Baada ya beef zito na Clouds FM: Lady Jaydee kuanzisha Radio yake

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Baada ya mwanadada nguli katika bongo flavour msanii Lady Jaydee kuwatolea uvivu radio ya watu (Clouds FM) kuwa hawapigi nyimbo zake mpaka wapewe rushwa sasa ameamua kuja na kituo chake cha redio.

Mwanadada huyo kafunguka kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa "Kwanza FM coming soon. Yangu mwenyewee".

Naona Lady jaydee aliamua kuwa strategic kwa kukaa kimya wakati ananyonywa na clouds fm pamoja la Ruge. Baada ya kuweka mambo yake sawa (kufungua kituo chake cha radio), kaamua kuwachana live clouds fm.

Maoni yangu: Ajiadhali tu na fitna za Ruge, hii radio isije ishia kwenye makaratasi tu. Ruge kakamata entertainment industry hapa Tanzania, yeye ndio Don, anaamua nini au nani afanikiwe kisanaa au nani afie mbali.

Otherwise, congrats binti komando aka binti machozi
 
Kama Mtangaji Abdallah Majura kaweza kuwa na Radio yake pale Dodoma(Sports FM), CCM hapa Lumumba tuna redio yetu(Radio Uhuru), kwanini Lady JD ashindwe?

Mwanadada 'Komando' songa mbele utafika tu.
Uliweza kuwa na Live Band yako(Machozi Band), Ukawa na Mgahawa wako(Nyumbani Lounch), Ukawa na Brand ya bottle water Pack yako(?!) kwanini ushindwe kuwa na Fm radio yako?
 
Majura amepewa tu kusimamia sio Radio yake!Hongera Mdada kaza buti ila ndio umeingia anga zao kwa nyodo hivyo?jiandae kweli kweli maana ushindani mkali sana sana na hivyo una hasira nao watakufanyia makusudi mengi ingawa sina hakika kama Kaka yako Joseph ana visasi!
 
Af Gadner ndo manager vipindi km kawa dada big up sna Jide na mshauri wako mkuu Gadner!
 
Me nafikiri swala hili inabidi tulichukue kwa upana zaidi sidhani kuanzisha Radio ni suluhu ya tatizo la wasanii na matitizo haya hayamuhusu jaydee pekee bali ni wasanii wengi!

Maana hapa kuna vituo vya radio na pia kuna mapromoter wa kazi zao amoja na show zao na ninge Mshauri jaydee hatua ya haraka kwa sasa ya kuchukua ni kuakisha wasanii hasa wakongwe na wengine wana kuwa na umoja maana wasanii wengi wanategemea show na huko kwenye show ndio wana nyonywa sana maana sidhani kama wanalipwa kulingana na jasho lao, na hili kuhakikisha wana wabana vilivyo hawa watu wanao jihusisha na kupromote music lazima wasanii hasa wakongwe wawe na sauti moja hata wakiweza kupanga kima cha chini cha malipo kwenye show.

Pengine watu wanadhani kutopigiwa nyimbo kwenye radio ndio tatizo pekee lakini sivyo,hawa wasanii wanazunguka wakipiga show lakini wanabaki maskini kila leo.

Hivyo ni wazi jaydee ajue kuwa kuanzisha Radio si suluhu la pekee la matatizo yao!

Ni vyema akatafuta njia ya umoja ili asije akapoteza mpambano mapema!
 
Baada ya mwanadada nguli katika bongo flavour msanii Lady Jaydee kuwatolea uvivu radio ya watu (Clouds FM) kuwa hawapigi nyimbo zake mpaka wapewe rushwa sasa ameamua kuja na kituo chake cha redio.

Mwanadada huyo kafunguka kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa "Kwanza FM coming soon. Yangu mwenyewee".

Naona Lady jaydee aliamua kuwa strategic kwa kukaa kimya wakati ananyonywa na clouds fm pamoja la Ruge. Baada ya kuweka mambo yake sawa (kufungua kituo chake cha radio), kaamua kuwachana live clouds fm.

Maoni yangu: Ajiadhali tu na fitna za Ruge, hii radio isije ishia kwenye makaratasi tu. Ruge kakamata entertainment industry hapa Tanzania, yeye ndio Don, anaamua nini au nani afanikiwe kisanaa au nani afie mbali.

Otherwise, congrats binti komando aka binti machozi
who is ruge? where is makaveli and B.I.G?
 
Msanii nguli wa kizazi kipya lady jay dee yuko mbioni kudondosha kituo chake mwenyewe cha radio kitakachoitwa KWANZA FM.
 
Mmmmh, ili apige nyimbo zake tu au ndio mambo ya ujasiri Amali?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
vyema tena ni khaki, nafikiri yeye na mumewe wana uzoefu wa kutosha na media industry, wana influence flani so mambo ya matangazo pia watafanikiwa,

kila la heri mwanamke komando
 
Mmmmh, ili apige nyimbo zake tu au ndio mambo ya ujasiri Amali?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

heeeeeeeeeeee watu wengine bwana,hiyo redio redio gani kwamba wao masaa 24 awe anapiga nyimbo zakeeeeee tu,where on earth have you seen that
 
Back
Top Bottom