Augustino Lyatonga MREMA, Namvulia Kofia

muhosni

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
1,108
152
Augustino Lyatonga MREMA, Nakuvulia kofia
Alianza siasa zamani sana, alichuja, sasa anang’ara tena
Muda wote ameheshimika, ni mpambanaji wa kikweli kweli dhidi ya udhalimu
Ni jasiri, mjanja, mvumilivu, mstaarabu
Lakini anapenda sana kuwa kiongozi wa juu kwenye taasisi yoyote atakayokuwemo.

Aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani, alifanya maajabu ya kupambana na ujambazi, kudhibiti wanaume wanaupiga wake zao, kuanzisha polisi jamii iliyofanikiwa sana. Alipambana na mafisadi kwa staili ya kuwapa siku saba watekeleze maagizo yake. Alisimamia maagizo na amri zake. Alifanikiwa kukusanya silaha za wizi na baadhi ya majambazi walitubu na kusamehewa. Wakati wa uongozi wake jeshi la polisi halikuwa lelemama.

Aliwahi kuwa waziri wa kazi. Utoro ulikoma, uchelewaji kazini ulikoma, na magari ya serikali yalipunguza safari za baada ya muda wa kazi. Alipatia vijana ajira na alitatua kero nyingi zilizokuwa zimeshindikana katika wizara hiyo.

Utendaji wake huu mzuri ulimfanya achukiwe na wanasiasa mafisadi. Walimuundia zengwe, na ilimlazimu kutoka serikalini na pia katika CCM mwaka 1995.

Alijiunga na NCCR ambayo ilikuwa haina umaarufu wowote, kwa masharti awe mwenyekiti wa taifa. Ndani ya muda mfupi NCCR ikawa na nguvu na ikawa tishio kwa serikali. Alipigwa mabomu ya machozi na polisi kuliko mwanasiasa yeyote aliye hai Tz, alinyanyaswa kwa namna nyingi. Lakini aliwezesha NCCR kupata wabunge kadhaa pamoja na kuonekana kuwa chama kikuu cha upinzani Tz kwa wakati ule.

Kwa kuwa NCCR nako kulikuwepo na mazagazaga ya mafisadi, alishindwa kuendelea kuwepo na akakimbilia TLP, pia kwa masharti kwamba yeye lazima awe mwenyekiti. Ghafula TLP ikafufuka na kuwa na heshima katika vyama vya upinzani. Kikajulikana, mrema akagombea ubunge Temeke akashinda.

Pamoja na umri kusogea, akachuja kwa muda kutokana na misuko suko ndani ya chama chake. Ameendelea kupambana na sasa amerudi kwenye chati. Alipotangaza kwamba anakwenda kugombea ubunge kule Vunjo kila mtu alidhani kuwa anazeeka vibaya. Ameshinda ubunge, na amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali za mitaa. Sasa ana uhakika wa maisha ya heshima zaidi.
Amerudi kwenye chati, anang’ara, na sasa anaheshimika tena
Na mimi, namvulia kofia na kutamani angeweza kuunganisha nguvu na Dr. Slaa (The Prezidaa)
 
You have said it all! he is the man! he is controversial and his propaganda tactics confuses people. He will remain on of the great leader to compete with CCM ever! alikichachafya CCM wakati muasisi wake yuko hai, aliwavuta wanafunzi wa sekondari na kuwa tishio in those days when teknolojia ya mawasiliano ilikuwa poor. Record yake kwa kipindi chake na hali ya kipindi kile haijafikiwa bado.

I am sorry to say watanzania wengi tumewarudisha nyuma wapambanaji kama hawa tumewadharau, tumewapa majina, tumewatupa na tumeshindwa kusoma historia , wengi huishia kuishi kama wananchi wanavyotaka, Mrema really amejitahidi kusimama kwenye games. his dictatorship attributes are best for Tanzania.

Mrema na Mtikila hawasahauliki kirahisi
 
Jambo moja nampendea huyu mzee ni pale umpe microphone, anaweza sana kujieleza na kuvutia wasikilizaji. Pengine alikuwa mtu wa kwanza tanzania hii kupambana na ufisadi kabla hata hatujajua kwamba kuna mafisadi wa kihindi wanaonyanya damu ya nji hii. Lakini sasa siku hizi amekuwa kibaraka wa mafisadi
 
Mbona huyo ni double agent?

Mlimtelekeza, mkamsahau, akawa hana namna nyingine zaidi ya kumsifu JK ili akashinde ubunge. Usisahau kwamba afya yake nayo ni gharama kui maintain

Usishangae kama hatutamjali Dr. Slaa pia akaishia kuwa double agent. Ni fundisho kwamba ni lazima tuwahudumie wapambanaji wa ukweli kama tunathamini mchango wao katika kulikomboa taifa hili
 
WABEROYA.......MREMA &MTIKILA kwangu ndo bado nawaona ni nuru na mwanga wa ukweli wa ukombozi wa taifa hili....michango yao katika taifa hili imeonekana
SIO WALE WANAOSIFIWA NA MEDIA HALI HAWANA MCHANGO WOWOTE WA KIMANTIKI KWA TAIFA
....SIMU YANGU NIMEWEKA RINGTONE YA MH.LYATONGA MREMA (mb)
 
Jambo moja nampendea huyu mzee ni pale umpe microphone, anaweza sana kujieleza na kuvutia wasikilizaji. Pengine alikuwa mtu wa kwanza tanzania hii kupambana na ufisadi kabla hata hatujajua kwamba kuna mafisadi wa kihindi wanaonyanya damu ya nji hii. Lakini sasa siku hizi amekuwa kibaraka wa mafisadi

mkuu huo ukibaraka unaweza kuwa wa kimkakati zaidi
 
If you scrutinise Mrema's ambitions vis-a-vis his fellow politicians in any undertaking, he is bluntly poor in thinking. Anaweza kuwa anaelewa mambo lakini uwezo wake wa ku-integrate mazingira yaliyopo ni mdogo. He is not remorseful.
 
Ninaweza kusema mafisadi wa CCM walimwangusha MREMA kifo kitakatifu. Hawa mafisadi sasa hivi tusiwape nafasi jamani wanatuletea mizengwe mingi ili wapate nafasi ya kufisadi nchi vizuri. Wakati huo huyu jamaa angepata sapota hatakama asingechukua nchi Tanzania tungekuwa tuko mbali sana. Yaani kila mtu alikuwa anawajibika ipasavyo. Ndio maana ninaagalia watu wanavyombeza lakini wanaombeza ni mafisadi. Lazima haki yake tumpe ya heshima kwa kweli apewe. Sasa hivi kama Kikwete angempa uwaziri kama alivyoomba mbona ungekuta Kikwete anapeta tu. Mnavyoona mrema akipata wafuasi ambao sio vigeugeu jamaa anamsimamo na anachapakazi. Inawezekana amekata tamaa baada ya watu kumzonga sana kuwa yeye ni CCM. Huku Moshi anavyowapeleka mchakamchaka huko halimashauri ya vunjo mungu anajua.
 
If you scrutinise Mrema's ambitions vis-a-vis his fellow politicians in any undertaking, he is bluntly poor in thinking. Anaweza kuwa anaelewa mambo lakini uwezo wake wa ku-integrate mazingira yaliyopo ni mdogo. He is not remorseful.

Unaweza ukawa uko sahihi kwa mtazamo wako, miaka ya 1994-1993 ungesema haya hakuna ambaye angekuelewa! sawa na leo ukinena vibaya kuhusu Slaa hakuna atakaye kuelewa, miaka 10 ijayo Slaa atakuwa na kusomeka kama unavyomuona Mrema leo!

kindly learn to appreciate foundation for the standing and magnificent structure!
 
I SAID THE TWO GUYS ARE UNIQUE IN THE HISTORY OF DEMOCRACY CUM OPPOSITION IN TANZANIA...ni watu wa daraja jingine...(MTIKILA&MREMA)
 
Anabaki kuwa mwanasiasa aliyepanda chati na kuchuja kwa kiwango cha kutia huruma. Amepigika kimaisha mpaka sisiem ilipomwonea huruma na kumpatia ubunge na uenyekiti wa kamati. Vinginevyo, mzee wa watu angekuwa choka mbaya. Angeanza hata kuongeza soli za viatu.
 
Anabaki kuwa mwanasiasa aliyepanda chati na kuchuja kwa kiwango cha kutia huruma. Amepigika kimaisha mpaka sisiem ilipomwonea huruma na kumpatia ubunge na uenyekiti wa kamati. Vinginevyo, mzee wa watu angekuwa choka mbaya. Angeanza hata kuongeza soli za viatu.

Mkuu, ikitokea kwa bahati mbaya ukawa kwenye mazishi ya mrema halafu ukaambiwa useme machache, je ungeyasema hayo?
 
Dah heri wewe uliemkumbuka, Enzi zake palikuwa hapatoshi mpaka leo namkumbuka kwani hizi polisi post huku mtaani ni zao lake. Mungu ampe uzima na amani.
 
Anabaki kuwa mwanasiasa aliyepanda chati na kuchuja kwa kiwango cha kutia huruma. Amepigika kimaisha mpaka sisiem ilipomwonea huruma na kumpatia ubunge na uenyekiti wa kamati. Vinginevyo, mzee wa watu angekuwa choka mbaya. Angeanza hata kuongeza soli za viatu.

wenye mtazamo huu ndio ambao hawawalipi wazee wa east african
hawawaenzi wanamichezo
hawakumbuki founders.....we have problem realy

atatokea mtu na kusema mwaka 2010 alitokea padri mmoja kugombea urais na akashindwa vibaya, at that time tutakuwa na wanasiasa wengine! kumbe uwepo wa hao wanasiasa unategemea sana na uwepo wa sasa wa akina Slaa, kama ambavyo ulivyosaidiwa na uwepo wa akina Mrema miaka hiyo

Niliwauliza swali watu fulani...je wangapi wako tayari leo hii kumlisha na kumtunza W.Slaa? kwa mahitaji yake yote? kama wafuasi wake hawako tayari siku akikaribia kufa kwa njaa aogope kurudi CCM? no way!!

tunarudisha nyuma upinzani kwa matendo yetu
 
Hii thread imenigusa sana, asante muhosni.

Hata huu upinzani pengine usingekuwa na mwamko wowote Kama siyo mrema kigogo wa ccm kujiuzulu uwaziri na kuja kuwasha moto upinzani.

Mrema akikaa mdahalo na maprofesa anawatoa nje, kwa sababu anaongea reality siyo nadharia.
Mrema kapigania ukombozi wa nchi hii kuliko mtu mwingine yoyote.
 
Back
Top Bottom