Azikwa akiwa hai Mbeya

inatisha,hivi mtu unahakikishaje kuwa fulani ni mchawi kiasi cha kuamua kumuua?mi nahisi wengi wanauliwa bila hatia.

kwa hakika hiyo ni kweli. k
Kama vile wanaouawa mitaani kwa kushukiwa kuwa wezi - wengine huwa hawana hatia lakini wanatiwa kiberiti.
 
kuna watu wataalamu wakuona hao wachawi, wanaitwa lifumu

kwa hiyo lifumu akisema Ukweli mtupu ni mchawi basi lazima tumuamini tu,sijui lifumu ni nani ila nahisi ndo kama wale tu waliokua wakisema mtoto sijui akizaliwa katanguliza miguu au mtoto akianza kuota meno upande fulani eti hafai auliwe.Sina imani na lifumu,watu wa aina hii ndo wanaosababisha mauaji ya kinyamba kinyama tu serikali inatakiwa kuwadhibiti.
 
Last edited by a moderator:
Embu fafanua ilikuwaje kisa hicho? Na nani wanyama hao? Kuna uhusiano na mambo ya kishirikina?
 
kwa hiyo lifumu akisema Ukweli mtupu ni mchawi basi lazima tumuamini tu,sijui lifumu ni nani ila nahisi ndo kama wale tu waliokua wakisema mtoto sijui akizaliwa katanguliza miguu au mtoto akianza kuota meno upande fulani eti hafai auliwe.Sina imani na lifumu,watu wa aina hii ndo wanaosababisha mauaji ya kinyamba kinyama tu serikali inatakiwa kuwadhibiti.

mkuu shakupata vizuri,. Ila hujaishi mbeya hata mie naogopa kwenda mbeya mwaka wa2 make huwezi fanya vitu vya maendeleo hata kujenga nyumba sababu ya wachawi kuogopa,. Wache wanambeya wafanye mambo yao kwa maendeleo yao
 
Last edited by a moderator:
Watanzania kama tuna hasira hivyo kwanini tusiwashugulikie mafisadi? wanaojilimbikizia mali huku mamilioni ya watu wanataabika na umaskini.
 
mnaounga mkono mnakosea jamani tukumbuke sisi sote binadamu ni wakosaji hakuna aliyemsafi, uchawi upo na kweli umekuwa ni kero Mbeya na hasa hii ni kutokana na kupakana na wazambia. nimeishi kule jamaa ni wachawi sana na haya ya kuchunana ngozi na mengineyo yanayotokea mbeya yanakuwa adopted kutoka huko. kikubwa huyo adhabu yake angeambiwa kwanza amrudishe mtoto na pili apewe adhabu tofauti na hiyo kama ni kweli. tusitafune maneno na kujifanya hatujui uwepo wa uchawi.
 
jamani kila mwanadamu ni mkosaji hivyo kabla ya kumuhukumu mwenzio jiangalie wewe kwanza. mi cku hizi naogopa kumuhukumu mwenzangu maana mi mwenyeme nna midhambi yangu kibao.
 



amka2.gif

UKISTAAJABU ya Mussa utayaona ya Firauni, ndivyo unavyoweza kusema baada ya wakazi wa Kitongoji cha Itezi Magharibi, Kata ya Itezi, jijini Mbeya, kuamua kumzika mwenzao akiwa hai.
Wananchi hao wanaodaiwa kuwa na hasira kali walifikia hatua hiyo ya kutisha, kuhuzunisha na kusikitisha kwa mkazi mwenzao, Nyerere Kombwee, wakimtuhumu kuwa ni mchawi, wakimhusisha na kifo cha mtoto wa mdogo wake aliyejulikana kwa jina la Leonard Kombwee.
Tukio hilo lilitokea jana katika kitongoji hicho, ambapo wananchi hao walimkamata Kombwee na kumpeleka mahali walipolichimba kaburi la kumzikia mtoto wa mdogo wake, ambalo lilikuwa na urefu wa futi tatu huku wakimlazimisha aingie ndani.
Kombwee alipoingia ndani ya kaburi hilo wananchi hao walitumia fursa hiyo kumtupia jiwe kichwani na kumfukia akiwa hai.
Awali kabla ya wananchi hao kufikia hatua hiyo, wakiwa katika shughuli za kuchimba kaburi hilo kwa ajili ya kumzika mtoto wa mdogo wake, walianza kujadili sababu ya Nyerere kutokuwapo kwenye msiba huo.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu walifikia makubaliano ya kuteua baadhi ya watu kwenda kumfuata ambapo walipofika nyumbani kwake hawakumkuta lakini waliamua kuwapiga mama na dada wa Nyerere ili wataje alipo wanayemhitaji.
Mama na dada wa Nyerere walipoona kipigo kimewazidi walilalizimika kutaja alipo Nyerere, ambapo alikamatwa na wananchi hao kisha kumpiga huku wakienda naye lilipokuwa likichimbwa kaburi la mtoto wa mdogo wake.
Maziko ya kumzika aliye hai
Wananchi hao walipomfikisha mtuhumiwa wao kwa wenzao majira ya saa tatu asubuhi, walimlazimisha Nyerere kuingia kaburini na alipoingia walimsindikiza kwa kipigo cha jiwe na baadaye walimfukia.
Mmoja wa watu waliokuwa makaburini hapo inadaiwa kuwa alimkandamiza kwa chepeo, hali iliyosababisha kushindwa kujinasua na kufukiwa kirahisi akiwa mzima.
“Baada ya kuona mchanga unazidi kujaa huku akiwa amekandamizwa na chepeo marehemu aligeuka na kulala kifudifudi hadi mchanga ukajaa kaburi,” alieleza mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.
Baada ya tukio hilo baadhi ya watu waliokuwapo makaburini waliamua kutawanyika kwenye eneo hilo huku wengine wakitoa taarifa za tukio hilo polisi.
Polisi walipofika eneo hilo majira ya saa nane mchana wakiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili DFP 474, walilazimika kufyatua risasi za moto na mabomu ya machozi ili kuwatawanya waliokuwapo na baadaye kufukua kaburi hilo ambapo walimkuta Nyerere amekwisha kufariki dunia.
Kisa chaelezwa
Baadhi ya majirani wa familia hiyo walidai kuwa tukio hilo limesababishwa na ugomvi wa kifamilia ambao umedumu kwa muda mrefu, ambapo inadaiwa marehemu Nyerere alikuwa akituhumiwa kumuua mtoto huyo wa mdogo wake na ndipo wananchi wakaamua kulipa kisasi.
Walidai kuwa baada ya mtoto wa Leonard kufariki dunia Aprili 27 mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha majira ya saa tatu asubuhi, walimshuku Nyerere kwakuwa hakwenda kwenye msiba.
Walidai kuwa hata hivyo Nyerere alizikwa hai kwa sababu alitoa vitisho kwa wananchi waliompeleka makaburini kuwa kipigo walimchompatia na kusababisha atoke damu hakitakwenda bure ni lazima atakilipa.
Naye Naibu Meya wa Jiji la Mbeya, Frank Maemba, aliyekuwepo makaburini kusimamia hali ya amani wakati wa ufukuaji wa mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu alisema tukio hilo ni la kikatili na lisilopaswa kuvumiliwa.
Maemba alisema wananchi wote walioanzisha uamuzi wa kuwashawishi wenzao kujichukulia sheria mkononi watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.


source: Tanzania Daima- Jumapili



Hili ni tukio liomefanywa na binadamu kweli au unatuletea habari za kututania hapa? Jamani mbeya watu wa Mungu hawa wanakuwaje siku hizi madhehebu yote hayo?
 
Nadhani muda muafaka wa serikali kuunda sheria ya uchawi maana kuendelea kukataa kuwa serikali haitambui uchawi ni uongo na wengi watakufa na wengine huenda ni muhimu katika jamii yao na wanaleta manufaa katika jamii zao
Nashauri wasajiliwe kuliko kukana kuwa haupo hali wanasiasa wanaenda kupata huduma za kiutawala na maamuzi katika mikutano iliyo ya siri mbon mambo ya Freemanson yapo wazi na anayetaka kujiunga anaruhusiwa?
Nashauri pia waelimishwe kuutumia kwa manufaa bora wazungu tunatumia sayansi yao kwanini ya kwetu isitambuliwe
Nafikiri watu washauriwe na wajitokeze kila mmoja na nguvu zake na aambiwe yeye anaweza kufanyia nini nchi hii ikapata
faida na uchawi wake badala ya kinachoendelea cha kuwaua kikatili
Na watu wa haki za binadamu wako wapi? maana mtu anaonesha ujuzi wake hawamtetei na kumtangaza!
Pawepo utaratibu na si ajabu kwani hamsoni habari za Firauni?Farao na Mtume Musa? Mbona hapakuwepo na madhara baada ya wao kuwa wanajumuishwa katika utawala
Wengine wanauwezo wa kuzuia mvua/kuleta mvua na kuleta ndege (Queleaquelea), kuleta maradhi, kuua na kufufua kwa mazingaumbwe/ kuondoa mguu na kuuficha,kuuondoa uume na kuuficha, kuzuia uzazi mwanamke asizae, kuharibu nyumba kwa upepo, kuchukua mazao ya wenzake nk
Huenda tungepunguza matumizi ya dawa za uzazi za mpango, gharama za mvua kama za Lowasa, kupunguza gharama za kuua ndege, maradhi, gharama za opereshaji ya uzazi na
 
Wewe ni NANI na hata uamue kumuua binadamu mwenzako HATA KAMA KAKOSEA, hata kama ni mchawi, mwizi, fisadi nk. Watu wanaodiriki kuua au kutamani binadamu mwenzake afe ni hatari sana kwa Tz yetu. RIP Nyerere!
 
Back
Top Bottom