B.O.T, kuanzisha noti ya sh.20,000, nini madhara yake?

Hii nchi bora iuzwe na wananchi tupewe pesa yetu tukatafute pa kuishi nchi nyingine. Vinginevyo tutakufa kabla ya wakati wetu.
 
kutokana na mfumuko wa bei unaoendelea nchini bila ufumbuzi wa tatizo hili,imepelekea thamani ya fedha za ndani kushuka..ni wazi sasa ukienda na sh.elfu kumi sokoni haitoshi kwa mahitaji ya nyumbani kwa siku.
Ni tofauti na miaka ya nyuma,kwani hadi mwaka 1993 shiling ya Tanzania ilikua na thamani kubwa angalau.
Kutokana na tatizo hili BOT yaweza kuanzisha noti mpya ya sh.elfu ishirini (20,000) kwenye mzunguko ili kupunguza hadha ya kubebelea noti nyingi kununua vitu vichache.
Je nini madhara yake(hasara na faida kama zipo) kiuchumi na kijamii?

Kwa maoni yangu si busara sasa hivi kwa BOT kufikiria kuchapisha noti ya TZS 20,000 kwa sababu mpaka sasa noti iliyo kubwa zaidi ambayo ni TZS 10,000 siyo watanzania wengi wa kawaida ambao at any time utakuta anayo mfukoni. Ni katika miji mikuu tuu ndiyo utakuta watu wengi wana hiyo TZS 10,000 na ukienda vijijini na hiyo hela unaweza kukosa huduma kwa sababu whawana chenji. Kwa sababu hiyo basi bado noti ya TZS 10,000 inafaa iwe nddiyo kubwa kuliko zote pamoja na kwamba hali ya maisha imepanda sana.

Hata hivyo tunahitaji kuhama kutoka katika katika mfumo huu wa kulipia matumizi yetu kwa fedha taslim badala ya kutumia kadi. Mfumo huu wa kulipia kwa kadi kama ukiimarishwa kutakuwa hakuna haja ya kubeba lundo la fedha kwa ajili ya kufanya manunuzi na kutakuwa hakuna haja ya kuchapa fedha nyingine kama unavyopendekeza.
 
mkuu,hali ya mfumuko wa bei huko vijijini ukoje? Wao hawalalamikii hali hii?
 
zimbabwe ile dola yao..ina noti kubwakubwa zaidi ya hii elfu 20..hii ni kutokana na hali ya uchumi wao..kwa mwenendo huu wa kwetu,noti ya elfu 20 haipukiki..
 
ni bora waanzishe tu-maana buku kumi kwa sasa haitoshi kabisa-
hii serikali inapotupeleka tutawazid zimbabwe-
 
Back
Top Bottom