Avua nguo Mahakamani Baada ya Kukosa dhamana

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,124
MSHITAKIWA Saidi Said [27] anayekabiliwa na kesi ya kuvuna zao haramu la bangi huko Chanika juzi alitoa kituko cha mwaka katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya kuvua nguo mahakamani na kubaki mtupu kama alivyozaliwa baada ya kukosa dhamana. Mshitakiwa huyo alifikishwa Mahakamani hapo mwishoni mwa mwezi uliopita akikabiliwa na shtaka la kulima zao la bangi kinyume na sheria za nchi.

Mshtakiwa hayo alisomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashitaka Mussa Gumbo mbele ya Hakimu Janeth Kinyage wa Mahakama hiyo.

Awali ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alikamatwa na askari wa doria huko Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam akiwa na bangi yenye uzito wa kilogramu 150 ambayo alikuwa ameivuna na kuiweka pembezoni mwa shamba lake.

Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo akisema kuwa hahusiki na ulimaji wa zao hilo na kwamba watu waliweka bangi hizo kwenye shamba lake bila ya yeye kuwa na taarifa.

Ilidaiwa kuwa upelelezi wa shauri hilo ulishakamilika na vielelezo vilifikishwa Mahakamani na gunia hilo la majani ya bangi lilifikishwa mahakamani kama kielelezo.

Siku hiyo mshitakiwa huyo hakuweza kupata dhamana kwa kuwa hakuwa na watu wa kumdhamini.

Mshtakiwa huyo aliporudishwa kwa mara ya pili katika mahakama hiyo aliiambia mahakama kuwa yeye halimi zao hilo ila yeye anavuta tu na sio kulima.

Mshtakiwa huyo alirudishwa tena rumande kwa kukosa dhamana kwa mara nyingine tena.

Juzi alipofikishwa tena katika mahakama hiyo mshtakiwa huyo alimwambia Hakimu kuwa anaomba aachiwe kwa kuwa kesi hiyo alisingiziwa ingawa alikubali kuwa yeye anavuta bangi.

Hakimu alimtaka kuwa asubiri hadi siku ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo ataweza kujielezea vizuri na kumuamuru alete wadhamini ili adhaminiwe lakini mshtakiwa huyo alidai kuwa hana ndugu wa kumtolea dhamana.

Hakimu alimwambia kuwa yeye hana mamlaka ya kumpa dhamana pasipo na yeye mwenyewe kuwa na wadhamini mahakamani kwakuwa akifanya hivyo atakuwa ametengua vifungu vya sheria vya nchi.

Katika hali ya kushangaza mshitakiwa huyo alianza kuvua nguo mahakamani hapo na kumfanya hakimu huyo mwanamke aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo kuogopa kushambuliwa na kijana huyo.

Mwendesha Mashtaka alisimama na kumuamuru kijana huyo avae nguo zake na baadae alirudishwa rumande.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2281790&&Cat=1
 
watu wamedata...kabisa maana jela si kuzuri kabisa alikuwa anajitetea labda angesamehewa....
 
Back
Top Bottom