Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,963
- 10,460
Mnyonge Mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
Katika kikao cha saba cha bunge lilohitimishwa jana, kamati yake ya Hesabu za serikali a mitaa ilitoa ripoti moja nzuri sana juu ya ubadhirifu mkubwa ulioonekana katika serikali za mitaa.
Kamati yake, tofauti na kamati nyingine za bunge, ilithubutu kutaja kwa majina na mahali walipo wahusika wa ubadhirifu wa mali za halmashauri na kutoa mapendekezo mazuri sana ya hatua za kuchukua dhidi ya wahalifu hao na namna ya kuzuia wizi huo kwa siku zijazo.
Mheshimiwa huyu aliongea kwa uchungu sana namna anavyoumizwa na wizi huu, huku huduma za kijamii zikizorota kwa kukosa pesa.
Behind the Scene (vibwagizo)
Mwenye vibwagizo zaidi aongezee.
Nawasilisha

- Mrema ni mtu pekee ambaye amewahi kupewa cheo kisichotambulika katika katiba ya nchi (Naibu waziri Mkuu), enzi za mzee Ruksa. Enzi hizo pia alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani na utendaji wake ulijulikana sana.
- Ni mtu pekee ambaye amekuwa mbunge katika majimbo mawili tofauti. Alikuwa mbunge wa Jimbo la Temeke mkoani Dar Es Salaam mnamo mwaka 1996 baada ya mahakama kutengua ubunge wa Ally Kihiyo, ambaye alighushi elimu yake katika wasifu wake, na kwa sasa Mrema ni mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro
- Ni mtu pekee ambaye amekuwa mwenyekiti wa vyama viwili tofauti vya kisiasa kwa nyakati fofauti na amegombea uraisi kupitia vyama hivi viwili tofauti. Alikuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mnamo mwaka 1995 enzi hizo Mabere Marando akiwa katibu mkuu na aligombea ubunge mwaka huo. Alihama NCCR na kuhamia TLP ambako alimpindua Leo Lwekamwa na kumtimua Thomas Ngawaiya aliyemkuta hapo, na amegombea uraisi mara mbili kwa tiketi ya chama hiki.
- Ni mmoja wa wabunge waliokunywa 'Kikombe' cha Babu Ambilikile Mwasapile wa Loliondo
Mwenye vibwagizo zaidi aongezee.
Nawasilisha