Wakati mjadala ukiendelea juu ya kuitambua au kutoitambua NTC, sasa imedhihirika kwamba utawala huo mpya wa waasi utalazimika ku-service deni linalokadiriwa kufikia dola la Kimarekani Trilioni 3 kama gharama na hasara ambazo wanachama wa NATO wameingia kwa kushiriki katika vita vya kumuondoa Colonel Gaddafi. Gharama hizo zinahusisha mabomu, makombora na bunduki na silaha nyingine zilizotumika katika vita hivyo, gharama za ndege zake nane zilizoangushwa na majeshi ya Gaddafi wakati wa mapambano, pamoja na askari waliopoteza maisha katika harakati hizi.
Deni hili kubwa na ambalo litachukua muda mrefu sana kulilipa, litaathiri kwa kiasi kikubwa mapato ya mafuta ghafi ambayo yatakuwa yanasafirishwa na Libya kwenda nchi za nje. Mpango huu ulijadiliwa kwa mara ya kwanza miezi kadhaa iliyopita na unaripotiwa kupingwa na kiongozi wa waasi wa wakati huo aliyekuwa akifahamika kama Yunus na kutokana na msimamo wake huo aliuawa siku moja baada ya kueleza msimamo wake huo kwa viongozi wa NATO. Gharama kama hizi zilirushwa kwa uongozi mpya wa Iraq baada ya utawala wa Saddam Hussein kuanguka na zitaiweka Libya na wananchi wake aktika wakati mgumu kwani italazimika kusalimisha pato lake lote la taifa kwa ajili ya kukidhi matakwa ya watu hawa ambao wakati wote wamekuwa wakionekana na 'wakombozi' wa wananchi wa Libya waliosemekana kuwa katika ukandamizaji wa utawala wa kiimla na wakishetani wa Gaddafi. Baada ya kusherehekea ukombozi huo, sasa watalazimika kujifunga mikanda ili kuwaridhisha 'waliowakomboa'!
Swali linalojitokeza ni kwamba, je, wananchi wa Libya waliridhia mpango huu ambao sasa unawagharimu? Je, kwa nini NATO wameonyesha kama vile walikuwa na nia njema kumbe lengo lao lilikuwa ni tofauti? Je, hii inaweza kuwa ndiyo sababu ya wao kuatoingilia migogoro ya nchi ambazo hazina rasilimali za kutosha ambazo wanaweza kuzitumia kulipia gharama zao kama Somalia, Madagascar na kwingineko?