Elections 2010 Atttention Wana-CHADEMA na Wapinzani kwa Ujumla.....!

jaxonwaziri

JF-Expert Member
Feb 17, 2010
375
195
Ni suala linalozidi kuwa wazi kuwa NEC inatangaza matokeo kule ambako CCM imeongoza. Kule wapinzani wanapoongoza hasa hasa CHADEMA hawatangazi! Na kuzuwia kusoma matokeo kwa majimbo kama Ubungo na Kawe wana-divert attention ya Taifa from kuhakiki na kusimamia kura za urais sehemu nyingine.

Wito wangu:

Kila Mgombea wa upinzani katika kila jimbo, asimamie ukusanyaji wa matokeo ya urais na ayawakilishe makao makuu ya Chadema ama CUF kwa majumuisho, huu si muda wa kuzubaa, by the tyme hawa wabunge wa CHADEMA ama CUF wanamaliza kushangilia ushindi wao wa ubunge na udiwani, CCM watakuwa wamemaliza kuchakachua kura za urais!
Kama tulivyofanya ubungo kwa ubunge, vivyo hivyo tufanye na urais nchi nzima jamani, tutakuja chekwa tukiwaachia hawa mafisadi!

Attn: Freeman Mbowe, Ndesamburo, Zitto Kabwe, Pro. Baregu, Dr Slaa, Sugu, Vicent Nyerere, Mpendazoe, John Shibuda, Halima Mdee, John Mnyika, Ezekiel Wenje, Peter Msigwa, Hiyness Kiwia,Meashack Opolukwa na wengineo.

Hata kama mbunge wa CHADEMA umeshindwa, simamia kura za urais na uzitume makao makuu kwa majumuisho!:thinking:
 
Mkuu unachosema ni kweli kabisa. CCM na NEC wanachofanya ni kuwafanya wananchi wapiganie matokeo ya Ubunge. Inasemekana ishu ya Mwanza ilibidi Mkuu mmoja Serikalini ambaye bado anaheshimika kutia shinikizo matokeo yatangazwe. Sasa hivi Kura za Urais zinachakachuliwa kama hawana akili nzuri. Sitashangaa JK kama atavunja rekodi ya 2005. TUMELIWA. Kinachoniuma hii hali tuliiona mapema sana lakini tukawa tunatumia NGUVU nyingi kujifanya HATUIONI na aliyejaribu kusema AMEIONA aliishia kuvurumishiwa matusi na kashfa. Imagine sasa hivi Lowassa, Rostam na 'fisadz' nyingine ukikutana nazo utaziangaliaje?
 
Sijui kama chadema wamekiona hicho kwani kwani wanatangaza maeneo ambayo CCM imeshinda kwanza ili wachakachue
 
Mawakala wa vituo vyote wa Chadema watakuwa na nakala ya matokeo ya Urais na hivyo nafikiri Chadema tayari wanamjumisho, na nafikiri wanaona si busara kuongelea hilo kwa sasa mpaka NEC watangaze ili Dr. Slaa akatae matokeo au akubali na kuwe na vigezo vya msingi vya kufanya hivyo.

Prof. Baregu na team yake sio kuwa hawayaoni yanayotendeka bali wanafanyia kazi plan A, B, C, ...
 
Nami nafikiri hivyo hivyo, ila ni vyema tu kukumbushana na kuweka msisitizo, bado nina imani ngoma haijaanza kuchezwa bado, tutashuhudia mengi safari hii.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom