ATN kuonyesha laivu 16 bora ya Mabingwa Ulaya

Mazengo

Member
Feb 9, 2011
30
17
satelite.jpg
agape.jpg

KITUO cha televisheni cha ATN ( Agape Television Network) kitaonyesha mechi zote 19 za Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kuanzia hatua ya raundi ya 16 itakayoanza Jumanne ijayo.

Kituo hicho ndicho chenye haki ya kipekee nchini katika kuonyesha mechi hizo za UEFA.

Akizungumza na Mwananchi jana, Meneja Mkuu wa Huduma za Maudhui wa kituo hicho, Steven Mshana alisema mechi hizo zitaonekana katika njia ya digital kuanzia Februari 14.

"Hivi sasa ATN imeanzisha vipindi vipya ili kufurahisha watazamaji wake, vipindi hivyo ni Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, Mapitio ya magazeti, vipindi vyenye radha ya Kiafrika, maigizo, vichekesho na sinema,"alisema Mshana.

Wiki ijayo ligi ya Mabingwa Barani Ulaya itaendelea, ambapo Jumanne, AC Milan itacheza dhidi ya Tottenham, Valencia itacheza dhidi ya Schalke na siku ya Jumatano Roma itacheza dhidi ya Shakhtar Donetsk wakati Arsenal itakuwa ikipambana na Barcelona, pia mechi zingine za hatua hiyo zitachezwa Februari 22 na 23.

Mshana alisema kituo hicho ambacho kinamilikiwa na Agape Life Church hivi sasa kimefunga mitambo yake ya kisasa Kisarawe,Tanga, Moshi,Arusha,Mwanza,Dodoma,Mbeya, Kigoma na Sumbawanga, hivyo watazamaji watarajie kuona picha zenye ubora wa juu.

Alisema kituo hicho hivi sasa kipo katika mchakato wa kuwa cha kawaida zaidi na kuanzisha televisheni nyingine ambayo itakuwa ikirusha vipindi vya kidini vya dini mbalimbali.

Alisema Agape Life Church ambalo makao yake makuu yapo Mbezi Beach, pia la matawi ya kanisa hilo sehemu mbalimbali mbalimbali nchini Tanzania.

Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya zinatarajiwa kuchezwa Mei 28 kwenye Uwanja wa Wembley nchini England, wakati zile za robo fainali zitachezwa Aprili 26,27 na Mei 3,4, ambapo hatua ya robo fainali itachezwa Aprili 5,6 na 12,13.

Klabu ya Inter Milan ya Italia ndiyo inayoshikilia ubingwa wa mashindano hayo, ilitwaa ubingwa baada ya kuichapa Bayern Munich ya Ujerumani kwa mabao 2-0.
source: ATN kuonyesha laivu 16 bora ya Mabingwa Ulaya
 
Back
Top Bottom