Baada ya bili ya umeme sasa ushuru wa mkaa

Mdede

New Member
Jan 14, 2011
2
0
Hi JF, Serikali baada ya kupandisha bill ya umeme kwa 18% sasa nimeona wizara ya maliasili imetangaza kuchukua ushuru kwa watumiaji wa mkaa. Tangazo ambalo limetolewa kupitia star tv kuwa watakatisha ushuru kwa watumiaji wa mkaa wote hata kama ni wa kutumia nyumbani kama utakuwa hujakatia ushuru mkaa utataifishwa na mhusika kushtakiwa. Wameona wakiwakamua watumiaji wa umeme tu haitoshi sasa wanarudi hadi kwa walala hoi. Mi sìilewi hii serikali ya awamu ya nne inawatakia nini raia wa tz. Sasa wanataka hata kula tusile ili tufe na njaa. Bado kidogo watakatisha ushuru wa kuni za majumbani. Wanahakikisha wanatukamua hadi tukome. Mi ni mgen kama kunamahali nimekosea naomba nielekezwe. Naomba kuwasilisha.
 
Ndo imekula kwetu Wadanganyika. Umeme juu, maji unit 850, mkaa ushuru juu, vyakula bei juu, sukari leo nimenunua 2000 kwa kilo, mafuta ya kupikia kindoo kidogo 25,000 we acha tu tutakoma
 
Mkuu mimi bado sijakuelewa hapo kwenye ushuru ni kwa mtumiaji au mfanyabiashara wa mkaa na kama kwa mtumiaji wa Mkaa watatumia njia gani za kuwatia hatiani watumiaji au ndo kila utakapo kutwa na Mkaa ni kosa na unawekwa ndani.
 
Na bado...mpaka kuni nazo zikatiwe ushuru ndo wale ambao bado hawajaamka nao wataamka!
 
Kweli nimesikia nikashangaa sana... Eti lazima ununue mkaa uliolipiwa ushuru kama haujalipiwa utapashwa kulipiwa... Sasa jamani huu si wizi????

Kweli jk aondoke sasa wakati ni huu..... Plz go and live our country.......
 
Sawa sawa tuu. Mkaa unaumiza nchi doing irreparable damage to our forests and environment in genera. It should be taxed enough to counter the effect it leaves in terms of the carbon footprint as well as other conservation methods.
 
Kinyambiss said:
Sawa sawa tuu. Mkaa unaumiza nchi doing irreparable damage to our forests and environment in genera. It should be taxed enough to counter the effect it leaves in terms of the carbon footprint as well as other conservation methods.
Hakuna mtu asiyejua ubaya wa matumizi ya mkaa, hata sisi masikini wa Tanzania tunajua. Tatizo kwa $erikali kandamizi ya CCM ni kuwa wameifisadi Tanesco mpaka imeshindwa kutoa nishati mbadala kwa gharama nafuu.

Huwezi kutoza ushuru kwa kisingizio cha kupunguza matumizi ya mkaa wakati hujatoa suluhu mbadala, huu ni unyonyaji!! Alert, hakuna wananchi waliokuwa royal kwa watawala wao kama Arabs, lkn sasa hivi ni machafuko kila kona kwa sababu ya mambo kama haya yanayofanywa na $erikali ya CCM.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom