Augustino Lyatonga MREMA, Namvulia Kofia

Mag3,

Asante kwa kuchangia mada na kutoa mawazo yako. Hata hivyo inaonekana tofauti kati ya mawazo yetu na yako iko kwenye uwezo wetu wa kuchambua mambo. Pia inaonekana kazi ya mrema ilikuzuia (wewe au ndugu yako wa karibu) kufanya jambo fulani (pengine la kifisadi) wakati fulani na hivyo ukajenga chuki kiduchu dhidi yake, chuki ambayo inakuweka pazi unashindwa kuona mambo mengine.
 
Mrema alipambana na ufisadi kwa dhati kabisa na alikuwa haogopi wala kurudi nyuma. Akisimamia jambo ni hadi amng'oe muhusika.

Unakumbuka alivyowakalia kooni akinia Iddi Simba, Profesa Simon Mbilinyi, na yule waziri mwingine nimemsahau jina. Alisimama nao kidete hadi waliachia ngazi hadi leo hawajakuwa tena kwenye serikali. Nakumbuka Iddi Simba ilikuwa ni swala la vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi hao wengine sikumbuki tena issue ilikuwa nini.

Sisi leo tunaimba tu kwamba eti mawaziri wajiuzulu lakini hatuna mikakati ya kuhakikisha madai yetu yanatekelezwa. Mrema alikuwa halali, haogopi, na hapotezi mwelekea akishaamua jambo.
 
Kwamba Mrema amekuwa na mchango mkubwa kwa nchi hii hilo liko dhahiri.
Ila nadhani Mrema anaweza tu kama ana madaraka makubwa hilo linadhihirishwa na utendaji wake pindi alipotolewa Home Affairs na kuwa waziri wa Kazi na Vijana. Mrema ni aina viongozi wanaitwa "One man show".
Kama kuna mtu ana kumbukumbu ya wazi anitajie jambo moja la maana alilofanya akiwa waziri wa Kazi.

Kwa upande wa upinzani Mrema aliikuta NCCR ya kina Marando iko imara, kama entry yake ingeongeza nguvu ya chama basi 2000 tungempiga chini Mkapa. By 2000 upinzani ulikuwa just a disappointment. Kufikia 2000 tayari NCCR kilikuwa kaputi, game likaongozwa na Professor Lipumba with some collaboration with Chadema.

Mwaka 1995 wakati watu tunajitolea kwa hali na mali akatungusha kwenye the only presidential mdahalo ever pale Kilimanjaro. Alitupotezea kura zote maana hakusikiliza ushauri wa kina Mvungi, Marando, Ndimara n.k badala ya kuongea issues yeye akabaki na story ya Chavda na dhahabu uwanja wa ndege akiacha sera nzuri za NCCR, Mkapa (bubu) akaonekana mahiri.

Kama mnataka historia ya kweli ni utani kusema Mrema kachangia mageuzi ya nchi hii eti kwa kupigwa mabomu ya machozi na kina Mahita. TLP ilipata umaarufu na viti vya ubunge at the expense of NCCR, hii inaitwa "transfer growth" kwa maana na waumini kutoka dhehebu hili kwenda lile na si kwamba ni ingizo jipya la waumini.

Nitampongeza Mrema siku zote kwa kazi aliyoifanya Home Affairs and for that he remains "the man of the hour" then!

Nikitazama Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) ya kesho naona CUF na CDM wakijipanga watatutoa.
 
Huyu Lyatonga anakumbukwa pia kwa kusuluhisha ndoa za watu kwani mke ilipotokea kapigwa na mmewe pengine kwa kosa lake(mke),Lyatonga hakuchelewa kumweka mme lupango.Vile vile anakumbukwa sana enzi zile akimkuta kiongozi fulani kakosa kwa jambo fulani au mtuumiwa wa wizi wa maprosoo,hakusita kumpa siku saba wakutane Moshi wakamalizane.Aisee jamaa kwa mchuzi halazi damu.
 
Huyu Mrema ni mtendaji. Sina shaka nae. Ngojeni muone maajabu atakayofanya katika jukumu hili jipya! Kichaa amepewa rungu!
 
mrema dume la mbegu. kote alikoenda alizaa mafanikio. sio mwanasiasa wa longolongo ila matendo tendo. mwansiasa pekee upinzani tanzania kupata asilimia kubwa za kura za urais kumzidi hata daktari wa wakatoliki wakati huo hakuna mitandao wala sms.

mrema dume la mbegu namkubali kikweli kweli. subirini huko serikali za mitaa hakutakalika.

hata chadema muone wivu mrema kuna matendo yanaonekana aliyofanya. mrema alipambana na baba wa taifa. daktari wenu kashindwa na mkwere ambaye hana kitu.

muhosni ningependa kukugongea senkis 1000 ila mafundi mitambo wetu wachoyo
 
Kwamba Mrema amekuwa na mchango mkubwa kwa nchi hii hilo liko dhahiri.
Ila nadhani Mrema anaweza tu kama ana madaraka makubwa hilo linadhihirishwa na utendaji wake pindi alipotolewa Home Affairs na kuwa waziri wa Kazi na Vijana. Mrema ni aina viongozi wanaitwa "One man show".
Kama kuna mtu ana kumbukumbu ya wazi anitajie jambo moja la maana alilofanya akiwa waziri wa Kazi.

.

umesahau alipofika wizara ya kazi akaanza kukamata wageni waliokuwa wanafanyakazi tz bila vibali. wizara iliyokuwa imelala ikaamka.
 
TAatizo la huyu mzee ni tabia yake ya kuua vyama vya siasa E.g the fall of NCCR MAGEUZI and TLP .
 
Mbona huyo ni double agent?

Not only that, mentally from beginning hana uwezo
Wa kutafakari mambo, he is the same old folk,
his era was over, he is far behind with time,
every time anaongelea vitu vya 1990's sijui
Kama anajua hata DOWANS exists, haendi
na wakati he is too static, elimu yake ndio
kikwazo. Hafai calas
 
Augustino Lyatonga MREMA, Nakuvulia kofia
Alianza siasa zamani sana, alichuja, sasa anang’ara tena
Muda wote ameheshimika, ni mpambanaji wa kikweli kweli dhidi ya udhalimu
Ni jasiri, mjanja, mvumilivu, mstaarabu
Lakini anapenda sana kuwa kiongozi wa juu kwenye taasisi yoyote atakayokuwemo.

Aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani, alifanya maajabu ya kupambana na ujambazi, kudhibiti wanaume wanaupiga wake zao, kuanzisha polisi jamii iliyofanikiwa sana. Alipambana na mafisadi kwa staili ya kuwapa siku saba watekeleze maagizo yake. Alisimamia maagizo na amri zake. Alifanikiwa kukusanya silaha za wizi na baadhi ya majambazi walitubu na kusamehewa. Wakati wa uongozi wake jeshi la polisi halikuwa lelemama.

Aliwahi kuwa waziri wa kazi. Utoro ulikoma, uchelewaji kazini ulikoma, na magari ya serikali yalipunguza safari za baada ya muda wa kazi. Alipatia vijana ajira na alitatua kero nyingi zilizokuwa zimeshindikana katika wizara hiyo.

Utendaji wake huu mzuri ulimfanya achukiwe na wanasiasa mafisadi. Walimuundia zengwe, na ilimlazimu kutoka serikalini na pia katika CCM mwaka 1995.

Alijiunga na NCCR ambayo ilikuwa haina umaarufu wowote, kwa masharti awe mwenyekiti wa taifa. Ndani ya muda mfupi NCCR ikawa na nguvu na ikawa tishio kwa serikali. Alipigwa mabomu ya machozi na polisi kuliko mwanasiasa yeyote aliye hai Tz, alinyanyaswa kwa namna nyingi. Lakini aliwezesha NCCR kupata wabunge kadhaa pamoja na kuonekana kuwa chama kikuu cha upinzani Tz kwa wakati ule.

Kwa kuwa NCCR nako kulikuwepo na mazagazaga ya mafisadi, alishindwa kuendelea kuwepo na akakimbilia TLP, pia kwa masharti kwamba yeye lazima awe mwenyekiti. Ghafula TLP ikafufuka na kuwa na heshima katika vyama vya upinzani. Kikajulikana, mrema akagombea ubunge Temeke akashinda.

Pamoja na umri kusogea, akachuja kwa muda kutokana na misuko suko ndani ya chama chake. Ameendelea kupambana na sasa amerudi kwenye chati. Alipotangaza kwamba anakwenda kugombea ubunge kule Vunjo kila mtu alidhani kuwa anazeeka vibaya. Ameshinda ubunge, na amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali za mitaa. Sasa ana uhakika wa maisha ya heshima zaidi.
Amerudi kwenye chati, anang’ara, na sasa anaheshimika tena
Na mimi, namvulia kofia na kutamani angeweza kuunganisha nguvu na Dr. Slaa (The Prezidaa)
.
Mtoa maada.
Tunakushuru sana.
umeonyesha uzalendo kwa kumkumbuka huyu mzee wetu.Hii maada imenigusa sana.Ubarikiwe ndugu.

Afande samwel
 
mrema dume la mbegu. kote alikoenda alizaa mafanikio. sio mwanasiasa wa longolongo ila matendo tendo. mwansiasa pekee upinzani tanzania kupata asilimia kubwa za kura za urais kumzidi hata daktari wa wakatoliki wakati huo hakuna mitandao wala sms.......

Benjamin Mkapa Chama Cha Mapinduzi 4,026,422 61.82%
Augustine Mrema National Convention for Construction and Reform–Mageuzi 1,808,616 27.77%
Ibrahim Lipumba Civic United Front 418,973 6.43%
John Cheyo United Democratic Party 258,734 3.97%
Invalid/blank votes 333,936 - Total 6,846,681 100%
Source: African Elections Database

Jakaya Mrisho Kikwete Chama Cha Mapinduzi 5,276,827 62.8%
Willibrod Peter Slaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo 2,271,942 27.1%
Ibrahim Haruna Lipumba Civic United Front 695,667 8.3%
Peter Mziray Kuga African Progressive Party of Tanzania 96,933 1.2%
Hashim Spunda Rungwe National Convention for Construction and Reform – Mageuzi 26,388 0.3%
Yahmi Nassoro Dovutwa United People's Democratic Party 13,176 0.2%
Muttamwega Bhatt Mgaywa Tanzania Labour Party 17,482 0.2%
Total Votes 8,398,415 100.00%
Source: Adam Carr's Election Archive

Tujadilini hoja ya Muhosni, ulevi uwe kando kidogo
 
mrema dume la mbegu. kote alikoenda alizaa mafanikio. sio mwanasiasa wa longolongo ila matendo tendo. ....... chadema muone wivu mrema kuna matendo yanaonekana aliyofanya. mrema alipambana na baba wa taifa. daktari wenu kashindwa na mkwere ambaye hana kitu...

JF inapokuwa na wachangiaji wa jinsi hii inanifanya nihisi tuko kwenye kilabu ya mataptapu.
Hivi kumbe mrema alimshinda JK 2005???

http://en.wikipedia.org/wiki/Jakaya_Mrisho_Kikwete
Jakaya Mrisho Kikwete Chama Cha Mapinduzi 9,123,952 80.28%
Ibrahim Lipumba Civic United Front 1,327,125 11.68%
Freeman Mbowe Chama cha Demokrasia na Maendeleo 668,756 5.88%
Augustine Mrema Tanzania Labour Party 84,901 0.75%
Sengondo Mvungi National Convention for Construction and Reform-Mageuzi 55,819 0.49%
Christopher Mtikila Democratic Party 31,083 0.27%
Emmanuel Makaidi National League for Democracy 21,574 0.19%
Anna Senkoro Progressive Party of Tanzania-Maendeleo 18,783 0.17%
Leonard Shayo Demokrasia Makini 17,070 0.15%
Paul Henry Kyara Sauti ya Umma 16,414 0.14%
Total Votes 11,365,477 100.00% Voter Turnout 72.4%
 
Kwa kuwa NCCR nako kulikuwepo na mazagazaga ya mafisadi, alishindwa kuendelea kuwepo na akakimbilia TLP, pia kwa masharti kwamba yeye lazima awe mwenyekiti. Ghafula TLP ikafufuka na kuwa na heshima katika vyama vya upinzani. Kikajulikana, mrema akagombea ubunge Temeke akashinda.

Muhosni ili kuweka rekodi sawa ni kwamba Mrema aligombea Temeke kwa tiketi ya NCCR baada ya Kihoyo kushindwa kesi iliyosimamiwa na kina Lamwai. Ni kutokea hapa mtu alokimbia umande tukamwita "Kihiyo".

Augustine Mrema NCCR-Mageuzi 54,840
Abdul Cisco Mtiro CCM 33,113
Hiza Tambwe CUF 3,324
Alec Che Mponda TPP 515
Mege Omar UMD 422
Samson Msambara CHADEMA 217
Legile Msonde UPDP 162
Ndembe Abdallah PONA 120
Rashid Mtuta NRA 114
Brighton Nsanya NLD 69
Shabaan Matembo UDP 67
Rachel Mutayoba TLP 62
Paul Mtema TADEA 54
 
Mrema mzee wa Kiraracha
Mrema mzee wa 7days orders
Mrema Rungu lao...
nakumbuka marehemu Remmy Ongalla alirekodi kibao akiwa UK kumsifia mzee huyu wa Vunjo ama kwa hakika mengi amefanya na ni mjanja sana...alipokuwa aameonja joto ya jiwe alijigeuza rangi akawa anafagilia JK,sasa tena rungu limerudi,ni mtu sahihi lakini asiye mahali sahihi!!
 
Augustine and Christopher they are only opportunistic idiot! Hivi Watu wenye uchungu na nchi hii kama Dr. Ndembwela Ngunangwa mna wakumbuka vizuri? mnafahamu mateso waliyo pata toka sisiemu chini ya uongozi wa Anna Semamba Makinda (Binamu yake) na walibaki kuwa watiifu kwa umma na sio ulamba viatu wa akina lytonga Mrema.Nendeni pale changanyikeni Mkamwone huyu mzee awaambie matatizo ya nchi hii na kilicho mpata kwaajili ya kupigania wananchi................
 
JF inapokuwa na wachangiaji wa jinsi hii inanifanya nihisi tuko kwenye kilabu ya mataptapu.
Hivi kumbe mrema alimshinda JK 2005???

http://en.wikipedia.org/wiki/Jakaya_Mrisho_Kikwete
Jakaya Mrisho Kikwete Chama Cha Mapinduzi 9,123,952 80.28%
Ibrahim Lipumba Civic United Front 1,327,125 11.68%
Freeman Mbowe Chama cha Demokrasia na Maendeleo 668,756 5.88%
Augustine Mrema Tanzania Labour Party 84,901 0.75%
Sengondo Mvungi National Convention for Construction and Reform-Mageuzi 55,819 0.49%
Christopher Mtikila Democratic Party 31,083 0.27%
Emmanuel Makaidi National League for Democracy 21,574 0.19%
Anna Senkoro Progressive Party of Tanzania-Maendeleo 18,783 0.17%
Leonard Shayo Demokrasia Makini 17,070 0.15%
Paul Henry Kyara Sauti ya Umma 16,414 0.14%
Total Votes 11,365,477 100.00% Voter Turnout 72.4%

Haukuielewa post ya Jenifa, aanasema Mrema alipambana na Nyerere, Dr. wenu Slaa alipambana na Mkwere! anafanya comparison. Ukirudia post yangu ya nyuma, ukiangalia mafanikio ya Mrema 1995 na slaa 2010 unaona ya Mrema yalikuwa na nguvu sana kulinga na wakati ule, nguvu ya CCM ikiwa na Nyerere, ugeni wa vyama vya upinzani, teknolojia ya mawasiliano!!!! sidhani kama hili linahitaji PhD kufanya analysis!
 
siku hizi watu wanasingizia foleni...mtu anaingia kazini saa 3 asubihi....hahahahhaha
 
siku hizi watu wanasingizia foleni...mtu anaingia kazini saa 3 asubihi....hahahahhaha

Enzi za Mrema wangekuwa wanaamka saa 11, wanaingia kazini saa 3, akisoma magazeti na umbea wa mjini saa 7 mchana, mambosi wakiwa kwenye vikao ndio ofisi iko huru watu wanatoka muda wanaotaka .......kufanya kazi serikalini kama unaipenda Tz inahitaji moyo sana-wavivu mpaka basi
 
Back
Top Bottom