Elections 2010 BAADA YA KIKWETE: Mgombea mwenza wa NCCR aishiwa nguvu, aanguka jukwaani

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Mgombea mwenza wa NCCR aishiwa nguvu, aanguka jukwaani Send to a friend Thursday, 21 October 2010 10:40 digg

Leon Bahati na Fidelis Butahe

MGOMBEA Mwenza wa NCCR Mageuzi, Ally Omar Juma, ameishiwa nguvu na kuanguka jukwaani wakati akihutubia kwenye kampeni za chama hicho kisiwani Pemba.

Akizungumza na Mwananchi jana, mgombea urais wa chama hicho visiwani Zanzibar, Ambar Khamis Haji, alisema hadi jana jioni hali ya mgombea huyo mwenza ilikuwa mbaya na walikuwa wanafanya taratibu za kumleta jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

"Hali yake ni mbaya, hawezi kula, tangu jana (juzi) tumesimamisha kampeni, majaliwa kesho (leo) tutakamilisha utaratibu wa kumleta kwa ndege huko Dar es Salaam kwa matibabu," alisema Haji.

Alisema matatizo yanayomsumbua mgombea huyo mwenza wa Hashim Rungwe, anayegombea urais Tanzania ni mafua na kifua kubana.

"Akila kifua kinambana na kukohoa sana," alisema Haji akibainisha "Inawezekana matatizo hayo yanatokana na vumbi kubwa ambalo tumekutana nalo hapa Pemba. Yani kuna vumbi sana."

Alisema Jumamosi iliyopita, aliishiwa nguvu na kuanguka jukwaani wakati anahutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kiuyu Jimbo la Mcheweni, kisiwani Pemba.

"Baada ya kuanguka tulimketisha kwenye kiti kwa muda mfupi, akasema ataweza kuendelea. Baada ya kampeni tulimpeleka kwa matibabu katika zahanati moja hapa Mcheweni na kutibiwa, lakini kesho yake hali ikawa mbaya na akawa anabanwa sana na mafua."

Alisema ingawa juzi aliweza kujikokota na kwenda kwenye mazishi ya wanaCCM waliofariki kwa ajali ya gari wakati wakiotoka kwenye mkutano, jioni hali haikuwa nzuri na akawa analalamika kubanwa na kifua.

"Jana (juzi) tulikuwa na mkutano Wete, alishindwa kuhudhuria... Tunachofanya kwa sasa ni kuandaa utaratibu wa kumleta huko Dar es Salaam kwa matibabu," alisema Haji.

Hata hivyo, alisema kwamba bado hawajajua watampeleka hospitali gani, lakini wanaamini ni kwamba uongozi wa NCCR makao makuu watawapangia mara baada ya kuwasili leo.

Akithibitisha tukio hilo Msaidizi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Danda Juju aliliambia gazeti hili kuwa hawezi kulizungumzia kiundani tukio hilo licha ya kukiri kuwa limetokea kweli na tayari wameamua kusimamisha kampeni zao.

“Siwezi kulizungumzia sana hilo suala, mimi nipo katika kampeni za Mwenyekiti (Mbatia), hivyo nina shughuli nyingi sana ila hilo jambo limetokea kweli ila sijui kinachoendelea kwa sasa, wasiliana na Mwenyekiti atakuwa na taarifa zaidi,” alisema Danda.


Taarifa nyingine zilizotolewa na NCCR makao makuu zilieleza kwamba mgombea huyo mwenza hali yake imeonekana ikidhoofu na kwamba atakapoletwa jijini ni kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake.



“Hali hii imetusikitisha kwani baada ya tukio lile tulijua hali yake itaendelea vizuri matokeo yake kila kukicha hali yake inadhoofu hatua iliyotulazimu kusimamisha kampeni zetu,” alisema Danda.


Gazeti hili lilifanya juhudi za kuwasilaiana na Mbatia bila mafanikio kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
 
Tumwombe Mungu ampatie nafuu mapema maana akimchukua, ni yale yale ya 2005 uchaguzi kuahirishwa wakati mpaka sasa umeshaligharimu Taifa pesa kibao.
 
Tumwombe Mungu ampatie nafuu mapema maana akimchukua, ni yale yale ya 2005 uchaguzi kuahirishwa wakati mpaka sasa umeshaligharimu Taifa pesa kibao.

heeeeheeee eeeeh unairishwa mpaka afufuke??sheria za wapi naipenda nchi yangu
 
Ilishatangazwa kuwa uchaguzi utaairishwa kutokana na kifo cha mgombea.
No wonder kuna mtu/watu wanasali hili litokee ili credibility yake/yao isishuke.
 
Back
Top Bottom