Augustino Mrema: Behind the Scene

Salim A Salim

Positions held in Tanzania
  • Chief Editor of a Zanzibar daily paper, Secretary General of the All-Zanzibar Journalists Organisation 1963–1964
  • Minister for Foreign Affairs 1980–1984
  • Prime Minister of Tanzania 1984–1985
  • Deputy Prime Minister of Tanzania 1986–1989
  • Minister for Defence and National Service 1986–1989
  • President of the Julius K. Nyerere Foundation 2001 – current
 
Ni kiongozi pekee wakati akiwa Naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani kwenye serikali ya CCM aliyekuwa anatoa siku saba tu kwa mhalifu yeyote inchini kujitokeza na kujieleza mbele yake bila upendeleo. Aliwafanya watu waiogope serikali na mali zake tofauti na sasa ambapo serikali yenyewe imejaa wadokozi kama alivyosema Tundu Lissu.
 
Naendelea...
1. Ndiye muasisi wa dhana nzima ya 'polisi
jamaa' akiita 'sungu sungu'..mzaz gan
ambaye hakuwah kuwa mlinz kipnd kle?
2. Kiongoz pekee mwenye uwezo wa
kuzururura usiku akiwa na kibukta katika
maeneo ya madada poa na wachoma
nyas..ili kutengeneza 'pschological unrest
ili waache uhalifu!
Mkuu nakubaliana na wewe kiasi ila jeshi la sungusungu lilikuwepo toka enzi za vijiji vya ujamaa miaka ya 70 likafifia, sema Mrema likuja kulifufua upya miaka ya 80 alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.
 
  • Ni mtu pekee ambaye amekuwa mbunge katika majimbo mawili tofauti. Alikuwa mbunge wa Jimbo la Temeke mkoani Dar Es Salaam mnamo mwaka 1996 baada ya mahakama kutengua ubunge wa Ally Kihiyo, ambaye alighushi elimu yake katika wasifu wake, na kwa sasa Mrema ni mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro

Murji Muhamed Hasnain ni mbunge ambaye ametumikia wilaya karibu zote za mkoa wa Mtwara - Newala, Tandahimba na Mtwara Mjini
 
naweka kumbukumbu sahihi, Mzee wa Kujaza mapesa amewahi kuwa Mbuge wa majimbo mawili tofauti
 
Mrema amewahi kuwa mbunge kwa kupitia yama vitatu tofauti CCM, NCCR Pamoja TLP
 
na wuro meeku,
mimi nilipita hiyo njia nikiwa naenda kilema kuchukua mwili wa mzee wangu
ndo nikaipata hiyo, ila kwetu ni kumoja mkuu.

mkuu mamdenyi inaelekea tumetoka sehemu moja, mbonyi mbee
 
Ni muasisi wa siku 7... zilikuwa zikifika pia anakumbuka alichokiagiza na anatoa feedback....Tofautisha na mkuu wa kaya aloagiza uzio wa bati pale jangwani ubomolewe kinyume chake.... Lol.
 
Ni waziri pekee aliyekuwa anaingilia maamuzi wa wizara zingine,
Aliamuru wenye maduka kupanda miti mbele ya maduka yao na kulazimisha wahindi
wa mtaa wa Samora na uhuru dar kutoboa velanda za zege ili wapande miti na alifanikiwa.
hii naikumbuka ilikua saaafi saana
 
Ni mtu pekee ambae jina lake ni Augustine Lyatonga Mrema :rolleyez:,
Nadhani tukiangalia kila mtu ni unique
 
Mnyonge Mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
Katika kikao cha saba cha bunge lilohitimishwa jana, kamati yake ya Hesabu za serikali a mitaa ilitoa ripoti moja nzuri sana juu ya ubadhirifu mkubwa ulioonekana katika serikali za mitaa. Kamati yake, tofauti na kamati nyingine za bunge, ilithubutu kutaja kwa majina na mahali walipo wahusika wa ubadhirifu wa mali za halmashauri na kutoa mapendekezo mazuri sana ya hatua za kuchukua dhidi ya wahalifu hao na namna ya kuzuia wizi huo kwa siku zijazo. Mheshimiwa huyu aliongea kwa uchungu sana namna anavyoumizwa na wizi huu, huku huduma za kijamii zikizorota kwa kukosa pesa.

Behind the Scene (vibwagizo)

  • Mrema ni mtu pekee ambaye amewahi kupewa cheo kisichotambulika katika katiba ya nchi (Naibu waziri Mkuu), enzi za mzee Ruksa. Enzi hizo pia alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani na utendaji wake ulijulikana sana.
  • Ni mtu pekee ambaye amekuwa mbunge katika majimbo mawili tofauti. Alikuwa mbunge wa Jimbo la Temeke mkoani Dar Es Salaam mnamo mwaka 1996 baada ya mahakama kutengua ubunge wa Ally Kihiyo, ambaye alighushi elimu yake katika wasifu wake, na kwa sasa Mrema ni mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro
  • Ni mtu pekee ambaye amekuwa mwenyekiti wa vyama viwili tofauti vya kisiasa kwa nyakati fofauti na amegombea uraisi kupitia vyama hivi viwili tofauti. Alikuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mnamo mwaka 1995 enzi hizo Mabere Marando akiwa katibu mkuu na aligombea ubunge mwaka huo. Alihama NCCR na kuhamia TLP ambako alimpindua Leo Lwekamwa na kumtimua Thomas Ngawaiya aliyemkuta hapo, na amegombea uraisi mara mbili kwa tiketi ya chama hiki.
  • Ni mmoja wa wabunge waliokunywa 'Kikombe' cha Babu Ambilikile Mwasapile wa Loliondo

Mwenye vibwagizo zaidi aongezee
Nawasilisha

Kweli Mrema alisoma taarifa nzuri na kama kawaida yake huwa analia machozi ya mamba. Jana alikaribia kutoa machozi ya mamba.

Hapo kwenye blue si kweli kwamba Mrema ni mtu pekee aliyewahi kupewa cheo cha Naibu Waziri Mkuu. Dr. Sali Ahmed Salim aliwahi kupewa cheo hicho mwaka 1985 baada ya Mwinyi kuchukua Madaraka na ikabidi Salim otolewe kwenye Uwaziri Mkuu (Katiba ilikataa) hivyo akawa Waziri wa Ulinzi na JKT pia Naibu waziri Mkuu!

Hapo kwenye Red: Si kweli pia kwamba Mrema ni Mbunge pekee ambaye ametumikia majimbo mawili. Yupo huyu mtu anaitwa Kisyeri Werema Chambiri alikuwa Mbunge wa Tarime miaka ya hapo nyuma na sasa ni Mbunge wa Babati Mjini.

Nilikuwa nataka kuweka historia sawa.

  • Mrema pia anakumbukwa kwa kumnyang'anya Chama mwasisi wa TLP bwana Leo Lwekamwa.
  • Anakumbukwa pia kwa kushiriki kukinyong'onyeza chama cha NCCR mageuzi
  • Mrema namkumbuka kwa kuwaamuru wanunuzi wa korosho watoke Mtwara wamfuate Moshi ili akawahoji
  • Alikuwa mpatanishaji mzuri sana wa migogoro ya kinyumba
  • Alipokuwa Shinyanga aliwatesa vikongwe
  • Hakujiuzulu nafasi ya Unaibu waziri mkuu/waziri wa mambo ya ndani ila aliondolewa na kupewa wizara ya kazi na kuamua kuachia ngazi.
 
Kweli Mrema alisoma taarifa nzuri na kama kawaida yake huwa analia machozi ya mamba. Jana alikaribia kutoa machozi ya mamba.

Hapo kwenye blue si kweli kwamba Mrema ni mtu pekee aliyewahi kupewa cheo cha Naibu Waziri Mkuu. Dr. Sali Ahmed Salim aliwahi kupewa cheo hicho mwaka 1985 baada ya Mwinyi kuchukua Madaraka na ikabidi Salim otolewe kwenye Uwaziri Mkuu (Katiba ilikataa) hivyo akawa Waziri wa Ulinzi na JKT pia Naibu waziri Mkuu!

Hapo kwenye Red: Si kweli pia kwamba Mrema ni Mbunge pekee ambaye ametumikia majimbo mawili. Yupo huyu mtu anaitwa Kisyeri Werema Chambiri alikuwa Mbunge wa Tarime miaka ya hapo nyuma na sasa ni Mbunge wa Babati Mjini.

Nilikuwa nataka kuweka historia sawa.

  • Mrema pia anakumbukwa kwa kumnyang'anya Chama mwasisi wa TLP bwana Leo Lwekamwa.
  • Anakumbukwa pia kwa kushiriki kukinyong'onyeza chama cha NCCR mageuzi
  • Mrema namkumbuka kwa kuwaamuru wanunuzi wa korosho watoke Mtwara wamfuate Moshi ili akawahoji
  • Alikuwa mpatanishaji mzuri sana wa migogoro ya kinyumba
  • Alipokuwa Shinyanga aliwatesa vikongwe
  • Hakujiuzulu nafasi ya Unaibu wa
  • ziri mkuu/waziri wa mambo ya ndani ila aliondolewa na kupewa wizara ya kazi na kuamua kuachia
Siyo kweli kwamba E.W.Chambiri amekuwa mbunge ka majimbo yote mawili,huyu mbunge wa sasa wa Babati Mjini ni kaka mtu,ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM,mkoa wa Mara,kabla ya Makongoro Nyerere
 
Ni mgombea urais pekee aliyewahi kutoa ahadi ya kuhalalisha gongo endapo atachaguliwa.
 
Ndie waziri wa mambo ya ndani aliyetuletea kero za kupiga marufuku gomba (gati), miraa. Asisamehewe kwa hili.
 
Back
Top Bottom