Anselm
JF-Expert Member
- Nov 16, 2010
- 1,710
- 291
Wako watu wanaamini kuwa Azam ni team pekee inayoonekana kuleta changamoto ya kweli katika soka na kumaliza utawala wa miaka mingi wa Yanga na Simba katika mchezo wa mpira wa miguu,binafsi naendelea kuwa mmoja wa wapingaji wa kubwa wa dhana hii.
Kwa mtazamo wangu soka la Tanzania litaendelea kucheza kwenye nafasi ya mia mbili kasoro mpaka hapo Ligi yetu itakapoundwa na team shindani za kweli, sijui lini....katika kipindi hiki ambacho Ligi yetu imejaa team zilizoundwa kwaajili ya kutengeneza njia za team nyingine tusitegemee miujiza.
Juzi tumeshuhudia 1 ya mechi iliyonithibitishia mimi binafsi uwepo wa team zilizopo kwaajili ya team nyingine,Simba kumfunga Azam 3-1 ni evidence tosha ya hili ninaloliamini, haiingii akilini ile team iliyokuwa inasifikia kuwa na ukuta imara na kufungwa magoli ma'2 tu katika mechi 7 inageuka kuwa team yenye ukuta mbovu kuliko wa Mgambo Shooting ya Tanga,kilichonishangaza zaidi ni kutoonekana kwa baadhi ya wachezaji ambao wameshiriki katika mechi 7 zilizoruhusu magoli ma'2 tu..hivi walikuwa wapi George Owino na Erasto Nyoni....je uongozi wa Azam hauoni haja ya kumtaka Kocha wao kujieleza kwa kufanya mabadiliko yasiyo na tija alipotoka Boko ambapo badala ya kumuingiza Mshambuliaji mwingine akamuingiza Kiungo Khamis Mcha na siyo hilo tu kuchelewa kwake kufanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji walioonekana kufa mapema hawaoni kama kulikuwa na tatizo? iweje waliona tatizo la Stewart Hall katika mechi ambayo Azam walipoteza dhidi ya Yanga iliyokuwa katika form ya hali ya juu kwenye michuano ya Kagame? au ksbb ile ilikuwa ni Yanga na hii ni Simba?
Bado nakumbuka shutuma zilizotolewa dhidi ya wachezaji fulanifulani wa Azam baada ya kupoteza mechi ile dhidi ya Yanga wakidaiwa kuhujumu,je uongozi makini wa wana'rambaramba hawa hawajaona element zozote za baadhi ya wachezaji kucheza chini ya viwango vyao hivyo kuhisi hujuma? au wanasubiri mechi na Yanga wakifungwa tena ndo waibue shutuma za hujuma tena?
Hivi kuna mtu anaweza kuniambia sababu ya msingi ya Stewart kufukuzwa Azam licha ya mafanikio aliyoiletea team hiyo katika muda mfupi? kuna kitu kinataka kunijia akilini...usije kukuta Stewart alifukuzwa kwa kimbelembele chake cha kuifunga Simba kwenye robo fainali ya Kagame akajipalia makaa zaidi kwa kitendo cha kufungwa na Yanga? ,inakuwaje Kocha aliyechukua nafasi yake licha ya kufungwa mechi zote na Simba he is still in safe side na si ajabu anaongezewa mshahara, mazingira haya hayatoshi kuonyesha kuwa baadhi ya team zipo kwaajili ya kuzisafishia njia team nyingine kweli? i.e Azam kwaajili ya kusafisha njia ya Simba?
Maswali niliyonayo ni mengi sana,nikisema niyaandike yote hapa naweza kujaza pages and pages.
Nawasilisha!