balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 14,437
- 12,558
Shusheni nondo jamani, historia yetu ingekuwaje leo bila tukio hili?
Bali...Shusheni nondo jamani, historia yetu ingekuwaje leo bila tukio hili?
Shusheni nondo jamani, historia yetu ingekuwaje leo bila tukio hili?
Baliba...Ilikuwaje TANU ikabadili msimamo wake ndani ya kipindi kifupi?
Asante Kwa historia nzuriBaliba...
Ingia hapo chini kupata kisa kizima cha Kura Tatu:
Mohamed Said: UCHAGUZI WA KWANZA TANGANYIKA ''UCHAGUZI WA KURA TATU'' 1958 KUTOKA KUMBUKUMBU ZAKE SHEIKH SEMBE
Tewe,Asante Kwa historia nzuri
Shekhe Said huwa nafarijika sana na rejea zako. Je umeshapata kusoma azimio la Tabora lililohuishwa na ACT wazalend? Ningelifurahi kusikia maoni yako juu ya hilo.Tewe,
Historia hii nzuri na mashujaa wake walioiwezesha TANU kuruka kizingiti
kile kigumu yeye Nyerere Mwalimu hakupata kuieleza popote.
Historia hii kama si kitabu cha Abdul Sykes ingelipotea na isingejulikana:
''Kufichuka kwa msimamo wa Mwalimu Nyerere wa kutaka TANU iingie katika Kura Tatu kulishtua uongozi wa Tanga. Majadiliano makali yalifuata uongozi wa Tanga ukionyesha upinzani wao kwa msimamo wa Mwalimu Nyerere. Baada ya majadiliano ya muda mrefu Mwalimu Nyerere alifanikiwa kuwashawishi wote wawili Hamisi Heri na Mwalimu Kihere ambao ndiyo walikuwa wapinzani wakubwa wa msimamo wa Mwalimu Nyerere na uchaguzi wa Kura Tatu. Mwalimu Nyerere aliutahadharisha uongozi wa Tanga kuwa agenda ya Kura Tatu itakapokuja anatabiri kupata upinzani mkali kutoka katika majimbo. Huko Tanga kwenyewe, TANU ilikuwa ikikabiliwa na upinzani mkali kutoka UTP iliyokuwa na nguvu Tanga kwa sababu ya walowezi waliokuwa wakimiliki mashamba ya mkonge katika jimbo hilo. Kwa ajili hii akina Rashid Sembe walikuwa wameelemewa na mashambulizi kutoka kwa wapinzani.
Maili tatu kutoka Tanga kipo kijiji cha Mnyanjani ambako kulikuwako na tawi la TANU lillilokuwa na nguvu sana likiongozwa na Mmaka Omar kama mwenyekiti na Akida Boramimi bin Dai akiwa katibu. Hawa wote ni marehemu na mchango wao hadi leo haujathaminiwa. Mwalimu Nyerere na Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani ili ifanyike tawaswil. Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimimi bin Dai na Mmaka Omari. Aliyechaguliwa kusoma Qur'an Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora.''
Mcubic,Shekhe Said huwa nafarijika sana na rejea zako. Je umeshapata kusoma azimio la Tabora lililohuishwa na ACT wazalend? Ningelifurahi kusikia maoni yako juu ya hilo.
Hakika historia nzuri ilifichika. Naomba unisaidie zaidi undani/maana ya kura tatuTewe,
Historia hii nzuri na mashujaa wake walioiwezesha TANU kuruka kizingiti
kile kigumu yeye Nyerere Mwalimu hakupata kuieleza popote.
Historia hii kama si kitabu cha Abdul Sykes ingelipotea na isingejulikana:
''Kufichuka kwa msimamo wa Mwalimu Nyerere wa kutaka TANU iingie katika Kura Tatu kulishtua uongozi wa Tanga. Majadiliano makali yalifuata uongozi wa Tanga ukionyesha upinzani wao kwa msimamo wa Mwalimu Nyerere. Baada ya majadiliano ya muda mrefu Mwalimu Nyerere alifanikiwa kuwashawishi wote wawili Hamisi Heri na Mwalimu Kihere ambao ndiyo walikuwa wapinzani wakubwa wa msimamo wa Mwalimu Nyerere na uchaguzi wa Kura Tatu. Mwalimu Nyerere aliutahadharisha uongozi wa Tanga kuwa agenda ya Kura Tatu itakapokuja anatabiri kupata upinzani mkali kutoka katika majimbo. Huko Tanga kwenyewe, TANU ilikuwa ikikabiliwa na upinzani mkali kutoka UTP iliyokuwa na nguvu Tanga kwa sababu ya walowezi waliokuwa wakimiliki mashamba ya mkonge katika jimbo hilo. Kwa ajili hii akina Rashid Sembe walikuwa wameelemewa na mashambulizi kutoka kwa wapinzani.
Maili tatu kutoka Tanga kipo kijiji cha Mnyanjani ambako kulikuwako na tawi la TANU lillilokuwa na nguvu sana likiongozwa na Mmaka Omar kama mwenyekiti na Akida Boramimi bin Dai akiwa katibu. Hawa wote ni marehemu na mchango wao hadi leo haujathaminiwa. Mwalimu Nyerere na Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani ili ifanyike tawaswil. Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimimi bin Dai na Mmaka Omari. Aliyechaguliwa kusoma Qur'an Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora.''
Suala si kwamba hawakupitia shule za mission bali hawakuwa wamesoma. Ni vizuri kuweka hiztoria sahihi. Mfano mimi Babu yangu ) mzaa mama ) ndio walikuwa wanaharakati wa kudai uhuru bahati mbaya hakuwa amesoma sana ( alisoma hizohizo shule za mission bali si kwa kiwango kikubwa), hakuweza kupewa madaraka makubwa kwa sababu elimu yake ilikuwa ndogo. Hata hivyo alikuwa akiheshimika kama muasisi wa kudai uhuru wa nchi hii. Na utambue kuwa wazee hawa walichofurahia ni kupata uhuru na walikuwa wanapewa hadhi kutokana na role yao waliyoifanya. On the other side babu yangu ( mjomba wake mama yangu) yeye alikiwa muasisi wa kupigania uhuru alipata wadhifa katika srekali kwani alikuwa msomi na alikuwa vna vigezo vya kuwaza kuongoza, hivyo ni vyema kuweka historia sahihi.Ni kutokana na uamuzi huo Chama kikatafuta watu wenye vigezo ambavyo kwakweli viliwabagua wazee waasisi wa Chama, wasomi ndyo walikuwa na nafasi hiyo, waasisi wazee wa kiislamu hwakuwa wamepita shule za mission hapo ndo wasomi wa makerere wakristo walipopewa nafasi ya kugombea ujumbe wa LEGCO ambayo TANU ilishinda karibia viti vote.
Ninachoweza kusema mkuu Mwana ni kwamba kiongozi siyo lazima awe amesoma elimu ya kizungu bali kiongozi lazima awe na kipaji cha uongozi tuu,inatosha.Tunachokiona hapa mkoloni alihitaji uongozi uende kwa tabaka la vibaraka wake aliodhanivni wasomi wa shule za mission kwa minajiri ya kuwatumia baadae kupitia ukoloni mambo leo.unaweza vipi kusema mashehe na maimamu hawakuwa wamesoma? Leo hii mbona viongoz wengi tuu ni darasa la saba na chini ya hapo? Katika uchaguzi huo wa kura tatu1958,mkoloni alishaanza kujenga mfumo mpya wa unyonyaji na ukandamizaji ndiyo maana akaweka vigezo baguzi na kandamizi.Suala si kwamba hawakupitia shule za mission bali hawakuwa wamesoma. Ni vizuri kuweka hiztoria sahihi. Mfano mimi Babu yangu ) mzaa mama ) ndio walikuwa wanaharakati wa kudai uhuru bahati mbaya hakuwa amesoma sana ( alisoma hizohizo shule za mission bali si kwa kiwango kikubwa), hakuweza kupewa madaraka makubwa kwa sababu elimu yake ilikuwa ndogo. Hata hivyo alikuwa akiheshimika kama muasisi wa kudai uhuru wa nchi hii. Na utambue kuwa wazee hawa walichofurahia ni kupata uhuru na walikuwa wanapewa hadhi kutokana na role yao waliyoifanya. On the other side babu yangu ( mjomba wake mama yangu) yeye alikiwa muasisi wa kupigania uhuru alipata wadhifa katika srekali kwani alikuwa msomi na alikuwa vna vigezo vya kuwaza kuongoza, hivyo ni vyema kuweka historia sahihi.