Atumia Dola 10,000 Kufanya Upasuaji wa Kujigeuza Shetani

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
Mwanaume mmoja nchini Uingereza ametumia jumla ya dola 10,000 kufanya operesheni za kumfanya aonekane kama shetani kwa kujipandikiza mapembe kama ng'ombe, kuugawanya ulimi wake vipande viwili uwe kama wa nyoka, na kuyatengeneza meno yake yawe kama vampire. Hivi sasa yupo kwenye hatua za mwisho za kujipandikiza mkia na kujiweka kibiongo mgongoni.

655.jpg


654.jpg


Habari yake kamili gonga hapa http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2526646&&Cat=7
 
Je amewahi kumwona shetani? maana kitabu ninacho fahamu mimi Biblia takatifu,ina muelezea vizuri shetani alivyo kabla kuasi(hajawa shetani) ameanza kuitwa shetani baada ya kuasi.shetani ni kiumbe cha mwenyezi Mungu na alikuwa karibu sana na Mungu mwenyewe na alipewa mamlaka kubwa kabisa aliopewa na Mungu viumbe vingine vyote vilikuwa vinamueshimu sana na alikuwa ni kiumbe mzuri sana kitabu kinavyosema,na si vinginevyo naona jamaa yetu anajifurahisha tu,hayo mapesa mara mia angefanyia mambo mengine ya muhimu.
 
Watu wakishachanganyikiwa na huku wanavijisenti wanafanya mambo ya ajabu ajabu na ya kijinga. Ndio nini sasa sijui nanikamwambia Shetani yuko hivyo!!!
 
Jamaa kama huyu nilishakutana naye. Sijui kama na yeye amefanya ulimi wake hivyo (lazima itakuwa iliuma sana), lakini na yeye alikuwa na pembe. Jamaa alikuwa na demu wake wanapiga round town...hahaha. Kweli huku ndo kuchoka!!
 
pesa za dhulma huisha kwa dhulma,zinapotea kwa upuuzi kama huu.hata hivyo ni zake
 
Nadhani huyu hafahamu kuwa shetani ana sura nyingi sana ambazo huzitumia kwa mazingira tofauti tofauti. Na mara nyingi shetani hutokezea akiwa na sura ya handsome/beautful ili aweze kupokelewa na wanadamu bila hofu yoyote.
 
Mbona bado anaonekana mzuri tuu!
Huyu hajamfikia hata robo Masoud Sura mbaya japokuwa yeye hakutaka kujifananisha na shetani.

"Nlikiwepo":bolt:
 
Kwa hiyo inabidi atembeee ulimi nje ili watu waone ulimi wake ulivyogawanyika?
 
shetani angekua na sura hiyo mbona hata asingeogopeka.. sura kitumbua hiyo.. raia nyingine zina minyoo ya rangi ya pundamilia kichwani
 
Haya Wabongo igeni, Mashauzi yeye aliiga mwimbaji wa Spice Girls kwa kutoboa ulimi.
 
shetani anamuonekano mzuri sana kuliko tunavyo dhania. na niupumbavu kushabikia picha za shetani mweusi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom