Aziz P. Mlima.. Almost ambassador?

sidhani kama hii peke yake inatosha kuwa sababu; maana tukifuata yanayofanywa na nchi nyingine "zinazokwenda na wakati" tunaweza kufuata mambo mengi kweli. Kuna mambo ambayo sisi wenyewe ni lazima tuyafikiri na kuyaamua kwa nia yetu sisi wenyewe.

Lakini kwenye suala la UN2 hatuwezi tu kutoka na kusema every one go!! hakuna sehemu duniani ambao wamefanya hivyo, kila watu wana utaratibu wao na sababu zao. Sisi wa kwetu uweje? hilo ndilo swali au hutaki hata tufikirie tufanye vipi turuhusu tu alimradi tumeruhusu bila kufikilia masuala mbalimbali?

Naam hatuwezi kabisa kufuata kila jambo linalofanywa na nchi nyingine hapa duniani, lakini yale ambayo yana faida kwa nchi kama hili la uDC halina ubaya wowote na sijasikia nchi yoyote ili iwe Afrika, Asia, America na kwingineko ambayo inalalamika kwamba uDC umekuwa na negative impact kwenye nchi hiyo na hivyo kuamua kuachana nao.
 
- Wewe bwana Tanzania sio mchezo watapeli wapo kila kona hata huko kwenye siasa za juu, huyu jamaa ameingizwa mjini tu kuna waliomlia pesa zake wakamuahidi ubalozi huku wakijua kwamba hawezi upata, sasa wamemuambia mbona hukusema mapema kua una uraia wa huko unaona sasa umejiharibia mwenyewe,

- I mean ili uwe balozi hata upendekezwe tu lazima jina lipitie Foreign kwanza wataalamu walipitie na kutoa ushauri wao kwa Rais, anytime ukiona balozi wetu anakataliwa na nchi haina maana kwamba system nzima ilikuwa haijui no way! kuna somebody alijua na alimfahamisha Rais mapema na ndio kazi hasa na Zahra-Nuru, lakini kwa sababu za utapeli jina lako linapelekwa anyways, limekatalia umetiwa ndani hela zako, case closed!

- Iwe fundisho tu kwa wengine kwamba utapeli upo mpaka huko juu!

Respect.

FMEs!
 
sidhani kama hii peke yake inatosha kuwa sababu; maana tukifuata yanayofanywa na nchi nyingine "zinazokwenda na wakati" tunaweza kufuata mambo mengi kweli. Kuna mambo ambayo sisi wenyewe ni lazima tuyafikiri na kuyaamua kwa nia yetu sisi wenyewe.

Lakini kwenye suala la UN2 hatuwezi tu kutoka na kusema every one go!! hakuna sehemu duniani ambao wamefanya hivyo, kila watu wana utaratibu wao na sababu zao. Sisi wa kwetu uweje? hilo ndilo swali au hutaki hata tufikirie tufanye vipi turuhusu tu alimradi tumeruhusu bila kufikilia masuala mbalimbali?

sera zimepitwa na wakati, huo ulikuwa tu uoga wa mwl, wapeni watu haki yao uraia wachukue raia.

asilimia 99.999999% walioamuwa kuchukuwa uraia ni masikini kwa hiyo walifanya hivyo si kwa mapenzi bali ni lazima iwe hivyo.
 
- Binafsi siungi mkono wananchi wetu kua na uraia wa nchi mbili, no way! haijawahi kuwa dhana ya maendeleo kwa nchi yoyote iliyongia huu mchezo, Eritrea ndio walioingia hivi karibuni eti sasa hivi wameendelea kuliko walivyokuwa kabla?

- Tanzania tuna a lot ya ku-deal with haya sio yetu! wala hayatuhusu!

Respect.

FMEs!
 
Nyie mnashangaa hili

Mbona tuna waziri wa Fedha ambaye ana degree feki?

sasa ipi sensitive btn the two?
 
Nyie mnashangaa hili

Mbona tuna waziri wa Fedha ambaye ana degree feki?

sasa ipi sensitive btn the two?

Wala sio mmoja tu. Tunao wengi tu. Na wabunge ndio usiseme kabisa. Na huko kwenye taasisi zingine ndio wamejaa kibao. Ukweli ni kwamba hakuna cha kushangaza hapa.
 
Quote>Bubu Ataka Kusema;Hatufuati nchi yoyote ile Mkuu Mkjj bali ni kwenda na wakati. Nchi nyingi sana zinaona faida kubwa ya kuwashirikisha katika ujenzi wa nchi zao raia wanaoishi nchi za nje ambao tayari wana uraia wa nchi nyingine, hivyo sioni sababu zozote zile za Tanzania kusubiri kuwa nchi ya mwisho katika Afrika kufanya hivyo. Wenzetu wa Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi etc wameshafanya hivyo sijui sisi tunangoja nini![/COLOR][/I]

Duh! Bubu nchi ulizozitaja walikua na sababu zao za kuruhusu. TZ kwa sasa hatuna sababu izo.Nchi aiendeshwi kwa kufanya kila jambo linalofanywa na jirani.Nina wasiwasi utakuja sema Rwanda, Burundi, Uganda walishapigana wao kwa wao sijui TZ tunangoja nini!
 
Taifa sio lazima liwe na sababu ya kupitisha sheria hiyo kwani wakipitisha sheria hiyo hatutakuwa na huo uraia wa nchi mbili au zaidi ya mbili automatically.. Mwenye sababu atakuwa ni mtu mwenyewe binafsi atakayeamua kufanya hivyo. Taifa linachotakiwa kufanya ni kutokumnyima kabisa raia wake fursa ya kufanya hivyo pale atakapo. Ila fursa hiyo lazima itolewe kwa kufuata sheria zitakazolinda maslahi ya taifa. Ubaya uko wapi hapo?

So I guess unaweza ukasema sababu ya taifa kufanya hivyo ni kuwapa fursa raia wake watakaopenda kufanya hivyo.
 
Membe atakuwa London kwenye mkutano wa diaspora wiki chahce zijazo.Nadhani itakuwa fursa nzuri akiulizwa kuhusu huo mchakato usio na mwisho about dual citizenship.
Anakuja lini, tarehe kama unafahamu?
 
Sawa lakini hao si "Halali" Kisheria,si raia wa Tanzania.

Sheria ipi ambayo wewe unasema? Mbona wanaingia Tanzania na kutoka bila kuchukuliwa hatua kama watanzania? Hizi sheria ambazo hazifanyi kazi ndio unazipigia debe? Sheria ambayo haifanyi kazi ina maana gani?
 
Ni kwa sababu ya Tanzania kutokua na data base ya wananchi wake! Najua hili si tatizo la Tanzania peke yake, lipo na nchi zingine, lakini haina maana kuwa ni sawa.

Serikali ingeweza kuanza tu kwa kuingiza kwenye data base wananchi wote wenye hati za kusafiria na hiyo data base iwe updated mara kwa mara (si kama website zao!)

Basi tunaonekana wajiiinga! Aibu!

Nchi nyingine wana data base za raia wao kwa njia nyingine. Ingekuwa vizuri utaje nchi ambazo hazina vitambulisho kama sisi ili tuweze ku-compare notes.
 
Marehemu Barbara Johansson aliwahi kuwa balozi wetu Sweden/Mbunge wa kuteuliwa wakati akiwa Mswidi/Mtanzania

Huyo mama alikuwa lini balozi wetu Stockholm? Hii hapa orodha ya waliowahi kuwa mabalozi Stockholm. Tuoneane huruma wakati mwingine.

Amandla.........

  • Vacant Oct. 2008- Todate

  • H.E. Dr. Ben Moses2005-2008

  • H.E. James L. Kateka 1998-2005

  • H.E. Wilson K. Tibaijuka 1994-1998

  • H.E. Mohamed Ramia Abdiwawa 1990-1994

  • H.E. Daniel N. Mloka1983-1989

  • H.E. J.F. Edward Mhina 1977-1983

  • H.E. Chief Michael Lukumbuzya 1969-1977

  • H.E. Philemon Muro 1964-1969
 
Labda anaitwa Vacant ........................tehe tehe tehe! kuna watu hawatofautishi maofisa ubalozi na balozi!
 
Julius.. usielewe vibaya mkuu. Binafsi sina tatizo kabisa na kuruhusu Watanzania kuweza kuwa na uraia wa zaidi ya nchi moja (sielewi kwanini lazima uwe wa nchi mbili tu!) lakini kama unavyosema lazima tuweke wazi exceptions kwa sababu.. nakumbuka Fujimori kilipomuungulia kule Peru akakimbia nchi ya asili ya wazazi wake (Japani!) akidai uraia wa kule.

Hili la Fujimori ni tofauti kidogo. Sidhani kama alikuwa na uraia wa nchi mbili alipokuwa rais wa Peru. Nchi nyingi tu zinatumia utaratibu wa uraia wa jus sanguinis, yaani mtu yeyote ambaye ana damu ya nchi hiyo ana haki ya kuishi nchini humo na akifuata utaratibu kupata uraia baadaye. Nchi hizi ni kama Ujerumani, Ugiriki, Japan, Estonia, Rwanda n.k. Baadhi ya nchi hizi (Rwanda n.k.) zinatoa uraia kwa yeyote yule atakayerudi. nyumbani. Fujimori kutokana na uzawa wake alikuwa na haki ya kuishi Japan na angetaka baadae kuchukua uraia. Kwa hali hiyo la Fujimori si suala la double citizenship bali mfumo wa uraia huko walikotoka wazazi wetu. Kwetu sisi, tukitaka kuzuia hiyo ni pengine kupitisha sheria kuwa mtu yeyote ambaye ana damu ya Rwanda asiwe na haki ya kutumikia nchi yake katika sehemu kadhaa! Hata kama ni babu zake ndiyo waliotoka Rwanda. Huu utakuwa ni ubaguzi wa hali ya juu.

Amandla........
 
Mcheza tennis, Mary Pierce alizaliwa Canada lakini alikuwa na uraia wa ufaransa, Canada na USA. Yeye aliamua kuwakilisha ufaransa katika michezo ya kimataifa. Hakuna aliyeona tatizo kwenye hilo.

Amandla.......
 
Sheria ipi ambayo wewe unasema? Mbona wanaingia Tanzania na kutoka bila kuchukuliwa hatua kama watanzania? Hizi sheria ambazo hazifanyi kazi ndio unazipigia debe? Sheria ambayo haifanyi kazi ina maana gani?

Sawa mkuu lakini kuwepo kwa sheria haina maana kwamba hazivunjwi.

Jasusi;Niliweka msisitizo kwenye pointi yangu kwasababu issue hiyo imemgusa "Mtanzania" asiye "Halali" kuliwakilisha Taifa ama serikali halali,hivyo pointi yangu haikuwa hao wabongo wengi.
 
Kuna watu wanatunukiwa ubalozi wa heshima na ma consulars .na wanaiwakilisha nchi vizuri husika kuliko sisi tunaojiita mabalozi raia bila kuwa wazelendo.

Lile sakata la ile Jengo la ubalozi wa Italy la Prof Mahalu mtibuaji wa dili nasikia ni mtaliano. sasa hapo nani alikuwa balozi Tanzania inayemuhitaji? Mahalu au Huyo mtaliano.
 
Wala sio mmoja tu. Tunao wengi tu. Na wabunge ndio usiseme kabisa. Na huko kwenye taasisi zingine ndio wamejaa kibao. Ukweli ni kwamba hakuna cha kushangaza hapa.

Na hili la kuficha ficha mambo ndiyo linaongeza rushwa. Baadhi ya Wabongo walioamua kurudi ili kufungua mabiashara (ambayo yanaruhusiwa kwa Watanzania tu) wanarudi kinyemela na wakati mwingi husaidiwa na hao hao watunza sheria za nchi ili waingie nchini kama Watanzania badala ya wageni kwa kuwa wamechukua uraia wa nchi nyingine.
 
Naamini wote (kwa kiasi kikubwa) tunakubaliana kuwa kuruhusu wananchi kuwa na uwezekano wa uraia zaidi ya mmoja siyo jambo baya kwa kipimo chochote. Naamini mgogoro unakuja kwenye kanuni za kuruhusu jambo hilo. Kusema tu kuwa kutakufa na faida za kiuchumi kama wengi wanavyojenga hoja sidhani kama inatosha.
 
Mkjj kwa maoni yangu sioni kasoro zozote hasa ukitilia maanani kwamba Tanzania inafikiria kwanza kuwapa uDC Watanzania ambao ni wazawa wa Tanzania kabla ya kuruhusu kwa wale ambao si wazawa wa Tanzania. Kama unaona faida za kiuchumi hazitoshi basi tuwekee mapungufu ambayo wewe unayaona.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom