ATCL to write off the crashed plane!?

Bila shaka hiyo ndege (ambayo ni ya kukodi) ilikuwa na bima ama sivyo ATC wangeondolewa operating licence na kufutwa kwenye orodha ya IATA. Jambo kubwa hapa kama ilivyogusiwa na wengine ni kwa Serikali kuacha mzaha na kuamua kama kweli tuwe na shirika la ndege la umma au la. Utaona nchi kama Ethiopia ambao hawatufikii kiuchumi wamedhamiria kwa dhati kabisha kufanya biashara ya usafiri wa ndege - kwa kujituma na kujitolea hasa. Ni biashara ngumu sana na inayohitaji umakini na uzalendo wa hali ya juu kwelikweli. Hakuna mtu anayepewa nafasi ya kufanya hata chembe ya uhuni katika hilo - udhibiti ni zaidi ya asilimia 100.

Kwa uswahili tulionao sisi katika mambo yote ya msingi ni bora tukakaa kando na kuwakabidhi haki zetu za anga (freedoms of the air) wanaoweza kuifanya kazi hiyo nchini kwetu tukaambulia angalau royalties. Na tatizo letu kubwa hata tukileta wawekezaji/waendeshaji ama tunaishia kuambulia wababaishaji au tunawafanya hata walio makini waanze kukiuka viwango - kwa ajili tu ya kutaka pasenti holela na kupuuza udhibiti (regulation).
 
Naomba nifafanue kidogo. Ndege iliyopata ajali Mwanza ni ndege ya kukodi (leased aircraft).Sio mali ya ATCL. La hasha. Ndege hiyo ina bima(insurance ) ya kiwango fulani. Ajali ilipotokea mwenye ndege na watu wa bima wamekwenda Mwanza na kuona jinsi ndege ilivyoharibika. Baada ya assesment inaonekana gharama ya kuitengeneza hiyo ndege inakuwa kubwa sana kuliko gharama ya bima (insured value) ya ndege. Gharama inakuwa kubwa kwa sababu imeharibikia Mwanza ambako hakuna vifaa na karakana (kama DAR) hivyo mobilazation ya vifaa inakuwa ya juu sana.

Baada ya kutafakari mwenye ndege na watu wa bima (sio ATCL) wamekubaliana mwenye ndege alipwe bima yake na hivyo ndege itabaki mikononi mwa kampuni ya Bima (Insurance company) ambayo itajua jinsi ya kufanya lakini sana sana ile ndege itauzwa kama scrap kwa ajili ya spea kwa kutangaza tender. This has nothing to do with ATCL. Ni jambo la kwaida sana kwenye mambo ya ndege. ATCL inaweza kukodi ndege nyingine au kununua. Hii ndio maana ya Bima.
Well said Byasel. Kama mkataba wa ATCL na mkodishaji ulikuwa mzuri, basi ATCL wanatakiwa kupatiwa ndege nyingine ASAP au kulipwa fidia ya kukosa uzalishaji. Lakini hili hatujalisikia likinenwa pengine halipo.
 
Well said Byasel. Kama mkataba wa ATCL na mkodishaji ulikuwa mzuri, basi ATCL wanatakiwa kupatiwa ndege nyingine ASAP au kulipwa fidia ya kukosa uzalishaji. Lakini hili hatujalisikia likinenwa pengine halipo.

Maana kwa mawazo yako, ajali ilisababishwa na ubovu wa ndege au?
 
Injinia,
How will they bring it from Mwanza to Shaaban Robert Street?

Mh, good question S ni S. This Injinia had not thought about it.

Hmm....if only we had breakdown Landrover airplanes to tow it!!

I suppose they can disassemble it, as someone suggested. But that would take another year - mpaka iundiwe kamati ati!!
 
Do weed need STATUS? ATCL inaleta watalii wangapi nchini? ATCL inahudumia watanzania wangapi nchini?ATC inashindania wateja na Precision.Ile package waliyopewa kunuanua mindege kwa nn wasingepewa TRL shirika amablo lina weza kuwa na poteantial Kubwa kwa uchumi na influence yetu afrika mashariki.

If i was a minister/PS wa miundombinu ningeondoa headache ya ATCL kichwani mwangu kwa kuiza na kupeleka akili na effort zangu zote kufufua na kuimarisha Reli.

Inawezekana ukweli huu haupendezi masikioni lakini ndio ukweli utakaotufikisha tunakoota kufika.
Mtazamaji,

Mimi na wewe tunaweza tukawa na mtazamo tofauti na Viongozi wa nchi kuhusu uwepo wa shirika hili. Lakini, ukimwuliza ghafla Mr. Presida au Mh. PM, atakuambia "...unajua Kenya wana shirika lao, Uganda wanalo, Rwanda wanalo, Msumbiji wanalo, Ethipoia wanalo; kwahiyo ni muhimu na sie tukawa na letu"
Ni STATUS tu hiyo, amini usiamini. Hakuna sababu nyingine.
 
Back
Top Bottom