ATCL Yasitisha Safari zake

Hii ndio tanzania, kila anayepewa cheo hafikirii maendeleo ya taifa bali yake binafsi
wameziua shule zetu nzuriii weruweru, kilakala, songea boys==wakaanzisha zao st marys, feza, alpha ...
Wakaua air tanzania ====wakaanzisha kina 540
wakaua usafiri wa reli =====wakaleta magari yao ya mizigo
wakaua uda ======wakaleta mabasi yao
wakawafutia madaktari wa serikali ajira ==== na kuongeza hospital binafsi za bei za kifisadi
wakampeleka ulimboka kumuua mabwepande====na kuwakumbatia mafisadi
dah
 
Mimi sina hisa PA. Unaposema shirika halikui sikuelewi kabisa. Leo hii PW itarusha ndege mara 19 kutokea Dar es Salaam. Tazama hapa : Airport Departures and Arrivals

Siyo kweli kabisa kuwa PW hawaruhusiwi kabisa kwenda international routes. Najua kuwa wanakwenda JHB na kwingineko.

Mimi nadhani ATCL wanamadhumuni ya kuua utalii Tanzania kuliko Kenya Airways. Kwani ATCL imesaidiaje?
 
ATCL wakikodi ndege nyingine wasiweke flag ya TZ wanaaibisha nchi na ni matusi kwa watanzania....this is another silly
 
Siyo lazima serikali yenyewe inunue hisa PW ina iruhusu mashirika yake kama NSSF, n.k. kununua hizo hisa kama yanataka kwani nielewavyo mimi ni kuwa yalikuwa tayari kununua hizo hisa lakini serikali iliyakataza. Mashirika/Serikali ikinunua hisa PW itapunguza unmiliki wa KQ kuwa chini ya 50%.
 
Katika hali isiyotarajiwa Shirika la Ndege Tanzania(ATCL) lenye ndege aina ya Boeing 735 lililokuwa linafanya safari kati ya Dar-Mwanza via K'njaro na Dar-Hahaya(Comoro) limesitisha safari zake hivi leo Asubuhi. Habari nilizozipata kwa jamaa yangu aliyekuwa asafili na ndege hiyo leo asubuhi ni kuwa abiria wote wa ATCL waliokata ticket kwenda Mwanza "wamefaulishwa" ktk ndege ya 540.Com aina ya CRJ.

Kwa habari ya chini ya kapeti ni kuwa ATCL imeshindwa kulipa malipo ya kukodi kwa kampuni ya AEROVISTA ilipoikodi Ndege hiyo,kampuni husika imeizuia ndege yake kuruka mpaka hapo itakapolipwa malimbikizo ya madeni yote na ATCL. Hii inatokea siku moja baada ya Wizara ya Uchukuzi kuwasilisha Bajeti yake ktk Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Boeing hawajawahi kutengeneza ndege aina hii tangu kiwanda kianze.
 
mtotowamjini,kuna habari nyingine imejitokeza hapo kwamba serikali imeikoidisha kwenda Ethiopia. Ukweli utajulikana. Kwa msaada kwako abiria wengi sasa hivi wanapendelea kutumia hiyo ndege kwa njia zilizotajwa hapo juu. Hii ni fahari yetu,kuna siku itafufuka. Zamani ukiwa nje ya Tanzania ukaona twiga anatua ama anaruka unajisikia fahari sana. Enzi hiyo itarudi!


Ni mawazo ya kimasikini sana kujisifia na kandege kamoja, tena ka kukodisha! Fikiria Tanzania ingekuwaje kama haya mashirika mengine yanayo rusha ndege zao nchini mwetu yasingekuwepo.

Nimeijua ATCL kwa miaka mingi sana, toka inazaliwa kutoka EAA. Sijawahi kuifurahia kabisa. Sikuipenda kabisa kwani safari zilikuwa hazitabiliki. Kuna wakati ATC ilikuwa inaitwa Any Time Cancellation, halafu walikuwa wanafanya hivyo bila taarifa yeyote kwa wateja. Wakati wa shida wafanyakazi wa ATC waligeuza ndege za ATC kuwa meli yao ya kuleta mizigo kutoka nchi za nje kama DUBAI nk kwa ajili ya kulangua Tanzania. Ilikuwa ukiingia ndani ya ndege unakuta 'cabin compartments' nyingi zimejaa mizigo ya wafanyakazi na wasafiri inabidi kuweka mizigo 'under the seats'.
 
Bajeti imepitishwa jana wafanye hima walipe deni la watu....:eek2:
 
Omujubi!

Uko sahihi tatizo ni Serikali na haswa huyo Mwakyembe anaota ndoto ya kuwa na National Carrier . Yeye na Dhaifu is another bunch of nicompoops . Kenya hawana national carrier Kenye Airways inayorusha ndege karibu duniani kote ni a Private Company na serikali ya Kenya inazo hisa only 23% .

It's quite simple Serikali inunue hisa PA na kutumia hiyo opportunity. Huwezi kodisha ndege moja halafu ukategemea ikutoe. Tulikuwa na Air Tanzania ikauwawa na Watanzania na hakuna aliyepelekwa Mahakamani but the dream goes on and on.

Wakati Dhaifu anazindua Hanger ya PA alipewa hiyo offer na Shirima lakini akitokea Mwakyembe aka sema dhamira ya kufufua ATC iko pale pale. Nadhani Mwakyembe ni Mkristo na anajua from the bottom of his heartbeat that hakuna kitu kilichowahi kufa kikafufuka ila yasemekana Yesu Kristo alifufuka I can't dispute that kwani wengi wanaamini.

Kufufua ATC under CCM is an impossible mission kwani it's still the same level. Just like watu Fulani wanafikiria kufufua JKT?

Simple solution lets jump at the offer ya PA tununue hisa tusonge mbele! Hizi ngonjera za kuanzisha Chuo cha air hostess is another failed CCM conception.

Mkuu hapo kwenye RED, ni kwamba Ford ilikufa mara tatu na kufufuka na sasa hivi ni moja ya makampuni makubwa ya magari. Although I dont see this happening kwa ATCL.
 
Bad news but it is OK...tumeishazoea.... Upande mwingine yaweza kuwa good news kwa Precision Air wanaolihujumu shirika letu la ndege.... Yote tisa ipo siku yataisha haya.
 
Kama kweli serikali inahitaji kuwa na shirika la ndege ni wanini isilivunje hili shirika la ATCL na kutumia ruzuku (ya mwaka mmoja tu) inayopelekwa ATCL kwa sasa kununua shares za Precision Air na kulifanya liwe ndio flagbearer wa nchi na kuliacha liendeshwe kibiashara. Hata kamati fisadi za bunge zisiruhusiwe kuingiza mikono yake badala yake shirika liachiwe bodi imara ya wakurugenzi watakaoteuliwa kwa sifa zao ili waliendeshe shirika kwa faida.

Sababu: Serikali ya Tanzania haiwezi kusimamia wala kuendesha biashara kwa faida wala shughuli nyingine yoyote kwa ufanisi.

Ushahidi: Mamia ya mashirika ya umma yaliyokufa kwa kushindwa kujiendesha kibiashara na hata serikali yenyewe imeshindwa kujiendesha na kutoa huduma muhimu kwa wananchi kama elimu, afya, maji. Kwa sasa iko ICU inategemea dripu za mikopo na misaada toka kwa wafadhili na wahisani wengine ile iendelee kuwepo.

Ni mtazamo wangu tu.
 
  • Thanks
Reactions: KVM
This thing was breathing on life support for a long time,now its about time it dies and saves us from all unnecessary outlays.

Dude ilikuwa ukipanda unalisikia springs zinasuguana kama mkweche, bora waachane nalo, lingeweza kuleta ajali.
 
ngoja ingine inakuja,na ile mipango kabambe ya mwakyembe!
 
Tanzania;sasa bado hawajala hela za bima baada ya ajali kigoma:hate this
 
yaani nilisema mwakyembe hataweza wizara hii...anatapatapa tu
 
Back
Top Bottom