Athari za mgao tumeziona

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kuanzia kushuka thamani kwa baadhi ya blogu na tovuti zinazoendeshwa kutoka Tanzania ni kati ya mambo ambayo yanaonyesha matatizo ya mgao wa umeme nchini Tanzania ulivyoadhiri kwa kiasi kikubwa ufanyaji wa kazi wa baadhi ya tovuti .

Watu wengi wanaotembelea blogu hizi na tovuti hizi wanategemea umeme ili kuwasha computer zao ambazo ndio wanatumia kwenye shuguli za kila siku kwenye tovuti na blogu hizo , umeme unapokuwa hamna ina maana tovuti na blogu zinakosa watu wa kuangalia na kufanya updates za mara kwa mara kwahiyo hata kwenye rank zinashuka .

Takwimu hizi zinahusu idadi ya watu wanaotembelea tovuti na blogu hizo , idadi ya matangazo ambayo yamewekwa ( na idadi ya watu walioclick matangazo hayo ) , idadi ya watu waliosearch jambo Fulani au habari Fulani inayohusu mambo ya ndani ya nchi .

Ingawa watu wengi wamekuwa wakipuuza habari zinazohusiana na biashara za mtandao kwa nchi yetu , hii biashara kwa sasa inainuka sana na tunategemea kupata mafanikio kiasi kwa mwaka huu kutokana na wingi wa tovuti zilizoanzishwa na huduma ambazo ziko ndani ya tovuti hizo na blogu .

Tatizo linakuja tu kwenye upataji wa huduma hizi za mtandao haswa wa watu walio mbali na miji , gharama za kutumia huduma hizi pamoja na uelewa wa masuala mbalimbali yanayohusu mitandao , kwa kweli wengi hawajui ni nini haswa wanataka kufanya pindi anapopata mwanya wa kuangalia tovuti , mkulima hajui aangalie wapi , vile vile fundi radio hajui aangalie nini .

Kuna hitajika awareness ya hali ya juu haswa kwa vijana wanaokuwa sasa hivi kuhusu masuala mbalimbali ya mitandao na jinsi wanavyoweza kuitumia kwa manufaa zaidi na kwa kule vijijini ambapo kuna wakulima wengi wako wanahitaji sana mawasiliano haya kwa ajili ya mambo yao yanayohusu ukulima
 
Back
Top Bottom