Elections 2010 Baada ya JK kumaliza ZIARA yake Kanda ya Ziwa

Mwandishi Wetu,Mpwapwa

POLISI katika Wilaya ya Mpwapwa, wameahidi kuendelea kupambana na wachimbaji wadogo wa madini katika kijiji cha Winza, wilayani humo kama watu hao wataendelea kung'ang'ania kuchimba madini.

Msimamo huo ulitolewa juzi Mkuu wa Polisi wilayani humo, Zedekia Makunja, ambaye alisema hatua hiyo inalenga katika kuwadhibiti wachimbaji katika machimbo hayo yasiyo rasmi.

Msimamo huo ulikuja kufuatia mvutano mkali uliotokea juzi kati ya pande hizo mbili kiasi cha kuwalazimisha polisi, kutumia nguvu za ziada, ili kuwaondoa wachimbaji.


Habari za awali zilisema wachimbaji hao wamevamia eneo hilo na kuanza kuchimba madini bila vibali vinavyowaruhusu kufanya hivyo.

Mwandishi wa habari hizi katika eneo la tukio, alishuhudia vurugu kubwa kati ya wachimbaji wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 2,000 na asari polisi.


Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa, aliwataka wachimbaji hao kuondoka katika eneo hilo na kuwapisha wenye leseni, kuendelea na shughuli za uchimbaji.


Akizungumza kuhusu hatua ya askari kutumia nguvu za ziada, Mkuu huyo (Makunja) alisema hatua hiyo ililenga katika kuhakikisha kuwa wachimbaji hawaendelei kuwa wakaidi na kuvunja amani katika eneo la machimbo.

"Askari wapo kwa ajili ya kulinda amani, hawawezi kurusha risasi bila sababu. Tatizo ni kwamba wachimbaji walikaidi amri na kibaya zaidi walianza kutoa maneno machafu na kuwarushia mawe askari," alisema Mkunja.



Alisema wachimbaji wote wasikuwa na leseni waliambiwa ama watoke au waungane na wenye leseni lakini wao walikaidi.

----mwananchi

 
Back
Top Bottom