Athari za kufanya mapenzi na watu usiowafahamu vizuri..........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Nimeisoma hii ya huyu serial killer kule Dar ambaye anawashughulikia watoto wa kike wa watu kwenye magesti na baadaye kuwanyonga...........it is so scary .........

SOURCE: HABARI LEO..............
 
Anayeua wanawake Dar es Salaam ashitukiwa

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 29th April 2011 @ 23:58 Imesomwa na watu: 1371; Jumla ya maoni: 4

WAKATI hofu ya matukio ya kuuawa kwa wanawake jijini Dar es Salaam ikitanda, jeshi la polisi limepokea taarifa kuhusiana na mtu anayedaiwa kuhusika na matukio hayo yanayofanyika katika nyumba za kulala wageni.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Kamanda Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa polisi imepata taarifa kuhusiana na mwanaume mweupe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, anayependelea kuvaa suruali aina ya Jeans, fulana nyeupe, raba na kofia kwamba ndiye mhusika wa matukio hayo ya mauaji.

"Inasemekana mtu huyu anapendelea kufuata wanawake weupe na hasa walioolewa na kisha huwapeleka katika nyumba tofauti za kulala hapa jijini na akishamaliza nia yake, huwaua," alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, matukio hayo ya mauaji yametokea katika maeneo ya Tandika, Mtoni kwa Aziz Ally, Buguruni kwa Mnyamani na Keko Machungwa.

Wanawake wameuawa baada ya kufanyiwa mchezo mchafu wa kuingiliwa kinyume cha maumbile na kisha kunyongwa mpaka kufa.

Kutokana na matukio hayo, Kamanda Kova ametoa onyo kwa wanawake kutokubali kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume wasiowafahamu.

Kamanda Kova amewakumbusha pia wahudumu wa mapokezi katika nyumba za kulala wageni kuhakikisha wanaandika majina na anuani kamili za mwanaume na mwanamke kabla ya kuingia katika chumba.

Amesema, Polisi kwa kushirikiana na jamii imeanza msako mkali kuwasaka watuhumiwa wote wanaojihusisha na matukio hayo na kuomba mtu yoyote mweye taarifa za watuhumiwa hao kutoa taarifa katika vituo vya polisi vilivyopo karibu au kutuma ujumbe mfupi katika namba 0783034224.

Hivi karibuni yaliripotiwa matukio ya mauaji ya wanawake watatu katika nyumba tatu tofauti za kulala wageni katika Manispaa ya Kinondoni na Temeke.

Polisi ilibaini kuwa wanawake hao wote waliouawa, walikuwa wamekwenda katika maeneo hayo kwa ajili ya kustarehe na wenza wao.
 
"Inasemekana mtu huyu anapendelea kufuata wanawake weupe na hasa walioolewa na kisha huwapeleka katika nyumba tofauti za kulala hapa jijini na akishamaliza nia yake, huwaua," alisema.

Mke wa mtu unakubali kutoxxxa na mwanaume ambaye si mume wako. SMH

Poleni mlioko kwenye ndoa.
 
Mke wa mtu unakubali kutoxxxa na mwanaume ambaye si mume wako. SMH

Poleni mlioko kwenye ndoa.

Kaka ashuakumu si matusi...lugha uliyotumia kama inachoma masikio vile....ingawa hoja yako inaweza ikawa ina ukweli kabisaaa
 
Kaka ashuakumu si matusi...lugha uliyotumia kama inachoma masikio vile....ingawa hoja yako inaweza ikawa ina ukweli kabisaaa

Hakuna cha ingawa hapo. Ni ukweli mtupu. Mwanamke umeolewa. Kisa cha kwenda kukazwa na mwanamme mwingine nini ihali bado uko kwenye ndoa?

Sielewi kwa nini watu wanaoana halafu wanaishia kutoka nje ya ndoa zao bila ridhaa za waume au wake zao. Ni bora ungebaki singo tu ufanye utakavyo.
 
mie bado siamini kuwa kuna mtu ataweza kuingia guest na mtu aliyekutana naye siku ya kwanza tu,huyo mtu anajulikana kwa hao victims pengine anaishi local,na ana mazoea nao......
 
Hakuna cha ingawa hapo. Ni ukweli mtupu. Mwanamke umeolewa. Kisa cha kwenda kukazwa na mwanamme mwingine nini ihali bado uko kwenye ndoa?

Sielewi kwa nini watu wanaoana halafu wanaishia kutoka nje ya ndoa zao bila ridhaa za waume au wake zao. Ni bora ungebaki singo tu ufanye utakavyo.
Are you single my dear friend? Tukikuchagua uwe rais lazima tutakuchagulia na first lady wa kukusindikiza ikulu...si afadhali uchague mwenyewe mmoja wa kufa na kuzikana hayo mengine yawe majaariwa??
 
Are you single my dear friend? Tukikuchagua uwe rais lazima tutakuchagulia na first lady wa kukusindikiza ikulu...si afadhali uchague mwenyewe mmoja wa kufa na kuzikana hayo mengine yawe majaariwa??

Hakuna cha ndoa siku hizi. Kila mtu msanii. Uaminifu na kuaminiana ni vitu vya kufikirika tu na siku zote huwaga ni siri ya mtu moyoni mwake mwenyewe. Kubali/ kataa huo ndo ukweli wenyewe.
 
hiyo ndio kuonesha kwamba maadili sikuhizi yamepungua sana, enzi zetu mke wa mtu ama mme wa mtu kuingia gesti na mtu mwingine ilikuwa ni ishu kwelikweli, sasa na huyo psychopath ameshapata iko alichokitaka uko gesti then why killing?
 
Mke wa mtu unakubali kutoxxxa na mwanaume ambaye si mume wako. SMH

Poleni mlioko kwenye ndoa.

kuwa na nidhamu, je unaweza kutamka neno hilo mbele ya wazazi wako? Hapa ni mkusanyiko wa watu wa rika tofauti, tusitumie maneno makali.
 
kuwa na nidhamu, je unaweza kutamka neno hilo mbele ya wazazi wako? Hapa ni mkusanyiko wa watu wa rika tofauti, tusitumie maneno makali.

Hakika naweza na nimeshawahi kulitumia bila athari zozote zile.
 
Kama hao wake za watu wanadanganyika kienyeji hivyo waume wengi kweli watagundua wake zao sio waaminifu!!Mwisho wa siku sidhani hata kama watakua na uchungu ...wataishia kufikiria ''i'm better off without her'' which is true maanaa ingekua anawaua taratibu kwa ngoma hata hao waume wangeishia udongoni kabla ya muda!!!

Haya wamama na wadada wa darSIsalama kuweni makini....msidanganyike!!!
 
wale wa one night stand watakoma mwaka huu, na kwa mtaji huu ukiona mwanaume mweupe ni kutoka mita tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom