Baa la njaa linakuja

Kifulambute

JF-Expert Member
May 8, 2011
2,539
755
natumaini hamjambo wanajamvi wenzangu.....najua mna habari kwa nini kinaendelea kwa wenzetu Kenya kuhusu balaa la njaa linalowakumba... Juzi nimeshuhudia malori( semi trailers) kama 50 zikiwa na shehena ya mahindi kuelekea mpakani Horiri zikipeleka mahindi kenya, kwa taarifa niliyonayo serikali imepiga marufuku usafirishaji huo haramu lakini cha kushangaza polisi waliopo maeneo hayo wanaruhusu magari yapite kwa kitu kidogo wanachopokea kwa gunia moja ni Tsh 1000. sasa ninavyojua mbeleni hali kama hii ikitokea kwetu Wakenya kamwe hawawezi kuleta chakula kwetu....lazima tufe maana serikali kwa sasa wamejikita kwenye Posho, Symbion a.k.a TANESCO, itakapokuja njaa tutakimbilia kwa nanai? ....tujihadhali watanzania kwa njaa inayokuja
 
Njaa mbona ipo tayari, longido wameomba msaada wa chakula, shinyanga na iringa wako mbiyoni. Nadhani tumuongezee posho Mh.mb wamaswa- shibuda ili aweze kuwagawia wananchi wake.
 
Njaa mbona ipo tayari, longido wameomba msaada wa chakula, shinyanga na iringa wako mbiyoni. Nadhani tumuongezee posho Mh.mb wamaswa- shibuda ili aweze kuwagawia wananchi wake.

Posho inatosha nini badala serikali inunue chakula na kuwapelekea! Watanzania tuna shida sana wanaacha kudiscuss mambo ya maendeleo wanapoteza muda kudiscuss posho? TUMELOGWA
 
Nchi ye2 ndivyo ilivyo Best! Wakisema wanadhibiti boda ya Holili inapita boda ya Namanga na wakisema wanadhibiti sana wanapitisha kwa Toyo ama baiskeli na ingali kuna police kila idara. Yani mi cjawahi ona uongozi mbovu km ya hii chama cha magamba ki2 kidogo wanapewa maaskari wanaruhusu ndg zao wafe kwa njaa na imeshakuwa kawaida yao miaka nenda rudi. (TABIA HAINA DAWA WanaJF)
 
Tabia ya Wakenya wanapenda kuexpose hata mambo madogo na si ajabu ukakuta kweli tuna njaa hapa kwetu sawa na wao lakini hizi sera za"tunashughulikia", "hakuna atakayekufa na njaa", "tuko kwenye mchakato" tunajisahau na kudhani njaa iko Kenya!
Njaa mbona ipo tayari, longido wameomba msaada wa chakula, shinyanga na iringa wako mbiyoni. Nadhani tumuongezee posho Mh.mb wamaswa- shibuda ili aweze kuwagawia wananchi wake.
 
Tabia ya Wakenya wanapenda kuexpose hata mambo madogo na si ajabu ukakuta kweli tuna njaa hapa kwetu sawa na wao lakini hizi sera za"tunashughulikia", "hakuna atakayekufa na njaa", "tuko kwenye mchakato" tunajisahau na kudhani njaa iko Kenya!

Mtu mwingine akiongea wanasema ' anatafuta umaarufu" tumtafuteni alietuloga watanzania kwa nini viongozi wetu hawafikirii positive?
 
Wait for the next generation of leaders, ndo mambo yatabadilika, sio leo...
 
Baa la njaa lipo siku zote, sema labda litaongezeka. Asilimia kubwa ya watanzania hatuli tukashiba na tunachokula sio chakula bora, upo hapo?
 
Mi np kibaigwa mkoani dodoma na hapa ni soko kuu la mahindi na anweza kusema ndio soko kubwa la mahindi hapa dodoma.mwaka jana muda kama huu tulikua tunanunua mahindi kwa sh elfu 25 kwa gunia la debe 7 na gunia la alizert tulinunua kwa elfu 22 ela ya kitanzania,but leo gunia hilo linauzwa kwa sh 48,500/= na alizert kwa sh 45,000/= na kwa sasa ndio kipindi cha mavuno.
Hebu tujiulize ifikapo mwezi wa 12 kipindi cha kilimo hilo gunia litauzwa kwa bei gn!??ni kweli kabisa,njaa inakuja na inatisha wakubwa.
 
nikweli kuna mikoa kuna njaa !!!!!!!!!!! lakini mkulima wa Rukwa hajui mahindi yake atmuuzia nani kwani mpaka sasa serikali hajatoa mahindi katika maghala yake ambayo ni vituo vya ununuzi.

Waachwe wajasiriaa mali wa tz wapelelleke mahindi kenya kwani hio itapandisha bei ya mahindi ambayo itamsaaidia mkulima wa sumbawanga
 
na bado, mpaka mfe nusu ya wananchi ndio next time mtachagua viongozi wanaofaa.ikitokea before 2015 labda watakaobaki watajifunza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom