Baada ya kuimaliza NCCR, Marando sasa aanza na CHADEMA

aibu juu ya aibu...ameshasema ushahidi anao na sote tunajua ushahidi unatolewa wapi sasa wewe na Nape mnashangaza mnapotaka atoe ushahiidi JF au Habari-Maelezo. Kama hamna guts za kumpeleka mahakamani, nawasihi mnyamaze. Unless anashindwa kutoa ushahidi unaokidhi kisheria otherwise Marando yuko sahihi. Jambo dogo mnatumia nguvu nyingiiiii kukanusha.
 
Kumbe mtu akisema anachokijua juu ya watu wa upande fulani inakuwa ni uzushi, utandale, kwa bibi nyau, kwa tumbo kwenye harufu mbaya n.k.
Wanajf ukweli utabaki palepale tu kwamba marando alikuwa katika vyama karibu vyote vya upinzani na kafanikiwa kwa kiasi fulani, kama sikosei alikuwepo pia cuf wakati ule kipo ngangari, sasa cuf sio tena ngangari bali ni chenye mlengo wa wastani sio mbaya kwani lengo ni kujenga nchi.
Aaaaaaaaaaaaaaah!!!!! Marando hongera sana umekuwa mzalendo wa ukweli kwa nchi yako kwani ukiona mabaya huachi kuyaweka hadharani na kuwataja wahusika.
Je, ukanda na ukabila nao mkuu haujauona? Ni mzuri kwa umoja na mshikamano wa taifa? Je katiba yenu inasemaje juu ya hilo?
Fanya kazi kwa maslahi ya taifa letu.
Mungu ibariki tanzania.
 
Swali rahisi hivi wewe leo ukapoteza sim card yako ukanunua simu card nyingine inakuaje unapotakuaje unapotake kuiendeleza namba yako ya simu ya zamani? kama wanaweza ku-swap namba ni nini kinashindikana ku-swap namba ya mtu mwingine kwa muda ikatumiwa kwa uhalifu na kisha kurudishwa tena hiyo namba? Tuaje ushabiki badala ya kuliangalia swala kitaalam.
unazungumza katika lugha usiyoifahamu...!
 
tandale One maelezo marefu lakini ulichokua unataka kumjua mtoto wa kigogo aliyetuhumiwa na Mabere Malando na umeandika habari kwa kumshambulia mtu bila hoja za msingi jipange na pole sana kwa kutumia muda mrefu kuandika hii news
yawezekana kuwa umesoma habari hii, lakini kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
Controversially, some of the info above connects/points to the man.

Of coz he's known to be what he is, and you should never trust him more than 12%. In politics, generally trust nobody more than 12%. You may ask why 12%, it's bcoz the % are dereived from some ambigious formulas.
lugha uliyoitumia ni lugha sahihi lakini itakuwa ni ngumu kueleweka kwa hawa "jamaa zangu wa CDM"
 
Uwanja wa fisi vp, bado libeneke linaendeleaga kama zamani zile nyama za kidizain niajeniaje zipo bado? Mkesha nini vp upo
Pumba na siasa za kijinga. Mtoa mada anatumia kichwa kubebea nywele na siyo kufikiri!!
 
TandaleOne Pole sana but my advise is this nenda nawe maelezo au itisha tv na magazeti kwa uwazi mjibu Marando kwa ushahidi
watu wanajibiwa kulingana na mashiko wa kile walichokiandika, ni upotevu wa muda, nguvu na rasilimali fedha kujibu hili katika mlolongo ulioutaja.
 
tukisema amemchafua 2 Marando tutakuwa wavivu wa kufikiri, Marando anatakiwa aangaliwe kwa jicho la tatu, mambo aliyoyafanya NCCR kamwe mpenda Demokrasia ya kweli hawezi kumsamehe wala kusahau, ccm walimpa mpaka ubunge wa EA, Binafsi si mwamini marando, kimuundo hata kesi zingine anazozisimamia zinapingana na muonekano wa wana CDM. Mi nadhani ametukumbusha tuwe makini nae
Ni bahati mbaya kwako, lakini ni bahati mbaya zaidi kwa wanachadema wote kuwa wakiaminishwa katika jambo hawana tena nidhamu ya kulitafakari.,hii ni bahati mbaya, ni bahati mbaya kwako kuwa unatamani wengine wangeliwaza kama wewe ili kufika mbali na kuyafikia mafanikio ya kisiasa ambayo kama chama mnayaota siku zote.
 
Maneno mengi lakini huna hoja za msingi. Yeye ameanza kuibua nawe fanya uchunguzo wako na kukanusha juu ya hoja za marando, sio kutulaghai na uCCM wako ukifikiri unaweza kubadili ukweli.
Bado watu wanayo safari ndefu sana katika kufikia ukombozi wa kweli, ambao huwa unaanza na ukombozi binafsi unaojengwa katika msingi wa ukombozi wa fikra. Kwa maana siku ukianza kuwaza kama wewe na si kuwaza kama wanavyotaka wao uwaze unaweza ukawa umepiga hatua moja katika safari ndefu uliyonayo ya kujikomboa.
 
Nilijua tu Marando alikuwa anazusha ,katika ile meza ukimuangalia Dr.Slaa alikuwa ana wasiwasi sana na yale aliokuwa akizungumzia Marando.
Mwandishi amewaonya CDM wawe waangalifu na huyo jamaa la sivyo anaweza akawazamisha na kuwaacha kwenye mataa baada ya kumaliza kazi iliyomleta hapo.

Ushauri mwingine ni kama Nguvu za giza!
 
JUMAMOSI iliyopita, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando alinukuliwa akiwatetea wabunge wa chama hicho John Mnyika na Tundu Lissu, kwa kusema hawakutishia kumuua Mbunge wa Iramba Magharibi mkoani Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba.

Marando ambaye pia ni wakili wa kujitegemea na afisa wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa (NSS), alisema siyo kweli kwamba wabunge hao walimtumia Nchemba meseji zenye ujumbe wa mauaji dhidi yake, vinginevyo aache kukifuatafuata chama chao katika harakati zake za kutaka kutawala mwaka 2015.

Alisema badala yake, meseji hizo zimetumwa kwa mbunge huyo na mtoto wa kigogo wa CCM anayemiliki mtambo wa kuingilia mawasiliano ya watu kwa mbinu za kijasusi, lakini akashindwa kumtaja jina wala kuzungumza chochote juu yake.

Huku akijitambulisha kuwa ni Kiongozi wa Idara ya Usalama na Upelelezi ya Chadema, alisema mtambo huo umenunuliwa nchini Israel, na kwamba umetumika kuandaa maneno na kuingilia mawasiliano ya simu za wabunge hao.

“Nchini Israel kuna kampuni mbili; Verinty na Nice Systems, hizi zimegundua mtambo wenye uwezo wa kuingilia mawasiliano ya watu kwenye mitandao yao iwe intaneti au simu”, alisema.

Nilibahatika kumfahamu vizuri Marando alipokuwa Katibu Mkuu wa chama cha NCCR – Mageuzi kati ya mwaka 1995 – 1999, wakati huo nikiwa mwandishi wa habari wa magazeti kadhaa nchini, hivyo nina mengi ninayoweza kuyaainisha juu yake ingawa sitaki kufanya hivyo katika makala hii kwa sababu siyo mahali pake.

Ninachotaka kusema ni kwamba kama ni taaluma ya ushushushu aliyonayo basi amehitimu kwa mafanikio sana. Ana uwezo wa kumwibulia tuhuma mtu yeyote na kuziweka wazi hata mbele ya halaiki, akazungumza kwa makini na uhakika mdomoni mwake, lakini ukifuatilia baadaye unagundua bila mashaka yoyote kuwa ni uzushi.

Ujuzi wake huo niliweza kuujua vizuri kati ya mwaka 1997 – 1999 alipokuwa akigombana kwa nguvu kubwa na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR – Mageuzi, wakati huo, yule ambaye hivi sasa ni Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema.

Lakini kwa vile naye ni shushushu na amewahi kuwa mpaka Afisa Usalama wa Taifa wa Wilaya (DSO) kule Kahama mkoani Shinyanga, fitina za Marando kisiasa kwa Mrema ziligonga mwamba hadi akakimbia yeye mwenyewe kutoka Makao Makuu ya NCCR – Mageuzi, Manzese Argentina jijini Dar es Salaam.

Ukimwacha Mrema, viongozi wengine waliowahi kupandikiziwa chuki katika chama hicho na Ofisi ya Katibu Mkuu chini ya Marando ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Kitengo cha Vijana, Msafiri Metemelwa ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Taifa wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Prince Bagenda.

Wakati ambapo Mtemelwa alizushiwa kwamba anaongoza kikundi cha kigaidi cha Black Mamba ili kuwadhuru viongozi wanaompinga Mrema katika upande wa kwanza, Bagenda katika upande wa pili aling’olewa kutoka Kamati Kuu ya Chama, lengo likiwa ni kupunguza nguvu za mbunge huyo wa sasa wa Vunjo katika chombo hicho cha uongozi wa kisiasa.

Inawezekana Mtemelwa na Marando katika kipindi hiki hawavutani wala kugombania tena jambo lolote la kisiasa na uongozi wakiwa wote Chadema, lakini mwanasiasa huyo kamwe hawezi kusahau yaliyomkuta ikiwemo kufukuzwa kwenye vikao muhimu vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya NCCR – Mageuzi, vyote vikifanyika kwa vurugu za kijinga kwenye Ukumbi wa Raskazone Hotel mjini Tanga kuanzia Mei 21, 1997.

Mwingine ambaye hawezi kusahau vurugu za Marando za kisiasa ukiwemo uzushi, uongo na fitina kwa wapinzani wake ni pamoja na Harold Jaffu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya NCCR – Mageuzi aliyekuja kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho na hatimaye TLP chini ya Mrema baada ya Bagenda kuachia nafasi hiyo.

Wengine ni pamoja na Thomas Ngawaiya aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa Taifa wa NCCR – Mageuzi na TLP, Hamduni Marcel aliyekuwa Mkurugenzi wa Taifa wa Kampeni na Uchaguzi wa NCCR – Mageuzi iliyokimbiwa na kina Marando na Cosmas Chenyenge, yule ambaye naye alikuwa Mwenyekiti wa vyama hivyo kwa nyakati tofauti wa Mkoa wa Mwanza.

Hao wote na wengineo wanamjua vizuri Marando kuwa kwenye siasa ni mzushi kiasi gani, mfitini wa daraja gani na rafiki namna gani, yule ambaye ana sura na rangi tofauti na yupo radhi na tayari wakati wowote na mahali popote kusema vyovyote, kuanzisha chochote na kung’ang’ania jambo lolote ili mradi tu anakidhi matakwa yake ya muda huo bila kujali kutatokea nini baadaye.

Kama ni kazi ya kutengeneza maneno mezani, kuyamwaga hadharani na kufanana na ukweli basi Marando amefuzu. Aliweza kumfitini Mrema na kila kiongozi aliyekuwa akimuunga mkono walipokuwa wote NCCR – Mageuzi, lakini dhambi hiyo ilikwenda naye sambamba hadi chama hicho kikasambaratika kama kishada kilichokwenda harijojo!

Kilikufa kama kibudu hadi mwenyewe akapoteza mvuto hata kwa wanachama, marafiki na viongozi aliokimbia nao kutoka Manzese Argentina, wakahamia Kisutu ambako walifungua ofisi mpya ya Makao Makuu ya NCCR – Mageuzi huku wakikomba ruzuku yote ya chama.

Ushahidi wa suala hili ni pale alipotaka kurudi tena kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR – Mageuzi kupitia uchaguzi mkuu wa chama hicho wa mwaka 1999. Katika zoezi hilo ambalo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam, Marando na aliyekuwa rafiki yake wa karibu, Dk. Masumbuko Lamwai walitupiliwa mbali na nafasi hiyo ikachukuliwa na James Mbatia ambaye bado anaendelea nayo hadi sasa.

Katika kutaka kwake kuwatetea Mnyika na Lissu kwamba hawahusiki na vitisho vya mauaji dhidi ya Nchemba, hakika shushushu huyo wa zamani wa serikali anajaribu kutwanga maji kwenye kinu, kazi ambayo kwa vyovyote siku ya mwisho itakuja iwe tasa.

Anajaribu kuogelea kwenye bahari yenye kina kirefu cha maji huku mawimbi makali na tena usiku wa manane yakimpiga usoni. Anataka kuwaokoa kutoka kwenye korongo lenye giza nene, lile ambalo bila kutumia umeme hata akikesha anamulika kwa tochi ya betri 10 hawezi kuona mlango wa kuweza kuwatolea.

Kama alivyoshindwa kumng’oa Mrema kutoka katika uongozi wa juu wa NCCR – Mageuzi, akajaribu kumvuruga mpaka kisaikolojia wakiwa kwenye kikao cha NEC kule Tanga, lakini akakimbia yeye mwenyewe usiku wa manane, akahamishia ofisi uchochoroni kutoka Makao Makuu yaliyoandikishwa kisheria; hakika hata juhudi hizi za kutaka kuwaokoa kina Mnyika na Tundu Lissu nazo zitakwama.

Anataka kuitumia nafasi hiyo kusaka umaarufu kwa kudai kuwa ametumia ushushushu wake akiwa ni Kiongozi wa Idara ya Intelijensia ya Chadema, akazichunguza tuhuma hizo kwa siku tatu tu na kugundua kwamba kuna mtoto wa kigogo wa CCM anayemiliki mtambo wa kufanyia ujasusi dhidi ya watu wengine.

Sitaki kuaminishwa uongo na kielelezo siyo kutaja majina ya makampuni yanayotengeneza mitambo hiyo kwa sababu hata kompyuta inafahamika wapi zinatengenezwa duniani, halafu hata Marando mwenyewe anazijua ni kampuni gani zinatengeneza na kuuza ndege za aina zote za Gulf Stream, Air Bus, Boeing, Fokker Friendship, Twin Otter na kadhalika, hivyo anaweza pia kusema chochote akitaka kuibua uzushi wowote kwa kutumia makapmuni hayo kama kigezo cha kuhalalishia uongo wake.

Kama hawadanganyi Watanzania basi atutajie majina kamili ya mtoto huyo wa kigogo wa CCM aliyenunua mtambo huo, aseme ilikuwa lini kwa maana ya tarehe, mwezi na mwaka gani, saa ngapi na atuonyeshe pia risiti ya mauzo hayo na ikiwezekana atuambie hata jina la afisa aliyehusika katika kuuza mtambo huo kule Israel.

Ataje mtoto huyo wa kigogo wa CCM aliondoka Tanzania tarehe ngapi, mwezi gani, mwaka gani na alitumia usafiri gani kama ni wa anga au meli na shirika lake, linamilikiwa na nani na kutoka nchi gani, alianzia wapi safari yake, saa ngapi, alipitia wapi na Israel alifika muda gani.

Aseme alifikia uwanja upi wa ndege au bandari gani nchini humo, akaishi huko kwa muda gani akiwa hoteli gani kabla ya kurudi Tanzania. Ataje pia usafiri aliotumia kwa safari hiyo na takwimu nyingine zote kwa wasafiri wa kigeni wanaokwenda na kutoka nchi nyingine.

Bila kufanya hivyo atakuwa anajaribu tena kurudia kazi iliyomshinda kwa Mrema, halafu akashindwa pia kurejea madarakani kama Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR – Mageuzi kwa awamu ya pili. Akagaragazwa vibaya na Mbatia hadi akatimka kutoka chama hicho na kujisalimisha mwenyewe Chadema.

Endapo amebobea katika uzushi wa kisiasa, majungu na fitina zake sasa namuomba asidhani Watanzania wote ni zezeta wa kufikiri au kutafakari vichwani mwao. Inabidi atafute namna mpya inayoweza kuwaokoa Mnyika na Tundu Lissu kama anataka aendelee kuaminiwa kuwa Kiongozi wa Idara ya Intelijensia ya Chadema.

Kubaki ameng’ang’ania uongo huo hatimaye ataaibika na kama alivyosema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye, shushushu huyo ni mzushi aliyewahi kumsingizia hata yeye, lakini alipombana akaomba radhi kwa maandishi kuwa alishinikizwa kufanya hivyo…“Hata haijapita angalau miezi mitano tu hivi anatoa uzushi mwingine”, anasema.

Huyo ndiye Mabere Marando, Katibu Mkuu wa zamani wa NCCR – Mageuzi aliyeongoza harakati za kukimaliza kisiasa chama hicho kuanzia mwaka 1997 – 1999, yule ambaye sasa anatetea uozo utakaoisambaratisha Chadema kwa kutumia uzushi mwingine![umejitahidi sana kumchafua Marando kwa insha hii, lakini umeshindwa kutofautisha alichokifanya huko NCCR na anachokifanya CHADEMA. kwa maneno yako umeandika kuwa alitaka kuwang`oa akina Mrema na hao wengine uliowataja, katika uongozi wa NCCR. Kwa maneno yako pia umeandika kuwa huyu Marando anataka kuwaokoa akina Mnyika na Tundu Lisu dhidi ya uongo ulionezwa na Mwigulu Mchemba. Kwa maneno yako pia unakubali kuwa Marando anao uwezo wa hali ya juu wa KUANGAMIZA na KUOKOA. Mbona unajichanganya mwenyewe? Tofautisha haya maneno mawili Kuangamiza na Kuokoa, ukiweza kutofautisha utakuwa kwenye nafasi ya kuelewa nini anachokifanya Marando katika ulimwengu huu wa siasa za chuki na fitina za CCM ]
 
umejitahidi sana kumchafua Marando kwa insha hii, lakini umeshindwa kutofautisha alichokifanya huko NCCR na anachokifanya CHADEMA. kwa maneno yako umeandika kuwa alitaka kuwang`oa akina Mrema na hao wengine uliowataja, katika uongozi wa NCCR. Kwa maneno yako pia umeandika kuwa huyu Marando anataka kuwaokoa akina Mnyika na Tundu Lisu dhidi ya uongo ulionezwa na Mwigulu Mchemba. Kwa maneno yako pia unakubali kuwa Marando anao uwezo wa hali ya juu wa KUANGAMIZA na KUOKOA. Mbona unajichanganya mwenyewe? Tofautisha haya maneno mawili Kuangamiza na Kuokoa, ukiweza kutofautisha utakuwa kwenye nafasi ya kuelewa nini anachokifanya Marando katika ulimwengu huu wa siasa
 
umeonyesha nijinsi gani hata jina lako na sehem unayoishi vinavyofanana na hiyo hadith yako
 
Najua kwamba wapo wengi wanaoamini kama mleta hoja hii. lakini kwa hakika tuna maelezo mengi ambayo hayajatolewa kuhusu mtambo wa fake sms.

Binafsi nina ushahidi wa watu ambao wameacha kutumia simu zao baada ya kupokea ujumbe kwenye simu yake kwamba Meseji kwenda kwa mtu fulani imefanikiwa kufika salama. 'your stationed text is delivered to ....... succesfuly'.

Hebu tuwaombe sana acheni kufanya ushabiki kwa serikali bila kufanya utafiti critical.

CCM wenyewe wanajua kwamba huu mfupa umewakwama.
 
Tutasikia mengi, hii story ipeleke kwa mhariri wa gazeti la ijumaa na magazeti mengine ya udaku utauza sana!
 
Back
Top Bottom