Kisoda2
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 2,475
- 745
Lucy kutoka Dodoma,ameolewa na mume mzuri tu na wamepata mtoto mmoja wa kiume umri wa miaka miwili sasa.
Katika ndoa yao wamehangaika kumtauta mtoto zaid ya miaka minne.
Ilifikia Lucy akamweleza mai husband wake wakapime kuona tatizo liko wapi ila mumewe aligoma na kujisifia yeye ni kidume cha mbegu,hivyo hana tatizo lolote katika hilo.Mumewe Lucy kutokana na tatizo hilo alianza kujitumbukiza katika ulevi wa kupindukia ili kufuta soo.
Lucy akajiiba mwenyewe na kwenda kupima nae akajikuta yupo safi kabisa.
Ndipo alipojaribu kuongea na mdogo wa mumewe ambaye ni pacha juu ya tatizo lilopo baina ya wanandoa hao.Mazungumzo hayo yalipelekea Lucy na pacha wa mumewe waingie katika kuivunja amri ya sita kwa siri,na Lucy akapata ujauzito ambao ndo umewapa huyo mtoto wa kiume(2yrs).
Mtoto alipopatikana mapenzi yamerudi kama mwanzo na jamaa anampenda mkwe na mtoto kuliko maelezo.
Tabu inakuja hapa sasa,pacha alietia mimba anamtaka shemeji yake waendelee na kula bata kwa kisingizio la sivyo atatoboa siri na kumdai mtoto wake.
Lucy amechanganyikiwa ataanzaje kumpa tena jamaa uroda,ama amweleze ukweli mumewe juu ya siri hiyo iliyo sirini.
Naomba kuwasilisha hoja tafadhali.