Baada ya kikao na IGP Mwema, Dr. Slaa Alonga

Hiyo ndo taarifa ya kikao kuhusu mauwaji?ama ni nusu ya taarifa?

jmushi1 hiyo siyo taarifa ya kikao ila ni taarifa kwa wanacdm kuwa hakutakuwa na mikutano ya m4c for the next 3 days. alitoa taarifa fupi kwa radio 1.
 
Asema baada ya mazungumzo na IGP wamekubali kusitisha mikutano yao ya M4C kwa muda wa siku 3, ili kupisha zoezi la sensa kukamilika kutokana na muda ulioongezwa,


Mie haya niliyajua tu baada yakusema kuwa kuna kikao kati yao. Sasa kwa nn asinge sitisha hivyo tangia mwanzo nakuepusha kifo cha mwandishi? Slaa ni janga la kitaifa
 
Hawa Chadema nao mara nyingine kama wanajichanganya hivi. Mara maandamano yanaendelea mara yanasitishwa. Kuweni na msimamo nyie.
 
Hawa Chadema nao mara nyingine kama wanajichanganya hivi. Mara maandamano yanaendelea mara yanasitishwa. Kuweni na msimamo nyie.

Washangae kwanza polisi wenu kwa kuwa kigeugeu!mara mikutano midogo ruksa mara tunatekeleza maagizo ya mtu asiyejulikana,mara mikutano ya kisiasa marufuku huku mikutano ya kampeni inaendelea yaani ni full kujichanganya.
 
Mwambie IGP aendelee tu kuwaua watu kwaajili ya ccm na serikali yake na shemeji. Kwani wao thamani ya utu wa mwanadamu ni pesa haramu wanazopewa
 
Hawa Chadema nao mara nyingine kama wanajichanganya hivi. Mara maandamano yanaendelea mara yanasitishwa. Kuweni na msimamo nyie.

Ebu kwa mfano unashughulika na mama watoto wako!!! ghafla chaga zinateuka mnakwenda chini!! Je utaendelea kushughulika na hiyo kazi au utaacha kwanza urekebishe kitanda???

Mwandishi kauwawa!! we unahoji kwanini wanasitisha eti!!! kwa nini hawakusitisha kabla! hii ni akili au Bange??
Dk hapa katumia busara tu!ili isimfanye marehemu kana kwamba alikuwa akifanya kazi ya cdm!! alitakiwa kusema tunasitisha M4C kwa sababu ya msiba wa mwandishi wetu!!
 
taarifa kuhusu mauaji amesema jeshi la polisi bado wanachunguza na wao kama Chama watatoa taarifa yao baada ya uchunguzi

vipi Dr.Slaa anaamini polisi watatenda haki kwenye huo uchunguzi.??
 
chadema inabidi itoe msimamo kuhusu hili la tume ya polisi kuendelea kuchunguza kuua yenyewe, kujichungunza yenyewe na kuandika ripoti ya mauaji waliyoyafanya wao wenyewe. chadema must categorical condemn this process. Any findings will be considered injustice and against rule of law then must be condermed by peace lovers all over the world.
 
Kwaiyo maisha ya jamaa yamepotea hivi hivi tu, alikua wapi kusubiri? Je anaona faida ya lolote na liwe? Kwakweli nimemzarau kabisa huyu mzee.

Mzee yupi ? Yule Police ? Maana Picha zinaonyesha Police kama watano hivi wamemzonga Mwandishi wa Habari, na Police mmoja, anamkandamiza Mwandishi wa habari Mashine kubwa tumboni ambayo mwishoni inaelekea ililipuka na kumwua ( Nimesoma vizuri report ya CNN, ikilaani vitendo vya Police wa Tanzania vya kupambana na raia). So ni vita kubwa kati ya Police na Mwandishi wa habari, sasa huyo mzee anaingiaje ? mbona hawakumpiga yeye ? Pale Morogoro pia, mbona walimpiga kijana muuza magazeti na hawakuwapiga hao wanaosema wanaleta vurugu ? Police wameua mwandishi wa habari. Ni hatari kubwa sana. Yeye alikuwa anatafuta news ili atujulishe watanzania wenzanke kile kinachoendele, kosa lake ni nini ? Na sisi tunaojadili ni vyema tujadili kile kinachoonekana mbele yetu (Tujadili tendo la police kuua raia tena mwandishi wa habari, ambaye alikuwa kazini kwake. NAPITA TU !
 
Kama ataishia kueleza kuwa anasitisha mikutano tu, basi ategemee kuambiwa kuwa CDM ndiyo iliyosababisha kutokea mauaji baada ya kukaidi kusitisha mikutano yake ili kupisha sensa. Inatakiwa aonyeshe vielelezo kuwa walikuwa na uhalai wa mkutano ule uliozuiliwa kimabavu na kusababisha kifo. Hawa jamaa si wakuwaamini tena, maana majibu yao tangu Dr.Ulimboka saga, kifo cha Ally Zoka wa Morogoro na sasa tutarajie taarifa ya kuichanganya umma na kupoteza ushahidi kwa polisi kuhusika licha ya mauaji hayo kuonekana waziwazi pamoja na kuwepo vielelezo vilivyokuwepo.
 
CDM wanaandaa tarifa yenye maelezo ya kina. Si vema wakakurupuka kusemea jambo hili ila nina imani kubwa kuwa wanalifanyia kazi. Tuwe na subira ila Makene tupe yaliyojiri humo jumba la kikao.
 
Back
Top Bottom