Atorokwa na MKE siku moja baada ya harusi!!! Toa maoni

Eng. Smasher

JF-Expert Member
Nov 13, 2010
745
23
Habari zenu wana JF!!

Ni wiki 2 sasa zimepita baada ya kutokea kisa kitaani kwetu kilichokuwa kama movie flani hivi lakini ni cha kweli. Jamaa wa kitaani kwetu aliamua KUOA na kufuata taratibu zote; KUCHUMBIA,KUTOA MAHARI, SEND OFF na mwisho HARUSI iliyofaana sana.

Baada ya harusi MUME an MKE wakaenda HONEY MOON ili kukamilisha ndoa kwa lile tendo lenyewe lakini Bi HARUSI akagoma sababu alikuwa amechoka sana na mishe za Harusi toka asubuhi, Bw Harusi akawa mwelewa coz anajua mali ni ya kwake siku zote na kuvumilia hadi asbh.

Kumekucha Bi. Harusi akaenda kuoga then Bw. Harusi akafuatia kwenda bafuni, alipotoka kuoga akamkuta mkewe keshavaa na kupendeza. Akamwambia mumewe kuwa anaenda hapo supermarket kuchukua Dawa ya meno ndo HAKURUDI TENA.

Baada ya uchunguzi wa Usalama wa Taifa na police wakaenda kumpata Tabora na huyo mchumba mpya aliyemtorosha na kumuoa badala ya MUME wa ndoa!!! hivi sasa wamekamatwa na Police inasubiliwa Bw.Harusi aamue nini cha kufanya!!

Ingekuwa wewe ungeamua nini????!!!!! Toa maoni. Ahsanteni mimi nilikuwa best man kwenye SEND_OFF nmeombwa ushauri.
 
Hakulazimishwa tena ni mtoto wa MCHUNGAJI kanisa moja la TAG!!
Siku ya SEND-OFF mimi nilikuwa shahidi walikuwa wanaonesha wanapendana sana hakukuwa na tofauti yoyote!!
Mchungaji naye alisema aliwaita ofsini kwake b4 uchumba na kuwauliza mara nyingi sana kama kweli wameamua kuoana!!!
Walipeana mabusu mengi mbele ya mchungaji!!!!!!


Labda nikuulize swali moja, je huyo binti alilazimishwa kuolewa?
 
Mimi ningedai kurudishiwa garama za harusi basi huyo hawezi kuwa mke mwaminifutena na anaweza kukuuwa
 
inategemea na "kilichomkuta alipoenda supermarket kununua coligeti ya kusafishia meno"...inawezekana ALITEKWA NYARA NA KUPELEKWA KUSIKOJULIKANA NA WASIOJULIKANA ....

pia inawezekana bi-harusi ana matatizo ya akili thats y alifanya kituko cha karne ijayo kwa tanzania ila kwa wenetu kina kim kardashian ni simpo tuuu....
 
yawezekana demu alifanya hivi kulipiza kisasi labda kuna mistake jamaa alimfanyia wakiwa wachumba.
 
Correction: Ni wa kanisa la EAGT..I know the girl toka
mdogo, hakilazimishwa kabisa.

Hakulazimishwa tena ni mtoto wa MCHUNGAJI kanisa moja la TAG!!
Siku ya SEND-OFF mimi nilikuwa shahidi walikuwa wanaonesha wanapendana sana hakukuwa na tofauti yoyote!!
Mchungaji naye alisema aliwaita ofsini kwake b4 uchumba na kuwauliza mara nyingi sana kama kweli wameamua kuoana!!!
Walipeana mabusu mengi mbele ya mchungaji!!!!!!
 
ILa bibi harusi noma sana, asingesubiri kupanda madhabahuni.

Hata gaharama zikirudishwa, huyo mgoni wa pili atakuwa ameoa mke wa mtu!
 
Bibi harusi ni muuaji huyo!

Hata kama ana sababu...hawezi kumshawishi mtu kwamba ilikuwa fair kulipiza kisasi namna hiyo!

Jamaa apige moyo konde na kuanza mchakato upya....Sheria imsaidie kupata haki yake ya talaka. Vinginevyo ataendelea kujulikana kama mume halali wa huyo mwanamke!
 
Asee....
Hapa ni jinsi gani ya kumwacha huyo 'mke'.......
na kufutilia mbali hiyo 'ndoa'....
 
Back
Top Bottom