Atn waishabikia pombe

wagagagigikoko

Senior Member
Dec 5, 2010
163
49
Agape tv wanahubiri dini au wanafanya biashara ya pombe.
Kwanza naona wanajichanganya na wabaguzi kweli wale wako kibiashara zaidi, ukitaka kujua kuwa si watu wa huduma bali biashara, walikuwa wa kwanza kujitoa kwenye public dish bila kujiuliza waumini wangapi wa neno la mungu wamewapoteza kwa kuondoa matangazo kwenye ungo wa kawaida eti kukwepa watu wasione bure matangazo ya mpira.

Najiuliza kila siku hawa core ni mpira au dini maana matangazo yao ya ting yameegemea zaidi kwenya mpira kuliko hata dini.
Mbaya zaidi kwenye kwenye mahubiri yao wanakataa pombe wakati huo huo ni mawakala wa matangazo ya pombe heineken. Kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya filauni
 
Wameamua kutenganisha DINI na BIASHARA ya kaisari wanampa kaisari na ya Mungu wanampa Mungu kwani matangazo ya pombe huwa yanatokea wakati wa kipindi cha mahubili? au wakati wa kipindi cha mpira?
 
Wako kibiashara zaidi ndio maana mahubiri yao screen inajaa namba za akaunti
m pesa
T pesa
z pesa
nbc nk muda wote wa mahubiri yao
 
Nchi hii ina pepo mtaka hela kila anayeingia nchi hii anatafuta jinsi ya kuchuma atakuja kama mhubiri ataondoka ni mwizi au mfanyabiashara wa madawa ya kulevya.Atajifanya mtoto wa mkulima mcha mungu ataondoka akiwa mzulumu wa haki
 
Natetea kwa kufumba macho.....wanaotoa matangazo ya pombe ni UEFA na si ATN
 
Tusipakane mafuta hapa, kama umeamua kua unaeneza dini basi na iwe hivyo. Tusijifanye pombe wanatangaza UEFA. Je bruweries wakiwaomba hao Agape wakabandike bango la bia kwenye mlango wa kanisa lao watakubali?
 
Kwani pombe dhambi? bibilia inasema mpe kileo maskini asahau shida zake.

na quruani inatuambia peponi tutawekewa mito ya pombe aina zote.

wewe dini gani?
 
Kwani pombe dhambi? bibilia inasema mpe kileo maskini asahau shida zake.

na quruani inatuambia peponi tutawekewa mito ya pombe aina zote.

wewe dini gani?

Umenena mkuu ndiyo màana kila siku lazima nipate castle lager 2 then napiga sala nalala.
 
ila swala la matangazo ya pombe hapo wamechemka kama kweli wao ni wacha Mungu
 
Sitaki kuhukumu kwa habari ya tangazo la pombe lakini hili la tabiri usinde si sawa kwa wacha Mungu kuendesha michezo ya kubashiri.
 
Back
Top Bottom