Je, Dawa za Minyoo zinatoa mimba?

Status
Not open for further replies.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,462
154,344
Wandugu wapendwa,

Poleni sana na kazi za ujenzi wa taifa na kujitafutia mkate wa kila siku.

Ninaishi na girl friend wangu ambaye siku ni mfanyakazi wa kampuni moja ya bima hapa DSM.

Wiki iliyopita aliniambia kuwa amepata ujauzito na anahisi una umri wa mwezi mmoja.

binafsi nilifurahishwa sana na taarifa hizo kwani sasa ka umri kamekimbia na sina hata mtoto wa kusingiziwa. Lakini mwenzangu hakuwa anaonekana amefurahishwa na jambo hilo la ujauzito wake na akanishauri kuwa atoe, nikagoma.

Leo ameamka mapema sana na ameniaga kuwa anaenda kununua dawa za minyoo zinazoitwa Zentel.

Je hizo dawa haziwezi kuharibu ujauzito wake?

NA NI NINI MADHARA YA DAWA HIZO KWA MTU MWENYE UJAUZITO MCHANGA KAMA HUO WA MWEZI MMOJA?
 
Sina utaalam wa kitabibu lakini huyo mwenzi wako amewahi kusumbuliwa na tatizo lolote na akahisi ana minyoo? amewahi kwenda hosp?

Kama ni mjamzito asinywe hizo dawa mpaka ashauriwe na daktari. Umewahi kumuuliza kwa nini hataki kuzaa kwa sasa na mpaka anataka kutoa huo ujauzito?

NB:k Kwanini unaendelea kukaa na binti wa watu bila ndoa? Maana hapa umesema ni gf wako.
 
Bwana Bujibuji, this is very interesting my dear, amekwambia kuwa ana mimba lakini akakushauri kuwa anataka kutoa. Hivi kutoa si ndio abortion? au nakosea? What does this mean so far?

Sitaki kukukatisha tamaa lakini chunguza kwanza kuhusiana na uhalali wa hiyo mimba kama ni ya kwako au la. Kwa fikira zangu nilitegemea huyu GF wako angefurahi kusikia wewe umeipokea hiyo mimba kwa moyo mkunjufu
 
Pole sana mkuu nilishawahi kukutana na situation kama hiyo.

Mchumba wangu alikuwa na mimba na hakuwa tayari kuzaa, nilijitahidi sana kumconvince yeye alichokuwa anataka ni abortion tu. Sababu nilikuwa nahitaji mtoto tena wa kwanza muda wote nilikuwa na hofu ya mimba kutolewa, hata alipokuwa akiniaga anakwenda mjini nilichokuwa nawaza ni hicho tu.

Aliyenisaidia alikuwa ni bestfriend wake ambaye alimwambia ukitoa mimba bila ruhusa ya mwenye mimba waweza kufa na akamwambia watu wengine kwenye koo zao mimba zao huwa hazitoki ukizitoa waweza kufa hivyo itabidi ushauriane na mwenye mimba.

Alipokuja kwangu alijifanya kunitega kwa maswali kama kwetu watu wanakufaga kwa kutoa mimba.sababu best yake alishaniambia mchezo wote aaah kwangu ilikuwa kama kuua tembo kwa ubua.

Nilimpa takwim za uongo tena huku machozi yakinilengalenga.now i am a dad of three months healthier baby!!.

Dawa za minyoo hazitoi mimba ila kwa ushauri, asinywe dawa yoyote bila ushauri wa daktari sababu mimba ni special case na hata wauza madawa hawakubali kutoa dawa kwa wajawazito bila cheti labda isiyoonekana kama ya girlfriend wako.
 
pole sana mkuu nilishawahi kukutana na situation kama hiyo.mchumba wangu alikuwa na mimba na hakuwa tayari kuzaa,nilijitahidi sana kumconvince yeye alichokuwa anataka ni abortion tu.Sababu nilikuwa nahitaji mtoto tena wa kwanza mda wote nilikuwa na hofu ya mimba kutolewa,hata alipokuwa akiniaga anakwenda mjini nilichokuwa nawaza ni hicho tu,aliyenisaidia alikuwa ni bestfriend wake ambaye alimwambia ukitoa mimba bila ruhusa ya mwenye mimba waweza kufa na akamwambia watu wengine kwenye koo zao mimba zao huwa hazitoki ukizitoa waweza kufa hivyo itabidi ushauriane na mwenye mimba.Alipokuja kwangu alijifanya kunitega kwa maswali kama kwetu watu wanakufaga kwa kutoa mimba.sababu best yake alishaniambia mchezo wote aaah kwangu ilikuwa kama kuua tembo kwa ubua.nilimpa takwim za uongo tena huku machozi yakinilengalenga.now i am a dad of three months healthier baby!!.Dawa za minyoo hazitoi mimba ila kwa ushauri Hasinywe dawa yoyote bila ushauri wa daktari sababu mimba ni special case na hata wauza madawa hawakubali kutoa dawa kwa wajawazito bila cheti labda isiyoonekana kama ya girlfriend wako.

Kweli dunia ina mambo, xperience tamu lakini iko very brief, tuandikie in detail utaokoa wengi mshikaji
 
Hizo dawa zimeandikwa kuwa asitumie mama mja mzito. Kwamba zinatoa mimba au kuharibu sijui.

Ila wanawake wengi hujaribu kutoa mimba kwa njia za hatari hatari sana kwa sababu hawana elimu ya uzazi. Matokeo yake huishia na madhara kibao hadi kifo kwa wengine.

Kama mimba haitakiwi si aende kunakohusika ajieleze apewe ushauri nasaha?
 
Ndugu Bujibuji,

Kuwa makini sana na huyo rafiki yako, kama ulivyo sema yeye akufurahia icho kitendo cha yeye kupata ujauzito na akakushauri mkaitoe, naona hapo kuna kamchezo anachotaka kukuchezea, anaweza kutumia hiyo dawa alafu akuambie mimba imearibika kutokana na hiyo dawa.

Ushauri: Mwambie asitumie hiyo dawa kwani mimba yake bado ni changa, na anapaswa kutumia dawa kutokana na ushauri wa daktari tu na sio vinginevyo.

Kama anahisi ana minyoo mpeleke hospitali mwenyewe akachekiwe.kitu kingine mkuu ebu jaribu kumchunguza kama yupo tayari kukuzalia mtoto maana usije kuta huyo msichana yupo na wewe tu kwa sababu zake binafsi na hana lengo lolote na wewe.

Swala la kuzaa mkuu sio la kukurupuka tu na kuchukua maamuzi ya ghafla,kaa nae chini mzungu mzie jambo hilo kwa makini.
 
Pole kaka, chunguza kwa umakini kwa nini anataka mimba itolewe, yawezekana hauko peke yako na inawezekana kabisa hiyo mimba si yako thus why anataka ku-abort, jaribu kukaa nae na umweleze madhara ya kufanya abortion yako mengi tu.

Nina wasiwasi kama anakupenda kwa dhati,au isije ikawa anakupima aone msimamo wako,maana wakati mwingine dada anaweze kuamua kukuchemsha.

Hii story yako imenikumbusha issue kama hii ilitokea mwaka jana,jamaa ana gf wake akamwambia hivyo kuwa ana mimba,jamaa kafurahia, mara dada akamwambia nataka kuitoa, jamaa akabaki anashangaa kwa nini anataka kuitoa, akanifata kuniomba ushauri nikamwambia akae na gf wake aongee nae ampe strong reasons kwa nini anataka kutoa, jamaa kajitahidi kukaa na huyo dada waongee kwani mdada anaelewa, ikabidi jamaa amtafute rafiki yake wa karibu na gf wake aongee nae, alipoongea na rafiki yake akamweleza kuwa wala hana mimba shida yake ilikuwa ni pesa maana alikuwa chuoni kwa wakati huo,jamaa alichoka.

Kwa hiyo kaka hebu jaribu hata kumtafuta rafiki yake wa karibu inawezekana amemgusia hiyo issue.
 
Ninavyofahamu mimi, mama mjamzito hatakiwi kutumia sawa za minyoo.

In the recent days nikamsikia daktari mmoja akaniambia anazuiliwa kutumia dawa hizo katika miezi mitatu ya kwanza ya ujazito wake baada ya hapo anaruhusiwa kutumia.

Sina hakika kama zinatoa ujauzito,lakini nina hakika zina teratogenic effect(naomba mwenye kufahamu kwa kiswahili alezee). Alisema mama wajawazito wenye HIV wanapewa dawa za minyoo,its a policy, Lakini ni baada ya hiyo miezi mitatu
 
Huyo demu hajakumind wala nini.Demu aliyekumind hawezi kusema anataka kutoa.

Ninavyojua mimi wanaume ndio wanakuwa hawahesabu mtoto mpaka azaliwe na ngoma yao inakuwa ngumu kwa sababu mara nyingi wanawake wanataka watoto, sasa hapa tunaona reversal of roles.

Kibongobongo abortion is murder, na kwa mwanamke ambaye ana a biological connection na mtoto ku advocate hili zaidi ya mwanaume inaonyesha yuko heartless na hana mapenzi na wewe.

Kuna kina mama wamezaa shule au katika stage muhimu sana za careers zao kwa hiyo hamna excuse hapa, unless kama kuna medical reasons ambazo hujazitoa.
 
Jamani asanrteni sana kwa ushauri na maoni yenu mbalimbali.

Mmenifungua akili yangu finyu na nimetua lile zigo la mawazo nililokuwa nalo.

Nasema asanteni sana.

Kweli hiki ni kisima cha maarifa.
 
Jamani asanrteni sana kwa ushauri na maoni yenu mbalimbali.
Mmenifungua akili yangu finyu na nimetua lile zigo la mawazo nililokuwa nalo.
Nasema asanteni sana.
Kweli hiki ni kisima cha maarifa.

Ukisoma maelezo ya hiyo dawa (zentel) imeandikwa kabisa kuwa wajawazito wenye mimba changa wasitumie hiyo dawa ,na utafiti wao walioufanya kwa kumjaribu panya mwenye mimba unaonyesha panya huyo alipata matatizo yalio pelekea mimba kuharibika.
 
wadau salama sana,
leo nimekuja na swali moja kuhusiana na hii dawa ya kuua minyoo ya AZANTEL kuwa inauwezo wa kutoa mimba?
 
Sina uhakika Zentel (albendazole) kama inatoa mimba au la, lakini haishauriwi kuitumia kwa wajawazito.

Nadhani maelezo haya hapa chini yatasaidia:

ZENTEL is used to clear worms or parasites from the gut and other tissues. ZENTEL is effective against threadworm or pinworm, roundworm, whipworm, tapeworm and hookworm among others.

ZENTEL is thought to kill these worms by causing them to starve. The eggs, larvae and adult worms are affected.

Do not take ZENTEL if:
* you have had an allergic reaction to albendazole or any of the other ingredients contained in thismedicine. Albendazole is also contained in Eskazole. The ingredients are listed at the end of this leaflet. Signs of an allergic reaction may include an itchy skin rash, shortness of breath and swelling of the face or tongue.

* if you have taken albendazole before and became unwell, tell your doctor or pharmacist beforetaking the first dose.

* you are allergic to medicines similar to albendazole such as mebendazole (Sqworm, Vermox)or thiabendazole (Mintezol).

* YOU KNOW OR SUSPECT YOU ARE PREGNANT. Pregnancy must be avoided (ie use effective contraceptive measures) during treatment, and for one month after stopping ZENTEL. In order to avoid taking ZENTEL during early pregnancy, treatment with ZENTEL should only be started during the first week of having your period or after a negative pregnancy test.

* you are breast feeding. Your baby can absorb albendazole from breast milk if you are breast feeding. Breast feeding should be stopped while taking ZENTEL, and for at least 5 days after finishing treatment.

* the expiry date printed on the pack has passed.

* the packaging is torn or shows signs of tampering.

ZENTEL is not recommended for children under 2 years of age. Do not give this medicine to anyone else; your doctor has prescribed it specifically for you and your condition.

Source: www.betterhealth.vic.gov.au
 
thanks mkuu sasa dosage inakuwaje kuna Pharmacy nimekutana na jamaa ananiambia kama nina tatizo sugu la minyoo naweza kutumia kwa siku tatu mfululizo je hii ikoje?
 
thanks mkuu sasa dosage inakuwaje kuna Pharmacy nimekutana na jamaa ananiambia kama nina tatizo sugu la minyoo naweza kutumia kwa siku tatu mfululizo je hii ikoje?

Jojipoji,
Usiitumie dawa hiyo kama hujaandikiwa na daktari (mfamasia anaweza kukupotosha!).

Ni vema ukafanyiwa uchunguzi kwanza kabla ya kuanza kuitumia. Prescription daktari ndio atakaye andika kutokana na matokeo ya uchunguzi wake.

Pole sana.
 
Sina uhakika Zentel (albendazole) kama inatoa mimba au la, lakini haishauriwi kuitumia kwa wajawazito.

Nadhani maelezo haya hapa chini yatasaidia:

ZENTEL is used to clear worms or parasites from the gut and other tissues. ZENTEL is effective against threadworm or pinworm, roundworm, whipworm, tapeworm and hookworm among others.

ZENTEL is thought to kill these worms by causing them to starve. The eggs, larvae and adult worms are affected.

Do not take ZENTEL if:
* you have had an allergic reaction to albendazole or any of the other ingredients contained in thismedicine. Albendazole is also contained in Eskazole. The ingredients are listed at the end of this leaflet. Signs of an allergic reaction may include an itchy skin rash, shortness of breath and swelling of the face or tongue.

* if you have taken albendazole before and became unwell, tell your doctor or pharmacist beforetaking the first dose.

* you are allergic to medicines similar to albendazole such as mebendazole (Sqworm, Vermox)or thiabendazole (Mintezol).

* YOU KNOW OR SUSPECT YOU ARE PREGNANT. Pregnancy must be avoided (ie use effective contraceptive measures) during treatment, and for one month after stopping ZENTEL. In order to avoid taking ZENTEL during early pregnancy, treatment with ZENTEL should only be started during the first week of having your period or after a negative pregnancy test.

* you are breast feeding. Your baby can absorb albendazole from breast milk if you are breast feeding. Breast feeding should be stopped while taking ZENTEL, and for at least 5 days after finishing treatment.

* the expiry date printed on the pack has passed.

* the packaging is torn or shows signs of tampering.

ZENTEL is not recommended for children under 2 years of age. Do not give this medicine to anyone else; your doctor has prescribed it specifically for you and your condition.

Source: www.betterhealth.vic.gov.au

Kwanza mkuu nashukuru kwa kuileta hii maneno hapa,binafsi nilikuwa najua kwamba albendazole ni contraindacated kwa mama mja mzito.Lakini hivi karibu niliwahi kuhudhuria workshop moja ya watu wanaohusika na masuala ya HIV,wakasema albendazole is contra-indicated in the first trimester,there after its ok.Nafikiri katika Hiv treatment guideline (new edition) ya tanzania maelezo ya kitu yatakuwepo.Na pia sidhani kama tatizo ni kutoka kwa mimba kwani hata hapo juu katika maelezo uliyoyaweka hayajaainisha tatizo.Na kulingana na hawa jamaa,wakina mama wajawazito wenye vvu wanapewa albendazole after the first trimester.
 
Jojipoji,
Usiitumie dawa hiyo kama hujaandikiwa na daktari (mfamasia anaweza kukupotosha!).

Ni vema ukafanyiwa uchunguzi kwanza kabla ya kuanza kuitumia. Prescription daktari ndio atakaye andika kutokana na matokeo ya uchunguzi wake.

Pole sana.

Ni kweli ni vizuri ukaenda kupima ili ijulikane una minyoo ya aina gani kwani hata dozi zinatofautiana kulingana na aina ya minyoo utakayokutwa nayo.Lakini pia chance za toxicity kutotea ni ndogo kwani ni kiasi kidogo sana cha dawa uingia katika mzunguko wa damu.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom