Haiwezekani! Tanzania ni nchi maarufu sana Afrika. Na umaarufu huo hautokani na jina la nchi kuwa zuri, bali utendaji wa marais wake pamoja na timu yake.
Hivi sasa ni miaka zaidi ya 40 toka tupate uhuru, Tanzania bado ni kioo na mfano kwa Afrika licha ya umasikini wetu. Kwani umasikini ni bahari ya Afrika nzima.
Kwahiyo sikubaliani nawe pale unaposema hayupo bado. Basi angalau ungesema ni yupi aliyekuwa afadhali, maana hata katika wajinga kuna kiongozi ambaye anaonekana kuwa mzuri kuliko wengine.
Nahisi bora ungewauliza hao wanaowaona umaarufu wa Tanzania kwa walio nje ya nchi kuwa kigezo cha ubora ama kwa sisi tunaotaka maendeleo iwe kipimo "tunasema Hayupo"