Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 297
Huu upuuzi wa polisi/ askari kanzu kunyanyasa wananchi unahitaji ukemewe na JK mwenyewe kwani ni kinyume kabisa na demokrasia. Ina maana Joe the Plumber wa USA itabidi aswekwe ndani Obama akishinda uraisi??
Atupwa selo kwa kumnyooshea mkono rais
Na Festo Polea, Mwananchi 10/20/2008
MLEMAVU wa mkono, Issaya Boniface Keraryo amekamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano baada ya kuibuka alikokaa na kusogea mbele ya halaiki kisha kusimama na kunyoosha mkono kuelekea juu kama mtu anayeashiria kutaka kuuliza swali huku akielekeza macho yake kwa Rais Jakaya Kikwete.
Mlemavu huyo alinyoosha mkono kwa muda wa dakika kama tatu na kulazimika askari kanzu waliokuwepo eneo hilo kumsogelea kwa lengo la kumtaka aeleze anachotaka kuuliza, ili kiwasilishwe meza kuu.
Baada ya kusogezwa pembeni askari kanzu hao walizidi kumsogelea na kumpeleka ndani ya jengo la Ukumbi wa Karimjee kisha kumuacha kwa muda hadi Rais na msafara wake walipoondoka ndipo askari hao walipomchukua na kuelekea naye Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano.
Akizungumza na Mwananchi, mlemavu huyo baada ya kuachiliwa na askari kanzu hao alisema alinyoosha mkono kwa lengo la kumtaka, Rais Kikwete kumtafutia wafadhili wa kumsaidia matatizo yake yanayomkabili.
"Nilitaka kumwambia Rais anisaidie kupata wafadhili kwani hali yangu ya afya hairuhusu kufanya kazi za kupata kipato na nyumba ninayoishi nitafukuzwa Ijumaa kwa kuwa sina fedha za kulipia pango," alisema Issaya na kuongeza
"Hata hivyo Rais Kikwete kipindi alipokuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa nilipata nafasi ya kukutana naye na aliniahidi kunitafutia wafadhili wa kunisaidia matatizo yangu, lakini hadi leo hakuna mafanikio yoyote," alisema Issaya na kutaka kusaidiwa na waandishi.
Mlemavu huyo kabla hajasimama na kuelekea mbele ya adhira, muda mrefu alikuwa amekaa pembeni jjirani na walipokuwa waandishi wa habari, akionekana akinyoosha mkono na kisha kuushusha bila kujulikana alikuwa na maana gani.
Baada ya muda kupita na kuona kuwa rais amemaliza hotuba yake na kitakachofuatia ni kuondoka bila kutoa dukuduku lake, akalazimika kusogea mbele ya watu na kunyoosha mkono kwa muda wa dakika kama tatu na kufanya watu kumshangaa kwa dakika hizo tatu hadi alipotolewa na askari hao.