampuni za kubroadcast msg via shortcodes. :A S 465:
 
unazungumza katika lugha usiyoifahamu...!
I doubt very much your ability to comprehend complex issues hence hujui unaloandika! Ingekuwa vyema ukaandika analysis yako ukaeleweka kuliko kukurupupa kana kwamba umetumwa kuandika chochote km afisa uhusiano.
 
uzi huu hauko focused kabisa
eti labda utufafanulie nini dhumuni lako mkuu kuanzisha hii thread?
 
Acha chuki binafsi
Cha muhimu ulitakiwa kujadili hoja, kama wewe si mtumwa wa ccm.
Hoja ni kwamba ujumbe umetungwa na hao hao wanaodai wametumiwa, ili kuwachafua wabunge wa cdm.
Swala kwamba Marando kasema uongo yatajulikana mahakamani.
Mambo ya NCCR-Mageuzi yameingiaje hapa?
 
Unataka tuamini unavyoamini weye kuwa nchemba kweli katishiwa? Ulishazisikia fake sms?
 
hoja si aliondoka lini,kwa usafri gan na alilala wap kwan kununua kifaa huwezi kuagza ata ukiwa chumbani kikaja?mwiba inaonekana ww na kundi lako hamjui kazi za DHL na WESTERN UNION
 
jumamosi iliyopita, mjumbe wa kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), mabere marando alinukuliwa akiwatetea wabunge wa chama hicho john mnyika na tundu lissu, kwa kusema hawakutishia kumuua mbunge wa iramba magharibi mkoani singida kupitia chama cha mapinduzi (ccm), mwigulu nchemba.

Marando ambaye pia ni wakili wa kujitegemea na afisa wa zamani wa idara ya usalama wa taifa (nss), alisema siyo kweli kwamba wabunge hao walimtumia nchemba meseji zenye ujumbe wa mauaji dhidi yake, vinginevyo aache kukifuatafuata chama chao katika harakati zake za kutaka kutawala mwaka 2015.

Alisema badala yake, meseji hizo zimetumwa kwa mbunge huyo na mtoto wa kigogo wa ccm anayemiliki mtambo wa kuingilia mawasiliano ya watu kwa mbinu za kijasusi, lakini akashindwa kumtaja jina wala kuzungumza chochote juu yake.

Huku akijitambulisha kuwa ni kiongozi wa idara ya usalama na upelelezi ya chadema, alisema mtambo huo umenunuliwa nchini israel, na kwamba umetumika kuandaa maneno na kuingilia mawasiliano ya simu za wabunge hao.

“nchini israel kuna kampuni mbili; verinty na nice systems, hizi zimegundua mtambo wenye uwezo wa kuingilia mawasiliano ya watu kwenye mitandao yao iwe intaneti au simu”, alisema.

Nilibahatika kumfahamu vizuri marando alipokuwa katibu mkuu wa chama cha nccr – mageuzi kati ya mwaka 1995 – 1999, wakati huo nikiwa mwandishi wa habari wa magazeti kadhaa nchini, hivyo nina mengi ninayoweza kuyaainisha juu yake ingawa sitaki kufanya hivyo katika makala hii kwa sababu siyo mahali pake.

Ninachotaka kusema ni kwamba kama ni taaluma ya ushushushu aliyonayo basi amehitimu kwa mafanikio sana. Ana uwezo wa kumwibulia tuhuma mtu yeyote na kuziweka wazi hata mbele ya halaiki, akazungumza kwa makini na uhakika mdomoni mwake, lakini ukifuatilia baadaye unagundua bila mashaka yoyote kuwa ni uzushi.

Ujuzi wake huo niliweza kuujua vizuri kati ya mwaka 1997 – 1999 alipokuwa akigombana kwa nguvu kubwa na mwenyekiti wa taifa wa nccr – mageuzi, wakati huo, yule ambaye hivi sasa ni mwenyekiti wa taifa wa tanzania labour party (tlp), augustine mrema.

Lakini kwa vile naye ni shushushu na amewahi kuwa mpaka afisa usalama wa taifa wa wilaya (dso) kule kahama mkoani shinyanga, fitina za marando kisiasa kwa mrema ziligonga mwamba hadi akakimbia yeye mwenyewe kutoka makao makuu ya nccr – mageuzi, manzese argentina jijini dar es salaam.

Ukimwacha mrema, viongozi wengine waliowahi kupandikiziwa chuki katika chama hicho na ofisi ya katibu mkuu chini ya marando ni aliyekuwa mwenyekiti wa taifa wa kitengo cha vijana, msafiri metemelwa ambaye hivi sasa ni mkurugenzi wa taifa wa kampeni na uchaguzi wa chadema na aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu, prince bagenda.

Wakati ambapo mtemelwa alizushiwa kwamba anaongoza kikundi cha kigaidi cha black mamba ili kuwadhuru viongozi wanaompinga mrema katika upande wa kwanza, bagenda katika upande wa pili aling’olewa kutoka kamati kuu ya chama, lengo likiwa ni kupunguza nguvu za mbunge huyo wa sasa wa vunjo katika chombo hicho cha uongozi wa kisiasa.

Inawezekana mtemelwa na marando katika kipindi hiki hawavutani wala kugombania tena jambo lolote la kisiasa na uongozi wakiwa wote chadema, lakini mwanasiasa huyo kamwe hawezi kusahau yaliyomkuta ikiwemo kufukuzwa kwenye vikao muhimu vya kamati kuu na halmashauri kuu ya taifa (nec) ya nccr – mageuzi, vyote vikifanyika kwa vurugu za kijinga kwenye ukumbi wa raskazone hotel mjini tanga kuanzia mei 21, 1997.

Mwingine ambaye hawezi kusahau vurugu za marando za kisiasa ukiwemo uzushi, uongo na fitina kwa wapinzani wake ni pamoja na harold jaffu, mjumbe wa kamati kuu ya nccr – mageuzi aliyekuja kuwa katibu mkuu wa chama hicho na hatimaye tlp chini ya mrema baada ya bagenda kuachia nafasi hiyo.

Wengine ni pamoja na thomas ngawaiya aliyewahi kuwa katibu mwenezi wa taifa wa nccr – mageuzi na tlp, hamduni marcel aliyekuwa mkurugenzi wa taifa wa kampeni na uchaguzi wa nccr – mageuzi iliyokimbiwa na kina marando na cosmas chenyenge, yule ambaye naye alikuwa mwenyekiti wa vyama hivyo kwa nyakati tofauti wa mkoa wa mwanza.

Hao wote na wengineo wanamjua vizuri marando kuwa kwenye siasa ni mzushi kiasi gani, mfitini wa daraja gani na rafiki namna gani, yule ambaye ana sura na rangi tofauti na yupo radhi na tayari wakati wowote na mahali popote kusema vyovyote, kuanzisha chochote na kung’ang’ania jambo lolote ili mradi tu anakidhi matakwa yake ya muda huo bila kujali kutatokea nini baadaye.

Kama ni kazi ya kutengeneza maneno mezani, kuyamwaga hadharani na kufanana na ukweli basi marando amefuzu. Aliweza kumfitini mrema na kila kiongozi aliyekuwa akimuunga mkono walipokuwa wote nccr – mageuzi, lakini dhambi hiyo ilikwenda naye sambamba hadi chama hicho kikasambaratika kama kishada kilichokwenda harijojo!

Kilikufa kama kibudu hadi mwenyewe akapoteza mvuto hata kwa wanachama, marafiki na viongozi aliokimbia nao kutoka manzese argentina, wakahamia kisutu ambako walifungua ofisi mpya ya makao makuu ya nccr – mageuzi huku wakikomba ruzuku yote ya chama.

Ushahidi wa suala hili ni pale alipotaka kurudi tena kuwa mwenyekiti wa taifa wa nccr – mageuzi kupitia uchaguzi mkuu wa chama hicho wa mwaka 1999. Katika zoezi hilo ambalo lilifanyika kwenye ukumbi wa chuo cha bandari, tandika jijini dar es salaam, marando na aliyekuwa rafiki yake wa karibu, dk. Masumbuko lamwai walitupiliwa mbali na nafasi hiyo ikachukuliwa na james mbatia ambaye bado anaendelea nayo hadi sasa.

Katika kutaka kwake kuwatetea mnyika na lissu kwamba hawahusiki na vitisho vya mauaji dhidi ya nchemba, hakika shushushu huyo wa zamani wa serikali anajaribu kutwanga maji kwenye kinu, kazi ambayo kwa vyovyote siku ya mwisho itakuja iwe tasa.

Anajaribu kuogelea kwenye bahari yenye kina kirefu cha maji huku mawimbi makali na tena usiku wa manane yakimpiga usoni. Anataka kuwaokoa kutoka kwenye korongo lenye giza nene, lile ambalo bila kutumia umeme hata akikesha anamulika kwa tochi ya betri 10 hawezi kuona mlango wa kuweza kuwatolea.

Kama alivyoshindwa kumng’oa mrema kutoka katika uongozi wa juu wa nccr – mageuzi, akajaribu kumvuruga mpaka kisaikolojia wakiwa kwenye kikao cha nec kule tanga, lakini akakimbia yeye mwenyewe usiku wa manane, akahamishia ofisi uchochoroni kutoka makao makuu yaliyoandikishwa kisheria; hakika hata juhudi hizi za kutaka kuwaokoa kina mnyika na tundu lissu nazo zitakwama.

Anataka kuitumia nafasi hiyo kusaka umaarufu kwa kudai kuwa ametumia ushushushu wake akiwa ni kiongozi wa idara ya intelijensia ya chadema, akazichunguza tuhuma hizo kwa siku tatu tu na kugundua kwamba kuna mtoto wa kigogo wa ccm anayemiliki mtambo wa kufanyia ujasusi dhidi ya watu wengine.

Sitaki kuaminishwa uongo na kielelezo siyo kutaja majina ya makampuni yanayotengeneza mitambo hiyo kwa sababu hata kompyuta inafahamika wapi zinatengenezwa duniani, halafu hata marando mwenyewe anazijua ni kampuni gani zinatengeneza na kuuza ndege za aina zote za gulf stream, air bus, boeing, fokker friendship, twin otter na kadhalika, hivyo anaweza pia kusema chochote akitaka kuibua uzushi wowote kwa kutumia makapmuni hayo kama kigezo cha kuhalalishia uongo wake.

kama hawadanganyi watanzania basi atutajie majina kamili ya mtoto huyo wa kigogo wa ccm aliyenunua mtambo huo, aseme ilikuwa lini kwa maana ya tarehe, mwezi na mwaka gani, saa ngapi na atuonyeshe pia risiti ya mauzo hayo na ikiwezekana atuambie hata jina la afisa aliyehusika katika kuuza mtambo huo kule israel.

Ataje mtoto huyo wa kigogo wa ccm aliondoka tanzania tarehe ngapi, mwezi gani, mwaka gani na alitumia usafiri gani kama ni wa anga au meli na shirika lake, linamilikiwa na nani na kutoka nchi gani, alianzia wapi safari yake, saa ngapi, alipitia wapi na israel alifika muda gani.

Aseme alifikia uwanja upi wa ndege au bandari gani nchini humo, akaishi huko kwa muda gani akiwa hoteli gani kabla ya kurudi tanzania. Ataje pia usafiri aliotumia kwa safari hiyo na takwimu nyingine zote kwa wasafiri wa kigeni wanaokwenda na kutoka nchi nyingine.

Bila kufanya hivyo atakuwa anajaribu tena kurudia kazi iliyomshinda kwa mrema, halafu akashindwa pia kurejea madarakani kama mwenyekiti wa taifa wa nccr – mageuzi kwa awamu ya pili. Akagaragazwa vibaya na mbatia hadi akatimka kutoka chama hicho na kujisalimisha mwenyewe chadema.

Endapo amebobea katika uzushi wa kisiasa, majungu na fitina zake sasa namuomba asidhani watanzania wote ni zezeta wa kufikiri au kutafakari vichwani mwao. Inabidi atafute namna mpya inayoweza kuwaokoa mnyika na tundu lissu kama anataka aendelee kuaminiwa kuwa kiongozi wa idara ya intelijensia ya chadema.

Kubaki ameng’ang’ania uongo huo hatimaye ataaibika na kama alivyosema katibu wa halmashauri kuu ya taifa (nec) ya ccm, nape nnauye, shushushu huyo ni mzushi aliyewahi kumsingizia hata yeye, lakini alipombana akaomba radhi kwa maandishi kuwa alishinikizwa kufanya hivyo…“hata haijapita angalau miezi mitano tu hivi anatoa uzushi mwingine”, anasema.

Huyo ndiye mabere marando, katibu mkuu wa zamani wa nccr – mageuzi aliyeongoza harakati za kukimaliza kisiasa chama hicho kuanzia mwaka 1997 – 1999, yule ambaye sasa anatetea uozo utakaoisambaratisha chadema kwa kutumia uzushi mwingine!
nahitaji kujua umri wako kama una miaka zaidi 67 basi unabembeleza pension upewe na ccm ,watz tumekustukia huwezi kututeka kashauriane na bi nyau pamoja na bonge bila kumsahau popo bawa jinsi ya kuinusuru cc magamba ife kifo kizuri
 
PAMBAFU; Maelezo pumba jamaa inaonekana kwa umri umekuwa kidogo lakini sijui ulisoma wapi mahala wanapofundisha kusoma na kuandika bila kukupa maarifa ya kufikiri
 
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa Mnyika na Lissu wamehusika katika sakata hilo? Magamba utawajua tu! Unatetea ushuzi?? Wabongo bwana noma; nimesomaaaaa....kumbe yooote ni fitna, majungu na umbea tu! Hakuna kitu hapa. Wewe kama una bifu na Marando um face sio unaleta umbea wa kiswahili hapa!!!!
 
Back
Top Bottom