Aunt:Uzinzi nimekoma

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125



Bonyeza maandishi kuona picha hapa chini
Mcheza filamu sistaduu wa Bongo aliye pia Miss Mwanza 2006/07, Aunt Ezekiel Grayson Jujuman ‘Gwantwa’, amebadilika kwani si yule wa mafumanizi na kashfa za ‘kutoka’ na waume za watu, Risasi limebeba kitu kamili.

Aunt wa ‘maskendali’, juzikati alivunja ukimya na kuweka kweupe kwamba, hivi sasa ameacha kabisa uzinzi na kuzengea waume za watu.

Akiongea katika ‘spesho intavyu’ na gazeti lenye heshima kubwa mbele ya mastaa, Risasi, jijini Dar Alhamisi ya wiki hii, Aunt alikiri kukumbwa na ‘kashkash’ lukuki kutokana na tabia aliyokuwa nayo ya kudandia waume za watu.

“Nimechoka kudhalilishwa na wanawake wanaonituhumu kutembea na waume zao. Nimebadilika kwa kiasi kikubwa na ijulikane kwamba, huu ni mwaka mwingine, sihitaji kuendelea kusakamwa,” alisema Gwantwa kwa huzuni kubwa.

Aunt alithubutu kwenda mbele zaidi kwamba, katika uchafu wote huo uliojazwa kwenye sahani moja, ni wanaume wawili tu alionao kibindoni ambao alikuja kugundua kuwa ni ‘mali’ za watu baada ya kuingia nao mkataba wa kizinzi.

Gwantwa aliwataja wanaume hao kuwa ni Mkurugenzi wa Hartmann Productions, Hartmann Mbilinyi na mume wa Miss mwenzake aitwaye Sarah, Mwilu Mwilola ‘Silvanus’ ambao aliingia nao kwenye uhusiano wa ‘kibaba na mama’, lakini akaishia kutendwa.

Alisema, katika vitu vilivyoutesa moyo wake ni kitendo cha kupakiwa rundo la kashfa chafu chafu zilizomnyima raha duniani na kuahidi kwamba, aibu yote iliyompata katika kipindi hicho itabaki kuwa ni historia.

“Kusema kweli nimekoma mie. Nimekosa raha kwa muda mrefu duniani, lakini aibu yote hiyo itabaki kuwa ni historia kwani ya kale yamepita natazama mapya,” alisema Aunt.

Sistaduu huyo alimalizia kwa kula kiapo cha kutoingia kwenye uhusiano ‘mbofu mbofu’ hadi hapo atakajiridhisha kwa kumpata mwanaume wa dhati wa kumuoa.

“Kwa sasa sina mwanaume na sihitaji kwani niko ‘bize’ nasaka mshiko, lakini naapa kutojiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi hadi nitakapopata mwanaume wa kunioa nitakayeridhika naye.

Kabla ya tamko hili, Aunt alikwisharipotiwa kuwa na mchumba ambaye alimtema alipopanda kwenye jukwaa la kuwania ‘krauni’ ya Miss Tanzania 2006 ambapo haukupita muda akaanikwa akiwa ‘kifuani’ kwa Mfanyabiashara ‘The Big Boss in Town’, Pedeshee Jack Pemba ambaye alikuwa ni mtu na ndoa yake changa.

Safari ya mapenzi ya Aunt ilitumbukia nyongo siku chache baada ya mwenye chake kushtukia mchongo ambapo ‘solusheni’ ilikuwa ni kumponyoka pedeshee huyo.

Baada ya hapo, Aunt alijikuta ‘akibanjuka’ na Hartmann, lakini napo hapakuwa salama kwani baadaye alikuja kunusa kuwa kibosile huyo alikuwa ni mtu na ndoa yake takatifu.
Funga kazi ilikuwa kwa mume wa mtu, Silver ambaye katika siku za awali za uhusiano wao, Aunt aliripotiwa kufumaniwa laivu ‘red handed’ na mke wa jamaa huyo.
http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/auntuzinzi-nimekoma
 
Kwahiyo aweke wazi gonjwa lake anaenda kabidhiwa nani watu wajiandae
 
- Duh!! huyo Aunt anapata faida gani kugawa gawa mwiliwake:angry: wanawake wengine bwana Kha!!!!!!!!!!!!!!!! hawadhamini maungo yao:angry:
 
Back
Top Bottom