BiMkubwa
JF-Expert Member
- Jan 9, 2007
- 529
- 97
Kuna vijana wako China wananieleza kuwa hawakuwa radhi kabisa kwenda huko kusoma ila walilazimishwa na wizara husika ili kumantain diplomatic relationship,
sasa kumbe masharti ni kuwa ukichaguliwa China means lazima uende huko bila kujali umechaguliwa sehemu gani.
Kuna ambao walipata UDSM,Mzmbe n.k,wahusika wa scholarships pale wizara ya elimu ya juu wanapitia lists za vyuo vyote,wakikuona tu huko unakuwa deleted na kukupeleka unakostahiki kwa mujibu wa taratibu zao.
Naweza kusema kuna matatizo mengi yanayomfanya mtu aone bora KUBINJUKA out kuliko kuendelea kusoma bongo;kwa mfano
(a)supplementary za ajabu/discontinuation
(b)matokeo si mazuri sana kiasi cha kutokuwa na uhakika wa kutopata chuo/mkopo
(c)kutoeleweka kwa bodi ya mkopo;mara itatoa 60% tu,mara vile.....wabaki mtu wa hali zetu za kimaskini kuyumbayumba.....hivyo kuongeza instabilty katika masomo.
(d)sometimes mazingira ya baaadhi ya courses(kama vile Computer) katika vyuo vyetu hayajatulia,nakumbuka mwaka 2005 vijana wengi sana waliikimbia hii kozi pale mlimani na kwenda India
Critique, Pole sana kwa misconstrued interpretation of my comments. Hata hivyo I was playing sarcasm of some of the reasons vijana wengine huzitumia kama basis ya wao kwenda kusoma nje.
Pia nawapa pole hao vijana ambao kwa mujibu wako walilazimishwa kwenda kusoma China. We need to look into this claim as well. Japokuwa ni vigumu kuamini hilo maana hata mwaka 1996 wakati serikali ilipoleta mkataba kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kulikuwepo na forms joint admissions board ambazo zilimtaka mwanafunzi aliechaguliwa zaidi ya vyuop viwili avijaze ili kuonyesha anataka kwenda wapi. Na uzuri wa hizo forms, zilikuwa zina include other East African universities as well.
Mara nyingi sisi wajazaji wa hizi forms tunadharau vipengele muhimu kama hizo. Na pia tabia ya procrastination ambayo imejikita miongoni mwetu husababisha wengi to fall into prey katika mikono ya administrators of these higher education offices. Watu wanaitwa kwenye orientation hawaendi kisa wanaogopa kuonekana wenye mshawsha wa shule. They come two weeks late, chuo imeshapitisha majina ya walio-report. Inaonekana mtu hajaripoti on time, they expect mtu ameenda kwingineko. Na taarfia kama hizi hufikia wizara husika mapema sana wakati wa orientation period. Sasa ikitokea bahati huyo mtu kachaguliwa China, basi wizara husika inamlazimu kwenda huko. I can take this scenario maana ilishawatokea kwa watu wawili ninaowafahamu na mmoja ilibidi aende India mwingine alienda Algeria. It does not sink in easily kuwa mtu unalazimishwa kwenda kusoma China kisa diplomatic ties, let us not justify some claims wakati kuna mechanisms zimewekwa kwa kusuluhisha matatizo kama hayo. Wapo wazazi wanawalazimisha watoto kwenda kusomea nje, mmoja wapo ni ndugu yangu wa karibu, alienda kusoma Urusi, maisha yakamshinda akarudi. Kama ushahidi upo wa watu kulazimishwa basi iwekwe bayana kama issues zingine humu JF tuone kama wahusika hawataadhibiwa.
Kuhusu kufeli, hilo lipo sehemu zote duniani na humu limezungumziwa mno na different influences zimetajwa hadi zile ambazo zipo personal. Swali je hakuna anayefaulu katika vyuo hivi? Kwa nini mtu ukimbie kusoma sehemu moja kwa sababu ya kufeli wakati hujasomea hapo ukajua kiini cha kufeli? Kuna somo moja la CT200 enzi hizo naona kwa sasa ina course code nyingine, wanafunzi walikuwa wanaiogopa hilo somo kama umande. wengi tulitishiwa kuwa tutafeli na hatutafaulu hilo somo. Wapo waliofeli na tupo tulio faulu. Tulipofika mwaka wa tatu tulifundishwa somo la education evaluation and measurements ndipo nikagundua wengi waliofeli ule mtihani walishindwa kwa sababu maswali mengi yalihusiana na application of theory.
Wenye kuelewa Bloom's taxonomy, watakubaliana na mimi. elimu yetu kuanzia sekondari kwenda chini na baadhi ya course za chuo (kutokana na udhaifu wa walimu wengine) imejikita katika ku-test "knowledge". Knowledge is the lowest level katika blooms taxonomy. Mwalimu ukitunga swali la "application" au "synthesis" wanafunzi wengi wanafeli somo ile mbaya na wanabaki kudai umetunga mtihani wa kukomoa. When in actual sense that is a level at least a student in a college should be able to attain. Sipendi kuingia katika mjadala wa supplementaries wala kufeli kwa wanafunzi.
Ila hao ndugu waliokwama huko Urusi au mahali popote duniani, kama walipewa scholarship za serikali kwenda huko na walikuwa wamechaguliwa kuingia katika chuo chochote Tanzania, THEY HAD A CHOICE! Wakumbuke if you make a choice you should be prepared for its consequence, let there be any. Kama wapo walioenda kwa sababu ndipo walipochaguliwa kwenda kusoma, wakumbuke maisha ni magumu popote maana hata UDSM wapo wanaolala na njaa but where there is a will there is a way.
Marekani pia shule ni ngumu na pengine ni ngumu kuliko jinsi watu wanavyofikiri. Scholarship ukiipata ni lumpsum humo humo ujitegemee pamoja na kulipia mahitaji yote ya shule na bado ununue vitabu maana ni lazima kama unataka kufaulu somo. Hawana makengeza ya kwamba unasubiri hela itumwe, wao wamekupa tarehe, wanategemea utafuta tarehe zao. Ukishindwa its none of their business. Bongo wanafunzi wanapewa hela za book allowance ambayo wameibatiza jina la "Simu allowance" halafu huyo akipata supplementary anasema ameonewa? Certain aspects just do not sit right.