Ayubu Van Damme Baada ya Jela Ukorofi kama kawa!

Huyo Double Diff last time kumuona ilikuwa 1997 Jamaa alikuwa Dude Dude na sikuwahi kumuona akifanya mazoezi huwa nasikia alikuwa anatuna balaa akiwa anatokea mbele ya njia lazima ugeuze tu utake usitake... hawa ni baadhi ya watu nchini ambao hawajawahi kuonewa... Polisi wakienda kumkamata lazima wambembeleze kama vile Zanzibar wafanyavyo....

Huyu Ayubu Van Damme hata hao watoto wa kinondoni wanamjua kwani huwa ni mjanja sana kama una silaha anakusogelea karibu ndio maana hata polisi always na wanajeshi huchemsha kumchukua ili kumuadhibu na mwishowe huadhibiwa wao..

Kuna siku alizingirwa kwenye nyumba milango yote akavunja ukuta kwa mgongo yaani alienda mbele kisha akarudi kwa nguvu hadi ukutani ukuta ukavunjika then akasepa na machizi...

ha ha ha ha ha....
 
teh teh teh..mkuu toka 2012 una-update tu habari!
...Ayubu kaisha kwa msala gani tena?...kitambo sijamsikia!

Kuna Moja walivunja gari na wakakuta silaha akabeba kwenda ndani akakutwa akimla mtu kiboga kesi iliisha kwa sasa tutamsahau yule si binadamu ni mnyama jela ndio panamfaa
 
Kuna Moja walivunja gari na wakakuta silaha akabeba kwenda ndani akakutwa akimla mtu kiboga kesi iliisha kwa sasa tutamsahau yule si binadamu ni mnyama jela ndio panamfaa

hahahahahaha...ayubu hata jela si unaona anaharibu pia....mi alikuwa mwanangu,japo kitambo sana alitakaga kutuzingua ground Abuja..Midada ndo akamtonya akaushe.,wadogo zake nanilii hao..akaenda kumuomba radhi broda hakujua..toka hapo respect!
...ndo basi tena hawezi badilika!
 
Majina haya yanawaharibu!eti van damme!enzi za ugangwe zimepitwa na wakati.
 
Huyu Mtu Maarufu sana Ndani ya Mji wa Sinza Full Mbabe na alishawahi Shinda Mashindano ya Mr Dar Es Salaam na aliposhinda na kukabidhiwa kikombe akakishika kwa Mkono wake akakiminya hadi kikawa chapati! huku akidai mnanipa kikombe kwani mimi mwanamichezo''' mimi nataka ''hela'' kwa sauti zito...

Huyu jamaa ana nguvu nyingi sana ila mvivu kwenye kufanya kazi i mean hupendelea Ujobless mwili nyumba ngumi tofari akikuzaba kofi unaweza kupatwa na ulemavu hata mishipa ya ndani sehemu alipopiga kofi inaweza hata kupasuka huyu mtu si wa kuchezea ngumi zake ni zaidi ya ajari... akikupiga ngumi lazima ukapate matibabu hospitalini.... sasa tatizo la huyu jamaa ni mwizi kwa kutumia nguvu zake... so anaweza kukusingizia tu kuwa unamchukua mke wake wakati hna then anakunyang'anya kama simu pesa n.k hata nguo amefanya vitu vya ubakaji kwa kila aina...

Alishampiga stop ya kutembea Sinza maisha Dudubaya wakati ule ana heat sana na ubabe wake... nadhani hadi leo Dudubaya no sinza visit....

Alifungwa miaka mitatu na alipotoka ndugu zake wamehama sinza nasikia kakimbilia Kinondoni kwa mzazi wake anaishi so Majuzi kati kamtokea Askari wa Ultimate Security kamsingizia anatembea na mke wake kamzaba kofi la uso kisha kumuibia alivyokuwa navyo askari anapatiwa matibabu ya uso na jicho na amekuwa na mpango wa kuchukua team yake ya ultimate kwenda kumdhibiti ila naona ataongeza maumivu kwa wengine huyo jamaa wanaomuweza ni ndugu zake tu polisi walishamshindwa....

Ningeopmba Serikali wampunguzie Nguvu za mwili huyu jamaakwani ni hatari ukikutana naye madawa yeye bangi yeye ana macho makali sana ukitizamana nae usoni kulishakuwa na watu kama Double Diff mwili mkubwa na alidhibitiwa na kupunguzwa nguvu na wamekuwa wapole tu wanaishi mitaani...

Kama unavituko vyake naomba mviongeze japo ni vibaya ila vinapendeza kusikiliza Amazing Young man

Tuwekee picha yake ili tukikutana nae tuwe tunamkimbia kama kalubandika
 
Tuwekee picha yake ili tukikutana nae tuwe tunamkimbia kama kalubandika

Utamuweza Kwa Mbio? woyi... Yupo Jela sio wa leo wala kesho labda Magufuli amtoe ampe kazi bandarini
 
hahahahahaha...ayubu hata jela si unaona anaharibu pia....mi alikuwa mwanangu,japo kitambo sana alitakaga kutuzingua ground Abuja..Midada ndo akamtonya akaushe.,wadogo zake nanilii hao..akaenda kumuomba radhi broda hakujua..toka hapo respect!
...ndo basi tena hawezi badilika!

Mkuu upiversity inaeleke broda nae alikua jambazi wa kutisha mpaka kuombwa msamaha na jambazi sugu kama hilo.
 
Jamaa huyu hafai katika Jamii bora angetafutiwa tiba ya Madawa ya kulevya kwanza then wampige sindano ya kulainisha mishipa Nguvu zake zinamuwasha sana kuchapa watu makonde...

Ndugu zake ndio wanamuweza kumkamata hata safari ya jela polisi walichemka ndipo ndugu zake wakamtia nguvuni kwa kumvizia walimpiga kama mwizi zaidi ya lisaa zima hadi akachoka

Yani ni kusema na ndugu zake ni mabaunsa pia?duh huo ukoo ni wa kina johncena au?
 
Kuna msiba majuzi liskia kia Damme amefariki alikua south afrika, au sio damme Ayubu Mkobo nn, huu ukoo ni noma wote walikua ni mipande ya watu yana Body sana, Baba yao mzee Mkobo nae alikua mtata alikua na Bittle ya Blue enzi za miaka 1995 kwao walikua na kigorifa Sinza nyuma fens ya Mawasiliano Posta(kwa wa Kush) sasahv Simu2000......
 
Huyu mbabe Ayubu Van Damme bado yupo hai au keshakufa na kama yuko hai yuko uraini au yuko jela bila Shaka atakuwa kashazeeka sana
 
Van dame wa bongo mara ya mwisho namuona alikua dereva au konda daladala za mwenge-posta, kakongoroka haswa
 
Back
Top Bottom