MNYISANZU
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 7,048
- 1,102
Hakuna kipindi kama hiki ktk historia ya Tanzania ambapo "AZIMIO LA ARUSHA" lilikuwa linahitajika sana!. Kwa sasa Azimio la Arusha lilikuwa linahitajika katika kutumika kama mwarobaini wa kudhibiti ufisadi uliotamalaki kila mahali [ rejea nyongeza ya posho za wabunge, mishahara na posho wanazolipana maofisa wa ngazi za juu BOT, TRA,NSSF na mashirika/taasisi zingine za umma]. Kushuka kwa uwajibikaji miongoni mwa viongozi na watumishi wa ngazi za juu, kupuuzwa kwa professions zingine kama madaktari,walimu,polisi,etc ni kielelezo kingine kinachoonyesha kuwa Azimio la Arusha lilkuwa bado relevant na linahitajika. Kila siku huwa najiuliza ni akina nani haswa walioliuwa hili Azimio? na kwanini hawakulifanyia marekebisho tu pale panapohitajika kufanya hivyo? . Mwisho kabisa walaaniwe wale wote ambao kwa namna moja au nyingine walishiriki kuliua hili Azimio.