Baada ya kichapo Igunga: CCM yashauri serikali kufuta chaguzi ndogo...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
BAADA ya kupata ushindi mwembamba katika chaguzi mbalimbali ndogo za ubunge likiwamo Jimbo la Igunga, CCM kimeiagiza serikali iweke utaratibu mpya kuondoa chaguzi hizo, imefahamika.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa uamuzi huo wa chama ulitolewa katika kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho iliyofanyika Dodoma hivi karibuni.

Taarifa ya uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Igunga iliyotolewa na Sekretarieti ya Organaizesheni ya chama hicho kwa wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC), inaeleza kuwa ili kuondokana gharama na vitendo vya uvunjifu wa sheria vilivyojitokeza katika chaguzi ndogo zilizopita, utafutwe utaratibu mpya wa kumpata mbunge bila ya kufanyika uchaguzi.

"Chama kiielekeze serikali itafute utaratibu mwingine wa kisheria wa kuondokana na chaguzi ndogo, lakini bila ya kubadilisha mfumo uliopo," inaeleza sehemu taarifa hiyo.

CCM imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa kutokana na chama hicho kutumia fedha nyingi katika chaguzi ndogo katika majimbo ya Tarime, Busanda na Igunga na vitendo vya uvunjifu wa amani vilivyojitokeza.

Chama hicho kinaeleza kuwa hatua hiyo ya kufuta chaguzi ndogo haitavunja katiba kwa sababu kinachoweza kufanyika ni kubadilisha vifungu vya sheria ya uchaguzi.

"Hili sio suala ambalo linagusa katiba ya nchi, bali linaishia kwenye sheria ya uchaguzi," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza;

Badala yake yafanyike mabadiliko katika vifungu vya sheria ya uchaguzi vinavyozungumzia chaguzi ndogo; hususan kifugu cha 46 (2) cha sheria hiyo.

Kifungu hicho kibadilishwe na kusomeka hivi: Wabunge waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliotangulia, chama cha siasa ambacho kilikuwa na mbunge wa jimbo kipewe nafasi ya kumpendekeza mtu mwingine wa kujaza nafasi hiyo kwa Tume ya Uchaguzi.

Hata hivyo, Chama hicho kimeeleza kuwa mchakato huo wa kumpata mtu atakayechukua nafasi ya mbunge aliyekuwapo ndani ya chama unapaswa kufanyika kwa njia ya kidemokrasia.

Katika uchaguzi mdogo wa Igunga, Mgombea wa CCM, Dk Peter Kafumu aliibuka mshindi kwa kupata kura 26,484, akifuatiwa na mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye aliyepata kura 23,260 huku mgombea wa CUF, Leopold Mahona akiambulia kura 2, 104.

CCM katika uchaguzi huo inadaiwa kutumia nguvu kubwa ya fedha wakati wa kampeni ikiwamo kutumia helikopta, magari na timu kubwa ya viongozi chama hicho, mawaziri na viongozi wastaafu.

Vilevile, vyama vya upinzani vya Chadema na CUF navyo vilitumia helikopta katika kampeni hizo hali ambayo iliongeza ushindani zaidi katika uchaguzi huo uliotawaliwa vitendo vya vurugu ikiwamo, baadhi ya watu kujeruhiwa, kumwagiwa tindikali, Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario kuwekwa chini ya ulinzi na makada wa Chadema na nyumba kuchomwa moto.

Chama hicho pia kimeeleza kuwa uchaguzi huo mdogo wa Igunga umekipa funzo kuwa chama hicho hakiko karibu na vijana, wasomi na wanahabari na sasa kinapendekeza mkakati wa kuhakikisha kuwa makundi hayo wanakuwa nayo sawa.

Kimeeleza kuwa makundi hayo katika chaguzi zilizopita waliyaacha mbali na ndicho kiini kupoteza baadhi ya majimbo kwa wapinzani katika baadhi ya maeneo nchini hususan ya mijini.

Majimbo yaliyokuwa ya CCM kabla uchaguzi mkuu uliopita ambayo hivi sasa yamekwenda Chadema ni Nyamagana lililopo Mwanza mjini, Jimbo la Mbeya na Jimbo la Arusha mjini.

Ili kuondokana na udhaifu huo, chama hicho kimeagiza watendaji wa chama kuhakikisha makundi haya wanakuwa nayo karibu kwa kuwafanyia semina, kongamano na njia nyingine ambazo zinaweza kuwapo.

Wachambuzi wa mambo ya siasa nchini na baadhi ya makada wa chama hicho, wanasema kuwa wasiwasi wa CCM kuendelea kufanyika kwa chaguzi ndogo unatokana na vyama vya upinzani hususan Chadema kuzidi kupata nguvu huku chenyewe kikikosa mvuto kwa wananchi.

"Sio mchezo uchaguzi wa Igunga umetupa funzo kubwa sana kwamba sasa chaguzi ndogo za ubunge sio za kukimbilia tena zinaweza kukimaliza chama, kwani kama tungepoteza jimbo la Igunga tulikuwa tumekwenda na maji," alidokeza kada mmoja ya CCM ambaye hakupenda kutajwa jina.

Hata hivyo, ibara ya 76 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Uchaguzi na Uteuzi wa Wabunge inaeleza kuwa kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katika jimbo la uchaguzi, ikiwa kiti cha Mbunge yeyote aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo hilo kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge.

Mara baada ya matokeo ya uchaguzi huo kutangazwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliishutumua Chadema kwa kusababisha chama chake kupata ushindi mwembamba kutokana wananchi wengi kushindwa kujitokeza kupiga kura kutokana na chama hicho kuingiza vijana 800 kutoja nje ya jimbo kuwatisha watu.

Alisema ushindi huo waliopita unatokana na kuanza kutekeleza kwa falsafa ya kujivua gamba iliyoasisiwa na Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete Februari 5 mwaka huu.

Kupoteza umaarufu wa chama hiki tawala kulianza kuonekana katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka jana baada ya mgombea wake wa kiti cha urais, Kikwete ushindi wake kushuka kutoka asilimia 81 alizopata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 hadi asilimia 61.

Katika uchaguzi wa mwaka jana, Rais Kikwete alipata kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 huku akifuatiwa na mgombea wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliyepata kura 2,271,941 ambazo ni sawa na asilimia 26.34.

Mbali ya Rais Kikwete ushindi wake kupungua, pia chama hicho kilipoteza majimbo mengi kwa wapinzani, huku vijana na wasomi wengi wakionekana kuvutiwa na sera za upinzani.

Jairo, Luhanjo, Ngeleja

Kuhusu uamuzi wa Bunge kupendekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini aliyesimamishwa, David Jairo na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Ludovick Uttoh kuwajibishwa, CCM imeridhia uamuzi huo.

CCM imepongeza serikali kwa kupokea maazimio ya Bunge kuhusu suala hilo, hali ambayo inaonyesha wazi kuwa chama hicho kinataka viongozi hao wawajibishwe kutokana na kashfa ya Jairo kuchangisha fedha za kusaidia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ipite bungeni kinyume cha taratibu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Ramo Makani akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo bungeni hivi karibuni, alisema baada ya kamati yake kufanya uchunguzi uliowezesha kuwahoji watu 146, imebainika kuwa utaratibu uliotumiwa na Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kutoka katika taasisi zilizoko chini ya wizara hiyo kwa ajili ya kusaidia upitishaji wa bajeti bungeni, haikuwa wa kawaida na kwamba ulikiuka taratibu na Sheria za Fedha.

Alisema utafiti ulibaini kwamba, Jairo akiwa Katibu Mkuu aliomba fedha kiasi cha Sh180 milioni kutoka taasisi nne ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililoombwa Sh40 milioni, Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) Sh40 milioni, Wakala wa Umeme Vijijini (REA) Sh50 milioni na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Sh50 milioni.

Hata hivyo, kiasi kilichochangwa ni Sh140 milioni tu kutoka Tanesco, REA na TPDC, wakati Ewura waligharamia chakula cha mchana kwa siku tatu pamoja na tafrija iliyokuwa imepangwa kufanyika baada ya kupitishwa kwa bajeti ambayo iliwagharimu Sh9.7 milioni.

Waziri Ghasia

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia alisema kuwa, suala la Jairo lipo kwa Waziri Mkuu hivyo ndiye atakayeweza kulizungumzia.
"Hilo suala mumuulize Waziri Mkuu, kwa sasa lipo chini yake yeye ndiye anayeweza kulitolea ufafanuzi," alisema Ghasia.

Hata hivyo, pamoja na serikali kuridhia maazimio ya Bunge ya kuwawajibisha wahusika, lakini mpaka leo hakuna hatua zilizochukuliwa. Katibu Mkuu Kiongozi, Luhanjo anatarajiwa kustaafu mwezi huu.

Vurugu za Mwanza, Arusha Mbeya

Kuhusu vurugu zilizoibuka katika miji ya Mwanza, Arusha na Mbeya mwaka huu na kusababisha vifo na uharibifu wa mali, Kamati Kuu ya chama hicho ilipendekeza kuwa dola ichukue hatua haraka kudhibiti vitendo hivyo na kwamba viongozi wa vyama vya siasa wanaojihusisha na kuchochea vurugu wakamatwe.

Ili kukabiliana vurugu hizo, CCM imeiagiza serikali kuharakisha kutatua matatizo yanayowakabili vijana wanaoishi maeneo ya mijini, hususan tatizo la ajira na kuwapatia maeneo ya kufanyia biashara ndongondogo.

"Pale ambapo itahitajika kufanya operesheni za kuwaondoa vijana katika maeneo wasiyostahili kufanya biashara katika maeneo ya mijini , basi busara itumike na sio nguvu kubwa kupita kiasi," sehemu ya mapendekezo ya kamati huu inaeleza.

Vilevile, Kamati Kuu ilitaka kikosi chake cha ulinzi cha vijana maarufu 'Green Guard' imepewe mafunzo zaidi ya kukabiliana na hujuma zinazofanyika za kushambuliwa kwa majengo na mali za chama katika maeneo mbalimbali nchini.

CCM imeenda mbali zaidi na kuitaka serikali kubadilisha mfumo wa elimu ya darasa la saba na kidato cha nne ili wanafunzi wanaopata elimu hiyo wafundishwe na elimu ya ufundi ambayo itawawezesha kupata ajira.


Source: Mwanachi Jumapili
 
Wanachomaanisha hawa Magamba ni kua tuwe tunachagua chama sio mtu,
So chama ndio kiweke mtu awe mbunge!!
Akifa huyo mtu basi chama kichague mtu mwingine!!
Wakati tupo kwenye mchakato wa kuondoa huu urasimu wa mgombea kupitia Chama bali awepo na mgombea binafsi, magamba wanatazamia kushinikiza tuwe tunachagua chama!!!!
 
Tunataka tamko la chadema mapema kuhusu hili tamko,inavyoonekana ni vita ya waziwazi dhidi ya chadema na demokrasia Tanzania.Huu ni mpango uliosukwa vema kati ya ccm na cuf.Nasikia yatapelekwa marekebisho bungeni bunge la February na yatapitishwa na wabunge wa vyama rafiki ccm na cuf.Inasemekana tayari mpango huu wa ccm ulishapelekwa katika vikao vya juu vya cuf na kukubaliwa.
 
Sasa naelewa kwa nini Kikwete ametunuku nishani Makinda. Huyu mama anaua demokrasia mchana kweupe na kama hili la kupata mbunge bila kufanya uchaguzi ni kielelezo tosha.

Nahisi CCM wanahofia wabunge wengi wanaweza kujiuzulu before 2015 na kusimama kwenye chaguzi ndogo kupitia tiketi ya vyama vya upinzani. Sasa ili kuziba hiyo threat Makinda kama kawaida ataandaa timu ya watoa matusi, Celina Kombani na Werema wake wateleta muswada wa kupata kupata mbunge kwa njia ya 'utawala wa kifalme' na utaungwa mkono na watoa matusi.

Tanzania tunarudi nyuma kwa kasi ya kutisha.
 
Hawatapona, ccm lazima itakufa! wingi wa hila hautawaokoa kamwe.
 
Chadema iongoze wananchi kulaani ubakwaji huu wa demokrasia unaofanywa na ccm na cuf
 
Wanachomaanisha hawa Magamba ni kua tuwe tunachagua chama sio mtu,
So chama ndio kiweke mtu awe mbunge!!
Akifa huyo mtu basi chama kichague mtu mwingine!!
Wakati tupo kwenye mchakato wa kuondoa huu urasimu wa mgombea kupitia Chama bali awepo na mgombea binafsi, magamba wanatazamia kushinikiza tuwe tunachagua chama!!!!

Mimi nashangaa sana sijui ukiwa chama cha magamba basi ufikiri wako unakomaa? Wanafikiri hiyo ndiyo soln?
 
Na hilo ndilo naloliona kuwa kuna lengo la kuzuia kupoteza majimbo,wanatambua kuwa wanaweza kupoteza majimbo mengi sana kama uchaguzi ukiitishwa leo,na kwahiyo ili kukwepa hilo wanatafuta njia ya kuzuia mapema upepo huu...kuna fununu kuwa kuna majadiliano kuondoa hizi ruzuku na lengo ni kuua nguvu ya CDM,na CUF wamepewa wataendelea kula kupitia ndoa yao na hawa magamba...
 
hawa jamaa hawa, yani ni aibu sana kwa chama kilichokuwa kinasifika africa kuanza kufikiri na kutenda mambo ya 1956 katika dunia ya leo.
Hawa ni wabakaji wa demokrasia.
Swala la matumizi ya fedha nyingi. Serikali haijalalamika kushindwa kuendesha chaguzi ndogo. Kama wao wametumia fedha nyingi wanatakiwa wajiulize ni kwa nini.

Nasema ipo siku wananchi watajua kutumia mabomu ya petrol na sukari. Ccm inatupeleka kwenye siku hiyo.
 
Na hilo ndilo naloliona kuwa kuna lengo la kuzuia kupoteza majimbo,wanatambua kuwa wanaweza kupoteza majimbo mengi sana kama uchaguzi ukiitishwa leo,na kwahiyo ili kukwepa hilo wanatafuta njia ya kuzuia mapema upepo huu...kuna fununu kuwa kuna majadiliano kuondoa hizi ruzuku na lengo ni kuua nguvu ya CDM,na CUF wamepewa wataendelea kula kupitia ndoa yao na hawa magamba...

hilo la ruzuku na mimi nimelisikia kutoka kwenye vyanzo vya uhakika. It is a sad.
Ccm wanajua kwamba wataendelea kichukua fedha zaa serikali kwa mbinu walizozizoea na watawapatia wake zao za mboga kidogo.
Wanashindwa kujua kwamba harambee iikianziswa ya kila mpenda demokrasia atoe sh 1000 cdm inaweza kipata zaidi ya 5,000,000,000 kila baada ya miezi mitatu.
 
Kweli ccm imeshikwa pabaya! Hawawezi tena kutumia akili! Wanafanya staili ya kulikimbia tatizo badala ya kulikabili.

Wapo kwenye mchakato wa kuunda katiba mpya huku wakifikiria kufanya ukarabati wa ile ya zamani!

Vijana tusimame na kukataa kwanza kuzuiliwa kwa maandamano na mikutano ya siasa maana wazee hawa wanatuhabiria taifa. Kisha tutoke barabarani kupinga hizi sheria za kipuuzi wanazoziweka ccm ili kujilinda.
 
Tunataka tamko la chadema mapema kuhusu hili tamko,inavyoonekana ni vita ya waziwazi dhidi ya chadema na demokrasia Tanzania.Huu ni mpango uliosukwa vema kati ya ccm na cuf.Nasikia yatapelekwa marekebisho bungeni bunge la February na yatapitishwa na wabunge wa vyama rafiki ccm na cuf.Inasemekana tayari mpango huu wa ccm ulishapelekwa katika vikao vya juu vya cuf na kukubaliwa.

Ndugu yangu hapa hakuna cha kusema chadema, dawa ni sisi wenyewe kujiandaa kuvamia Dodoma kila pembe. Tuhamasishane kila kona mswada ukisomwa na sisi tupo mlangoni ili wajua wenye nguvu ni watawaliwa au ni watawala. Hawa watu hawawezi kutupeleka kama mapimbi hakuna aliyezawa na kuhalalishiwa kutawala milele.
Na Makinda asipoangalia vizuri wananchi watamvamia hapo Dodoma, na ndio itakuwa mwisho wao na Kikwete. Kama ni kweli tunaomba lipaaziwe sauti ili wananchi wajiandae vema kwa February.
 
Chadema wanapaswa kuwa wakali katika hili,hiyo ndio gharama ya kuwa kiongozi wa upinzani.Freeman Mbowe afahamu kwamba akiruhusu uharamia huu kupitishwa kamwe historia haitamsamehe!
 
hivi mnazani hii nchi ni ya chama kimoja na huo utaratibu maalumu mnajua madhara yake hiyo itapelekea wabunge kuuwawa watu wakitengeneza mazingira ya kuteuliwa kurithi kiti.Mmesahau kuwa mbuge ni mwakilishi wa watu waliyomchagua? Siungi mkono mawazo yenu hata kidogo
 
Ndugu yangu hapa hakuna cha kusema chadema, dawa ni sisi wenyewe kujiandaa kuvamia Dodoma kila pembe. Tuhamasishane kila kona mswada ukisomwa na sisi tupo mlangoni ili wajua wenye nguvu ni watawaliwa au ni watawala. Hawa watu hawawezi kutupeleka kama mapimbi hakuna aliyezawa na kuhalalishiwa kutawala milele.
Na Makinda asipoangalia vizuri wananchi watamvamia hapo Dodoma, na ndio itakuwa mwisho wao na Kikwete. Kama ni kweli tunaomba lipaaziwe sauti ili wananchi wajiandae vema kwa February.

mkuu Fastafasta umesema vema.Lakini fahamu kwa hali hii ni lazima tuwe na kiongozi.Na chadema wanapaswa kutuongoza kwa sababu wao ndio walengwa wa mpango huu haramu.
 
Ukiona mtu aliyekuwa anadhaniwa ana akili anaanza kufanya mambo kama haya ujue anakaribia kukata roho. Magamba kila wanaposhika pana joto siku si nyingi wata - give up.
 
Mapendekezo hayo inasikitisha ya kwamba hayakubahatika kuhemewa hewa safi ya UHURU WA KUCHAGUA na dhana zima ya demokrasia ya uwakilishi kama ilivyotamkwa na katiba yetu.

Pamoja na gharama zake zote, demokrasia ya uchguzi mdogo haina mbadala yake chini ya katiba ya sasa.
 
Nafikiri CCM wanafanya 'destructive experiments' ili kupata njia ya kutokea. Kama wameanzisha mchakato wao wa Katiba kwa nini wasielekeze nguvu zote huko na kuhakikisha kifungu hicho kinapitishwa badala ya kufikiria sheria za kuua demokrasia?. Walijaribu mfumo wa primaries umewatokea puani, sasa wanataka kuleta mfumo wa kuteuana katika nafasi za uwakilishi wa wananchi.

CCM hivi sasa ina vichwa ambavyo kila siku vinafikiria jinsi gani vitajaza sahani zao hata kama cha kujazia ni ukoko na matandu yaliyo chacha. Mawazo kama haya ni dalili kuwa hata katiba mpya wanayodai wanaiasisi wanajua itakuwaje na kushirikisha wananchi kutoa maoni ni kuwapotezea muda wao. What if wananchi watataka mtu asiyekuwa na chama agombee ubunge na huyu akifa naye wataokota mtu mtaani na kumteua?.

Mfumo huu wanaoufikiria utakuwa ni sumu kwao kuliko hata mfumo wa primary voting alioupendekeza Dr Bilal. Kama mimi ni mbunge niliye ndani ya bunge la sasa bila kujali kuwa ninatoka chama gani mfumo huu ni toxic kwangu. Mfumo huu utaondoa nguvu ya wabunge waliomo bungeni kwani nafasi watakazokuwa wanashikilia hazitakuwa za wananchi bali za chama. Hiyo gharama ya uchaguzi mdogo ambayo chama inaiogopa ndiyo price tag na pia security ya mbunge aliyepo madarakani. Kama gharama hii haipo, mbunge anaweza kuadhibiwa na chama kwa kufukuzwa wakati wowote kwa fitina tu na mtu mwingine kuteuliwa kushika nafasi yake. Hii itawafanya wabunge wazidi kuwa watumwa zaidi wa watu wachache ndani ya chama. Pia unatoa mwanya kwa ugaidi dhidi ya wabunge, mfano katika vinyang'anyiro vya uteuzi hakuna hata mmoja anyeshindwa anafurahia mwenzake kuchaguliwa, possibility ni kuwa hawa wanaweza kutafuta wauaji na kumuondoa duniani mtu anayeshikilia nafasi wakidhani wanaweza kuteuliwa kuchukua nafasi zao moja kwa moja hata kama haitakuwa hivyo.

This is a worse idea I have ever seen in any democratic society, only psycho can come with this sycophant idea. Haya ni mawazo ya watu wavivu wanaoogopa challenges za uongozi toka kwa wananchi na hivyo wanaona njia pekee ya kukaa miguu juu ni kupigana tooth and nail katika uchaguzi mkuu then baada ya hapo ni kula kuku kwa miaka mitano. CCM kama inafanya kazi za wananchi isihofie chakuzi ndogo bali wazione kuwa ni changamoto za kuwaamsha usingizini kwa faida ya Taifa na maendeleo yetu. Waache mentality ya kuonekana kuwa ushindi katika uchaguzi ni kipimo cha uongozi katika chama. Igunga imewaumiza sana kwani kwa kina Mukama na wenzake walioingizwa katika uongozi wa chama ile ilikuwa na test yao ya kwanza kuhusu ufanisi wao katika chama. Matokeo yake wakajikuta wanaandaa vikundi vya ujasusi na ugaidi kutisha na kuua wananchi ili wao waonekane mbele ya NEC yao wamefanya kazi nzuri na kuwahakikishia ulaji endelevu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom