Baad ya idara za Jeshi la Polisi Zimebinafsishwa?

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Kwa wanaJamii wote
Salamu, Natumaini kuwa Jumapili hii imewakuta wote mkiwa wazima wa afya.
Kama tulivyoshuhudia kuwa kitengo cha Parking katika kila Jiji na manispaa zetu kimekwisha binafsishwa. Hali kadhalika usafi wa manispaa na jiji vyote viko mikononi mwa wanainchi wafanyabiashara. Kuna hizi kampuni za binafsi za Ulinzi zimekwishaingia katika kusaidi na kama sio kuondoa kabisa uwajibikaji wa Jeshi la Polisi wa Ulinzi wa Raia wa Tanzania na mali zao. Nasema hivi kwa sababu kila mtu na kila mashirika ameajiri kampuni ya kulinda mali zake. Jeshi liko likizo na wengi wao sasa wanashinda baa kutwa nzima wanapombeka tu. Ndio! Hawana kazi za kufanya. Wafanye nini? Kila kona kuna walinzi binafsi?
Kali mbayo inanifanya niandike hapa ni pale hata kazi ya askari wa usalama barabarani imechukuliwa na kampuni binafsi. Ninasema haya kwa sababu siku za hivi karibuni kuna hawa askari wapya wanaojiita askari WRONG PARKING.
Sina hakika kama Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani wamekabidhi baadhi ya majukumu yake kwa hawa watu.
Kama ndivyo,
Je?
Hawa askari wamesomea wapi taratibu hizi.
Mkuu wa jeshi hili ni nani.
Kikosi cha usalama barabarani kinafaidika nini na kikosi hiki?
Je wanazijua sheria za usalama barabarani?

Nasema hivi kwa sababu kuna baadhi ya miji ukitembelea utakuta wamechora michoro barabarani chini (sio vibao vinavyoonyesha parking signs) ambayo haina maelekezo yoyote. Mbaya zaidi michoro hii haizingatii sheria za usalama barabarani. Mfano utakuta mtu amechora kiboksi kwenye kona kabisa na anadai ni parking. Kwa ulewa wangu kupark kwenye kwenye kona ni hatari hasa kwa gari linaloingia barabara nyingine. Pia kuna kiasi cha mita zitakiwazo kuzingatiwa kupark toka kwenye kona.
Ninaposema Jeshi linafaidika ama serikali yetu inafaidika vipi ni kwa sababu hawa jamaa huvizia magari yasiyopark kwenye viboksi walivyochora na kufunga minyoro yao yenye miiba. Pindi mwenye gari atokeapo umtishia na kutaka kuvuta gari. Kwa wenye uelewa mdogo hutishika na kuanza ku-negotiate na hawa jamaa. Faini yao ni shs 50,000 Lakini kama mkielewana utalipa shs 10,000 hadi 20,000. Je jeshi linafahamu haya? na kama wanaelewa wao hupelekewa fungu kiasi gani.
Mimi naona hatari ya kuja kuwepo na mgongano wa maslahi ya jeshi letu na hizi kampuni binafsi.
Nawakilisha
 
Back
Top Bottom