Awekwe wapi kiongozi huyu?

Ticha

Senior Member
Aug 26, 2007
135
8
Katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Rais ni JK
Makamu wake ni Dkt Shain
Namalizia na Mtoto wa Mkulima kama Waziri Mkuu.

Naomba uiendeleze safu yetu hiyo hadi kufikia Mwenyekiti wa serikali yako ya mtaa kama unamfahamu.
Na ni serikali ya Muungano wa Nchi mbili.

JE RAISI WA ZANZIBAR NI NANI KATIKA SERIKALI HIYO YA MUUNGANO?
 
Kuna spika wa Bunge na jaji mkuu...

hold on lengo la huu mjadala ni kuelekea wapi if i may ask
 
Ni raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Huwezi kumweka kwenye level wa serikali ya muungano. Maana tukianza hapo tutataka kujua nafasi ya waziri kiongozi, na mawaziri na wakuu wa mikoa, wilaya mpaka sheha!

Nadhani yatosha kuwaacha wa muungano na serikali yao na wazanzibar na serikali yao
 
Ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi. Katiba ya JMT inamtambua hivo. Anaingia kwenye Cabinet ya serikali ya JMT kwa wadhifa wake. Ukimtafutia nafasi nyingine utakuwa unashusha hadhi yake.
 
Kwa ilivyo, katika serikali ya Muungano yeye anatambulika kama waziri (Lakini sijui ni waziri wa wizara gani).
 
Hii ni serikali ya nchi mbili ndio maana ikaitwa ya muungano, kwa maana hiyo rais wa Zanzibar angekuwa na nafasi katika madaraka ya muungano huo.

Ukidhani ni uongo hata kama ungemuuliza rais wa Zanzibar kuhusu hilo angekwambia kuwa napaswa kuwa na nafasi katika serikali hiyo
 
Fanya ufanyavyo, sema uonavyo, danganya uwezavyo lakini siku moja tutakubaliana kwamba muungano huu una kasoro nyingi.

Ukiishaungana hasa kwa style hii ya muungano wetu lazima kuwepo na chain of command inayo usisha pande zote za muungano, kwa mfano mawaziri wa wizara zilizo kwenye muungano wanaripoti kwa marais wote wawili au wanaripoti kwa rais wa muungano tu?

Kama hivyo ndivyo basi rais wa Zanzibar atakuwa hajatendewa haki. Kuna serikali mbili ndani ya muungano wa nchi mbili, eti moja ni serikali ya muungano yenyewe(maana serikali ya tanganyika haipo) na serikali ya Zanzibar, sasa hii confusion yote ni ya nini?

Halafu kuna shida gani ya kuunganisha wizara zote? Ili tuwe na serikali moja? Mimi bado sana huu muungano unanipa shida kuuelewa maana naona kama ni wizara fulani zimeunganishwa na ni heri serikali ya Zanzibar iwe inapewa nafasi ya kuteua mawaziri wa wizara zilizounganishwa.
 
Wakuu hili ni swali zuri halipaswi kudharauliwa..
Ikiwa mnatambua kwamba huu ni muungano wa nchi mbili na mojawapo ina rais wake iweje huyu rais asiwe na nafasi ktk serikali ya Muungano huo!
 
Ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi. Katiba ya JMT inamtambua hivo. Anaingia kwenye Cabinet ya serikali ya JMT kwa wadhifa wake. Ukimtafutia nafasi nyingine utakuwa unashusha hadhi yake.

......period!
 
Nimeangalia kwenye Tanzania Country report Dec 2009 pp. 37 inayotolewa na Economist Intelligence Unit (EIS), political structure ya nchi yetu ni kama ifuatavyo:

Official Name United Republic of Tanzania
Form of State Republic, formed by the 1964 union of Tanganyika and Zanzibar
Legal system Based on English common law, the 1977 union and 1985 Zanzibar constitutions as amended
National legislature National Assembly (members from the mainland and Zanzibar Parliament; Zanzibar's House of Representatives legislates on internal matters
Head of state President, elected by universal adult suffrage every 5 years
National Government The President, vice – president and Council of Ministers
Main political parties CCM, CUF, NCCR-Mageuzi, UDP, Chadema, TLP

President Jakaya Kikwete
Vice-president Ali Mohamed Shein
President of Zanzibar Amani Abeid Karume
Prime Minister Mizengo Pinda

Tanzania Country Profile 2008 pp. 27 nayo utolewa na Economist Intelligence Unit (EIU) pia inaonesha kuwa muungano wetu hauweleweki vizuri: quote:

Zanzibar
Politics: Zanzibar consists of two Indian Ocean islands, Unguja and Pemba, and several islets. It is ruled as part of the Union but has its own government, which has sovereignty in internal matters. The 1977 constitution granted the Union government competence in external affairs, defence, external trade, currency and similar matters, with the Zanzibari authorities retaining responsibility for the development of the isles and other domestic matters, although the line between the two governments has often been blurred.

Sasa angalia mambo yalivyokorogwa mpaka EIU wameshindwa kuelewa na kusema kama ilivyo kwenye sentensi ya mwisho ambayo nimeizidishia wino na neno la mwisho katika ‘red'. Maana ya ‘blur' ni:
blur noun
/blɜːr / /blɝː/ n [S]
•
something that you cannot see clearly
If I don't wear my glasses, everything is just a blur.
•
something that you cannot remember or understand clearly
It all happened so long ago that it's just a blur to me now.
The last few days seem to have gone by in a blur.
(Definition of blur noun from the Cambridge Advanced Learner's Dictionary)


Kwenye katiba ya URT 54 (1) inasema rais wa Z'bar ni mjumbe wa baraza la mawaziri wa jamhuri ya Muungano; 54 (2) inasema rais wa Jamhuri ya Muungano ndio mwenyekiti wa baraza la mawaziri, kama hayupo basi Vice president ataendesha kikao, kama naye hayupo basi waziri mkuu ataendesha kikao.

Hapa rais wa Z'bar hana nafasi ya kuendesha baraza la mawaziri kama wengine hawapo.

37 (3) (a) – (c) inasema: Rais wa URT akindoka nchini VP anakaimu, VP naye akitoka nje ya nchi Spika wa Bunge la URT anakaimu, naye akitoka nje ya nchi Jaji Mkuu wa mahakama ya rufaa anakaimu kama rais wa URT. (http://www.tanzania.go.tz/constitutionf.html)

Hapa utaona tena Rais wa Z'bar wala PM hawana nafasi ya kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Aliyeleta thread hii anataka tuondoe hiyo "blur": kazi kwetu! Nahisi ‘Blur' ikiondoka huyu jamaa anakuwa waziri mwenye wizara inayoitwa Utawala wa Mkoa na Serikali za Mitaa ya Z'bar!!! Kwani wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inaijumuisha Z'bar? Sasa kuvunja muungano ni sawa na kuacha wizara ijitawale au/ na mkoa ujitenge – ngumu ingawaje Eritrea walifanikiwa!
 
kwakweli katiba hii inavyunjwa sana akitokea rais wa zenj kichwa maji muungano utaishia kubaya sana cha msingi ni kuandika katiba mpya itakayokidhi na kuendana na hali halisi tuache bla bla katika mambo ya msingi
 
Back
Top Bottom