Autorun sio Virus

Nyasiro

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
1,200
551
Autorun sio virus!!! Hizi ni files ambazo zinabeba instruction na kusaidia files/program husika kufunguka hasa pale unapoweka CD au Flash

Kwa nini sio virus?

  • Kwanza ina extension ya .inf ambayo haizwezi moja kwa moja kudhuru pc yako
  • Pili autorun inaweza kuwa modified kirahisi kuliko .exe au bat

Umuhimu wake?
  • Inasaidia kulaunch files/progs automatically

Jaribu kutengeneza autorun kwa ajili ya Flash yako:

Fungua NotePad halafu andika:

[AutoRun]
open=Setup.exe
icon=Setup.exe

Ukimaliza save hiyo file na uipe jina hili: Autorun.inf

NB: Kitu cha muhimu ni open then = halafu unaandika file ambalo unataka lifunguke ukiweka flash(hili faili lazima liwe kwenye flash). Kwenye icon unaandika icon then = halafu jina na extension ya icon sio lazima uweke setup(icon lazima iwe kwenye flash) hii icon itatokea kwenye My Computer pale kwenye drive yako badala ya default icon!

Chukua setup file yoyote halafu uiweke kwenye flash
Chukua na hilo file ulilotengeneza yaani autorun.inf uliweke ulipoweka setup HALITAKIWI LIWE NDANI YA FOLDER
Sio lazima uandike Setup unaweza tumia jina lingine
Chomoa halafu chome tena flash. Kama kila kitu umefanya sawa setup itafunguka na icon kwenye my computer nayo itabadilika. Jaribu afu toa majibu.



 
Back
Top Bottom