Azikwa akiwa hai Mbeya

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213




amka2.gif
UKISTAAJABU ya Mussa utayaona ya Firauni, ndivyo unavyoweza kusema baada ya wakazi wa Kitongoji cha Itezi Magharibi, Kata ya Itezi, jijini Mbeya, kuamua kumzika mwenzao akiwa hai.
Wananchi hao wanaodaiwa kuwa na hasira kali walifikia hatua hiyo ya kutisha, kuhuzunisha na kusikitisha kwa mkazi mwenzao, Nyerere Kombwee, wakimtuhumu kuwa ni mchawi, wakimhusisha na kifo cha mtoto wa mdogo wake aliyejulikana kwa jina la Leonard Kombwee.
Tukio hilo lilitokea jana katika kitongoji hicho, ambapo wananchi hao walimkamata Kombwee na kumpeleka mahali walipolichimba kaburi la kumzikia mtoto wa mdogo wake, ambalo lilikuwa na urefu wa futi tatu huku wakimlazimisha aingie ndani.
Kombwee alipoingia ndani ya kaburi hilo wananchi hao walitumia fursa hiyo kumtupia jiwe kichwani na kumfukia akiwa hai.
Awali kabla ya wananchi hao kufikia hatua hiyo, wakiwa katika shughuli za kuchimba kaburi hilo kwa ajili ya kumzika mtoto wa mdogo wake, walianza kujadili sababu ya Nyerere kutokuwapo kwenye msiba huo.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu walifikia makubaliano ya kuteua baadhi ya watu kwenda kumfuata ambapo walipofika nyumbani kwake hawakumkuta lakini waliamua kuwapiga mama na dada wa Nyerere ili wataje alipo wanayemhitaji.
Mama na dada wa Nyerere walipoona kipigo kimewazidi walilalizimika kutaja alipo Nyerere, ambapo alikamatwa na wananchi hao kisha kumpiga huku wakienda naye lilipokuwa likichimbwa kaburi la mtoto wa mdogo wake.
Maziko ya kumzika aliye hai
Wananchi hao walipomfikisha mtuhumiwa wao kwa wenzao majira ya saa tatu asubuhi, walimlazimisha Nyerere kuingia kaburini na alipoingia walimsindikiza kwa kipigo cha jiwe na baadaye walimfukia.
Mmoja wa watu waliokuwa makaburini hapo inadaiwa kuwa alimkandamiza kwa chepeo, hali iliyosababisha kushindwa kujinasua na kufukiwa kirahisi akiwa mzima.
"Baada ya kuona mchanga unazidi kujaa huku akiwa amekandamizwa na chepeo marehemu aligeuka na kulala kifudifudi hadi mchanga ukajaa kaburi," alieleza mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.
Baada ya tukio hilo baadhi ya watu waliokuwapo makaburini waliamua kutawanyika kwenye eneo hilo huku wengine wakitoa taarifa za tukio hilo polisi.
Polisi walipofika eneo hilo majira ya saa nane mchana wakiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili DFP 474, walilazimika kufyatua risasi za moto na mabomu ya machozi ili kuwatawanya waliokuwapo na baadaye kufukua kaburi hilo ambapo walimkuta Nyerere amekwisha kufariki dunia.
Kisa chaelezwa
Baadhi ya majirani wa familia hiyo walidai kuwa tukio hilo limesababishwa na ugomvi wa kifamilia ambao umedumu kwa muda mrefu, ambapo inadaiwa marehemu Nyerere alikuwa akituhumiwa kumuua mtoto huyo wa mdogo wake na ndipo wananchi wakaamua kulipa kisasi.
Walidai kuwa baada ya mtoto wa Leonard kufariki dunia Aprili 27 mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha majira ya saa tatu asubuhi, walimshuku Nyerere kwakuwa hakwenda kwenye msiba.
Walidai kuwa hata hivyo Nyerere alizikwa hai kwa sababu alitoa vitisho kwa wananchi waliompeleka makaburini kuwa kipigo walimchompatia na kusababisha atoke damu hakitakwenda bure ni lazima atakilipa.
Naye Naibu Meya wa Jiji la Mbeya, Frank Maemba, aliyekuwepo makaburini kusimamia hali ya amani wakati wa ufukuaji wa mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu alisema tukio hilo ni la kikatili na lisilopaswa kuvumiliwa.
Maemba alisema wananchi wote walioanzisha uamuzi wa kuwashawishi wenzao kujichukulia sheria mkononi watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.


source: Tanzania Daima- Jumapili


 
nawashangaa sana hawa viongozi wanaochezea wananchi,kuna watanzania wakatili sana na wakiamua kuharibu basi hakutakalika hapa!
RIP nyerere
 
Huwaga imani za kishirikina zinarudisha nyuma sn maendeleo mbeya,. Waache vijana wajichukulie sheria labda ndo watapungua ili tuijenge mbeya yetu,. Mungu ibariki mbeya
 
Mbeya haiishi vituko kila kukicha, ee Mungu inusuru mbeya na mambo kama haya
 
Inasikitisha enzi hizi za www bado watu wanashabikia ushirikina kiasi cha kuuana!
 
tukio limetokea asubuhi polisi wanafika saa 8 hii inaonesha jinsi gani ambavyo vyombo vya usalama havitekelezi wajibu wake.
Haya mambo haya ni hatari sana kwa mustakabari wa taifa letu.
U will get what you deserve poor mr the late nyerere
 
inatisha,hivi mtu unahakikishaje kuwa fulani ni mchawi kiasi cha kuamua kumuua?mi nahisi wengi wanauliwa bila hatia.
 
Back
Top Bottom