Elections 2010 Awamu ya Kwanza Kampeni ya Dr. Slaa kuelekea Ikulu

Kumwita kikwete. Dokta[/B]. Hivi, ni ushabiki, ni ufala au ilimbukeni, au kujikomba???[/B]

Aiseee, yani hata mimi hii kitu huwa inanishangaza. Yani jinsi wanahabari wa bongo walivyolikomalia, hadi inakuwa kero, sasa madokta wa ukweli hapa watawaitaje? kaaazi kweli kweli.
 
Wapi Sikonge,umeona Nyomi hiyo ya Mwanza? Mwaka huu na sisi tumeamka,Dr.Slaa si mchenzo,hata akifanyia mkutano uchochoroni watu watakwenda kumsikiliza Rais mtarajiwa! CCM mwaka huu watajibeba!
 
Slaa+Geita.jpg

Dr Slaa anakubalika sana kanda ya Ziwa, lakini mbona naona watoto wapo wengi? Je hawa ni wapiga kura hapo Oct 31?
 
nilikuwa naongea na jamaa yangu ambaye ni askari polisi anaomba sana Dr Slaa apite ili waweze kujenga walau nyumba make maisha magumu inafikia wanastaafu bila ya kujenga nyumba tokana na kodi kubwa ya vifaa vya ujenzi
 
.....Na pia hukusanya lundo la wanafinzi na kuwapeleka kwenye mkutano ili waongeze idadi ya waudhuliaji.

Mbona hata kwenye hiyo picha mliyotuma kumejaa watoto wengi? Kampeni za uchaguzi ni sinema tosha kwa wananchi wengi hasa huko mikoani.

Kumbukeni ya Mrema 1995, sio tu kwamba wananchi walienda wenyewe, bali pia walimbeba juu juu kama maiti lakini ilipofikia siku ya uchaguzi wakaipigia CCM.

Dr. Slaa usibweteka, endelea kukata mbuga hasa huko vijijini. Njia ya kwenda Ikulu bado ni ngumu sana na imejaa miiba. Inatakiwa uwe na watu mara tatu ya JK kwenye mikutano yako.

Halafu mikutano mingi ya kampeni naona inajaa wanaume tupu. Angalieni sana kura za wanawake, hizo ndio zina uhakika na wako wengi na wakiamua huwa habadiliki kirahisi.
 
nilikuwa naongea na jamaa yangu ambaye ni askari polisi anaomba sana Dr Slaa apite ili waweze kujenga walau nyumba make maisha magumu inafikia wanastaafu bila ya kujenga nyumba tokana na kodi kubwa ya vifaa vya ujenzi

binafsi nilikataa kazi ya upolisi kulingana na mazingira ya kazi hiyo, na polisi tz kuonekana kama mganga njaa tu,
wanafuarahia flat zilizojengwa ufundi polisi kana kwamba watapewa mara baada ya kustaafu, maisha ya pilisi ni magumu kupita kiasi
 
Mbona hata kwenye hiyo picha mliyotuma kumejaa watoto wengi? Kampeni za uchaguzi ni sinema tosha kwa wananchi wengi hasa huko mikoani.

Kumbukeni ya Mrema 1995, sio tu kwamba wananchi walienda wenyewe, bali pia walimbeba juu juu kama maiti lakini ilipofikia siku ya uchaguzi wakaipigia CCM.

Dr. Slaa usibweteka, endelea kukata mbuga hasa huko vijijini. Njia ya kwenda Ikulu bado ni ngumu sana na imejaa miiba. Inatakiwa uwe na watu mara tatu ya JK kwenye mikutano yako.

Halafu mikutano mingi ya kampeni naona inajaa wanaume tupu. Angalieni sana kura za wanawake, hizo ndio zina uhakika na wako wengi na wakiamua huwa habadiliki kirahisi.

Sasa ukitaka wakawabebe wanawake na malori waje kwenye mkutano? Au Ulitaka wawakataze watoto wasije kwenye mkutano au
 
:crutch:
Slaa+Geita.jpg

Dr Slaa anakubalika sana kanda ya Ziwa, lakini mbona naona watoto wapo wengi? Je hawa ni wapiga kura hapo Oct 31?

Watoto wapi kama hawa utawazuia mahali hapa? Tofauti nim kwamba hawana uniforms za shule wako kwa wanajinafasi ama vipi ni wapiga kura watarajiwa.,
 
Kiukweli kupanga nyumba mjini au kutafuta pa kuishi ni adhabu tosha. Nyumba zinapanda kodi kila siku. Nyumba zenyewe viwango duni. Zile viwango safi kodi ni maumivu. Madalali nao micharuko, basi alimradi fujo tu. Tumchague slaa tupate unafuu wa ujenzi
 
Kwa wenzetu nchi kama veitnam mfuko wa simenti wa kilo 100 ni tshs 2500 za Tanzania na vifaa vya ujenzi havina kodi , gharama ya ujenzi wa nyumba Tz ni mara 7 ya vietnam uwezi kuamini....... Dawa ni kulinda waiba kura CCM wasitupotezee Rais wetu. Chadema lindeni kura mengine yanawezekana
 
Nawashauri Chadema walinde kura zao . Maana jitihada zote za kufanya kampeni hazitakuwa na manufaa kama hatutalinda kura zetu. Maana Mtaji wa CCM ni kuiba kura ndio maaana wanatumia umasikini wa mawakala na wasimamizi wa chaguzi kwa kuwarubuni kwa Tshs 10,000 mpaka laki moja na wanjizolea mamia ya kura ambozo mpinzani amezitafuta kwa jitihada kubwa. Chaedema lindeni kura na mengine yote yanawezekana
 
Back
Top Bottom