Awatia Mimba Wanawake 12 Aliojuana nao Kwenye Facebook

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
3509926.jpg

Dominic Baronet kulia akiwa na mmoja wa wanawake aliowapachika ujauzito na kisha kuwatekeleza

November 10, 2009 1:49 AM

Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza amebatizwa jina la 'Speminator' baada ya kuwapachika ujauzito wanawake 12 aliofahamiana nao kwenye mtandao wa Facebook wawili kati yao aliwapachika mimba ndani ya usiku mmoja.

Wanawake nchini Uingereza wanaotumia mtandao wa tovuti ya Facebook wameshauriwa kutofanya urafiki na Dominic Baronet, raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni hatari sana katika kuwalaghai na kuwapachika ujauzito wanawake anaofahamiana nao kupitia mtandao wa Facebook.

Katika kuthibitisha kuwa Dominic ni hatari sana kwa kuwapachika mimba wanawake, aliwapachika mimba wanawake wawili ndani ya usiku mmoja na kulifanya gazeti la News of The World la Uingereza limbatize jina la "Sperminator".

Dominic hutumia siku chache kufanikiwa kuwalaghai wanawake anaofahamiana nao kwenye Facebook na kisha kufanya nao mapenzi.

Wanawake watano tayari wameishajifungua watoto wake, wanawake watano wengine wanafikiria kuzitoa mimba zao na wanawake wawili wanatarajia kujifungua watoto wake hivi karibuni.

Miongoni mwa wanawake waliokumbana na zahama la Dominic ni Kerry Martin, 24, ambaye aligundua kuwa Dominic ana wapenzi wengi baada ya kutembelea ukurasa wake kwenye Facebook na kukutana na ujumbe wa Baronet akijipongeza kumpachika ujauzito mwanamke mwingine aliyejulikana kama Stacy Jones mwenye umri wa miaka 24.

Kerry alipounda urafiki na Stacy aligundua kuwa wote wawili walipata ujauzito siku moja ndani ya usiku mmoja isipokuwa nyakati tofauti.

"Dominic inabidi apigwe marufuku kwenye Facebook, anatumia tovuti ya Facebook kuwalaghai wanawake na kuwapachika mimba na kisha kuwatelekeza bila ya kujali matokeo yake", Stacy aliliambia gazeti la News of the World.

Stacy ameutaka uongozi wa Facebook umfute Dominic kwenye mtandao huo na umpige marufuku kujiunga tena.
 
Huyu anaweza ku launch career ya kuwapachika mimba wake wa watu ambao hawawezi kufanya shughuli hiyo.
 
Back
Top Bottom