ATCL saga

Watanzania mlivyo wapumbavu nawaona live kuwa umaskinii huu wa nchi yetu sio bahati mbaya kabisa. Ni sababu ya bongolala. Mnadharau credentials za Paul Chizi katika mambo ya aviation?? Nahisi mkija kuanzisha kijikampuni cha computer halafu Bill Gates na Michael S Dell waonyeshe nia ya kuajiriwa mtataka wafanyiwe interview kwanza kufuata sheria ya kuwashindanisha na wengine ili waajiriwe kihalali wakati hao ndio nguli wa hiyo sekta, na kama Dell akitokea kuajiriwa bila kufuata sheria mtamuondoa na kuweka binamu zenu...

utaratibi ni utaratibu haujalishi unguli, kinachotakiwa ni policy na procedure kufuatwa.
 
Muongo mkubwa wee.... Imagine u hear such a cooked story like this, sweeted with liars carefully formulated as if ur ab aviation expert.... of which ur not..... I am experienced flyer.... Leo Alhamis Waziri Mwakyembe kaja ATCL Terminal One kuongea na wafanyakazi woote, i was there... KAWEKA KILA KITU PUBLIC... Mpaka wafanyakazi tumeshangaaa.... Uozo ulioko ATC....
One example ... Hiii ndege iliyokodiwa....
1: hata kopi ya mkataba AG hana
2: Wizara haina Mkataba
3: ATCL walipewa waoperate 3 months free... Kumbe mkataba unaitaka ATCL wailipie hiyo ndege insurance ya miaka kadhaa huko nyuma.... Kumbe ndege inadaiwa billions of Tsh na insurance huko itokako....
Pili Katibu mkuu aliagiza ndege isiruke na wafanyakazi wa ATCL kwenda Mwanza na kurudi, eti wanasherehekea, imagine ndege inaruka free na wafanyakazi Dar - Mwanza - Dar.... UNASHEREHEKEA NINI? Chizi alikaidi amri ya Katibu mkuu....
Pili... Uteuzi wa Chizi hukufuata taratibu na kanuni za utumishi wa umma.... This does not mean or inaondoa kwamba Chizi sio aviator mzuri....
Kikao cha leo kila mmoja alishangaa na kubaki kumshangilia Mwakyembe....
So stop coming here with story ya mtu wa Stanbic....
Stanbic.... Kazi yao ni finance tu... Si ndege, period...

Asante kwa updates mdau, nadhani mleta mada ametumwa na chizi
 
Wadau,

Nasikitika kwamba badala ya mimi kushangilia maamuzi ya waziri, kwa hili naomba nionyeshe masikitiko yangu makubwa hasa kwa mtu muelewa kama Dr Mwakyembe. Alichokifanya mh huyu ndo yale yale ambayo yalilalamikiwa nab w Lowasa wakati ule, maamuzi ambayo hayatokani na utafiti bali mujungu na kutafuta kuonekana kutenda hata kama unafanya madudu.

  1. ATCL kwa mara ya kwanza mefanikiwa kupata ndege ya kukodi kwa bei chini ya wastani wa bei ya soko (block hour rate below market standard) ambayo kama nakumbuka vema ni USD 1,700 wakati soko liko USD 2,400
  2. Kwenye mkataba huu ambao wakubwa wanasikitika kupigwa chenga ya mkataba ambayo kwa kawaida ndiyo sehemu ya ulaji wa wakubwa wetu, umeondoa yale mazoea ya kulipa kishika uchumba (down/advance payment) ambayo nayo huwa inachakachuliwa na wakubwa. Badala yake hii ya sasa ni kulipa kutokana na matumizi based on block hour usage
  3. Market penetration yao ambayo return ticket ya KIA ni tzs 199k (against 340k ya PW) na Mwanza tzs 199k (tzs 420 ya PW) ambayo kwa wale wanaotumiwa na wazito wa PW, wameona ATCL ni threat at least kwa hizo routes mbili.
  4. Majungu kwamba ATCL management amepokea hela nyingi na kuzifuja during month of May ambapo mpaka waziri na naibu wake walinitembelea hapa J3 asubuhi na kuwapa ukweli bayana (as we are the only banker of ATCL) and yet wamekwenda kufanyia kazi fitna na mujungu
  5. Paul Chizi ambaye alikuwa sourced from Community Air, being of less than 5 Tanzanians who pocess an MBA in Aviation, leo mnasema vifungu vilikiukwa na ukweli unafahamika mtendaji mkuu wa wizara ni katibu mkuu…So, wa kuwajibika ni Eng Chambo ambaye ndiye alikuwepo Aug last year wakati Paul Chizi anapewa nafasi ya kukaimu u-CEO wa ATCL.
  6. ATCL kulaumiwa kulipa deni la Ultimate Security above $0.9m wakati kesi iliamuliwa na mahakama ya biashara Mar 2011 ambapo uongozi huu haukuwepo madarakani, ATCL hakuwa na pesa na hivyo serikali kupitia barua ya Eng Chambo kucommit kulipa deni ambalo hata hivyo kila wakiandikiwa barua wanapotezea kwa zaidi ya mwaka. Matokeo last week ATCL amepata mpunga wa malipo ya bima ya ndege iliyotembelea tumbo Kigoma, mdeni akawahi mahakamani na kuleta zuio la hela benki (garnishee nisi) na tumezuia pesa ambapo ATCL amerejea mahakamani kuomba kesi itizamwe upya na kukubaliana payment plan, yet wanasemwa kuwa wametumbua pesa.
Tunabaki tunakurupuka kama kawaida yetu na kuishia kuwaonyesha watanzania kwamba kukosoa kumbe ni rahisi kuliko kuongoza. Tunaishi kwa majungu na utafutaji wa njia za mkato wa kupata umaarufu kwa wananchi.

Natamani kama ningeyasema haya ana kwa ana badala ya kuyaandika. Lakini naona mazingira hayaruhusu. Binafsi nimefuatilia hili sakata toka early last week, nimeketi na watendaji wakuu wa ATCL, Wizara na mpaka juzi waziri na naibu wake. Ajabu sana, narudia tena ajabu sana uvumi kwamba nia ni kumg’oa Chizi ili awekwe ndugu wa mh toka nyumbani kwetu Mbeya nilikuwa nayo toka 28 May 2012. Mwisho wa siku ndicho kilichotokea.

Stanbic ndo sole banker wa ATCL, sasa mtu anaposema kuna fedha zimefunjwa wakati ATCL hajawahi kuwa na hela ndani ukiachilia ka-OD kadogo ambako tuliwapa ili waweze kuwa wanalipia mafuta PUMA Energy, maelekezo ya kulipa tumekuwa tunafanya wenyewe hapa ndani, pesa pekee walopata mwezi May ni ya mshahara toka serikalini few millions. Then mtu anasema wamefuja?!?

Unless mtu anambie kuna pesa ATCL alikuwa anapelekewa cash na serikali pale ofisini kwao, kitu ambacho ni non sense.Wadau,

==> Si maneno yangu wana jamvi, bali ni maneno ya mdau wa karibu wa Stanbic<===

Kiko wapi??wezi wachomwe moto tu...dawa ya mwizi ni moto pekee.
 
Ma bankers wa bongo hao. Upande mmoja nakuwa kama siwezi kuamini kwamba banker anayeijua kazi yake anaweza kuandika hivi.

Upande mwingine bongo anything is possible, why, Kikwete kawa rais.

ha ha..nimeipenda sababu yako ya kwanini 'anything is possible' bongo..

Huyu banker atakuwa ni moron mmoja yuko involved kwenye payment authorization hierachy ya stanbic kwa ivo anajaribu kufunika kombe..au he is only an overly talkative employee trying to brag around his unconscious incompetence..either way,he remains a moron..an ignorable moron.
 
I know Paul Chizi tangu alipokuwa Engineering Dept ya ATCL kabla haijafa na alipokuwa Manager wa ATCL Jo'rburg. Lakini sishangai Mwakyembe kumwondoa Chizi, nina uhakika Mwakyembe amevutwa na hulka za kikabila tu. Sijui aliyeteuliwa na Mwakyembe, bila shaka ni M-Kyela mwenzake au mtu kutoka Mbeya.

Paul chizi is full grown in aviation industry from engineering to marketing to operation....It is too bad that this country is running on its own bullshit!

effectiveness ndugu yangu ndiyo cha msingi kwenye kazi...mimi nafanya kazi na mtu ana digrii tatu za field tofauti zenye maana tu..lakini ukikaa naye unatamani umpige vibao kwa reasoning yake ilivyo hovyo..effectiveness mkuu..haya ya kusema unamjua fulani toka lini..watu tulikuwa tunamjua kikwete toka akiwa waziri wa mambo ya nje,ccm,daruso..halafu ametufikisha wapi.
 
Kwa heshima na taadhima mkuu na wewe fanya utafiti kwanza, chizi hakuondolewa kwa sababu ya kufuja hela ! jamani hata wewe unatupotosha, Chizi ameondolewa kwa sababu nyingine kabisa.wasiliana na wahusika !
 
OK. Well said. Lakini vipi kuhusu waliomuajiri Paul Chizi, including Katibu Mkuu ambaye ndiye mtendaji wa wizara. Hatujasikia hatua zinazochukuliwa juu yao.

hayo ni maneno yako. Mwakyembe alicho sema ni kwamba "ajira yake haikufuata taratibu za kuajiriwa" anaweza akawa amefanya mengi lakini mwakyembe anacho taka ni kufuatwa kwa taratibu za ajira.
Unaweza ukawa unajua kuendesha gali vizuri lakini kama hauna leseni trafiki lazima akukamate.[/QUOTE]
 
Whatever the case it's, ukweli utabaki pale pale kuwa Mwakyembe ni mtu wa fitna na pia ni mkabila mkubwa!
 
Mwakyembe: Nimemng'oa bosi ATCL kwa ufisadi Send to a friend
Thursday, 07 June 2012 19:54
0digg

atcl-mwakyembe.jpg
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza katika mkutano na na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) uliofanyika Dar es Salaam jana. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi mpya wa ATCL, Milton Lazaro na Mkurugenzi Rasilimali Watu, Judith Ndaba. Picha na Rafael Lubava

ASEMA WANAOUNUNG'UNIKA WAKO HURU KUJIONDOKA
Fidelis Butahe
SIKU nne baada ya kung'olewa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameamua kuanika tuhuma za ufisadi zinazodaiwa kufanywa na kigogo huyo.Miongoni mwa tuhuma hizo ni kuingia mkataba wa kununua ndege bila kumhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na kununua sare 15 za watumishi wa ndege kwa dola 50,000 za Marekani.

Juni 5, Dk Mwakyembe alitengua uteuzi wa Chizi na kumteua rubani wa muda mrefu, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi hiyo, akisema uteuzi ulikiuka Sheria za Utumishi wa Umma.

Mbali na kutengua uteuzi huo, pia alitangaza kuwasimamisha kazi vigogo wengine wanne wa shirika hilo, hatua ambayo ilianza kuibua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi kwamba hatua hiyo ilitokana na majungu na ukabila.

Waliosimamishwa kazi na Dk Mwakyembe ni Kaimu Mkurungenzi wa Uhandisi, Jonh Ringo, Mwanasheria ,Amini Mziray, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Justus Bashara na Josephat Kagirwa ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Biashara.

Jana, waziri huyo wa uchukuzi aliamua kufafanua tuhuma moja hadi nyingine zinazomhusu kigogo huyo na wenzake na kusema, mbali ya tuhuma za Chizi, wakurugenzi wawili wa shirika hilo walikwenda kushonesha sare 15 za wahudumu wa ndege nchini China kwa gharama ya dola 50,000 za Marekani (karibu Sh80 milioni).

Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika Uwanja wa Ndege wa zamani (Terminal One) jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe alisema kutokana na hali hiyo, ameagiza kujazwa kwa nafasi zilizo wazi na kuwaonya watakaozichukua, kuhakikisha wanachapa kazi ili ATCL ipige hatua na kama wakishindwa watakuwa wamejiondoa wenyewe.

Dk Mwakyembe alitoa miezi mitatu kwa shirika hilo kuanza kujiendesha kwa faida, ikiwa ni pamoja na kupata fedha za kuwalipa wafanyakazi wake.

"Kwa kasi niliyoanza nayo watu kama Chizi ni lazima wakae pembeni, ni mtaalam katika masuala haya, lakini tatizo lake hakuwa muwazi," alisema Dk Mwakyembe.Chizi hakupatikana jana kuzungumzia tuhuma hizo, wakati wote Mwananchi ilipompigia simu yake ya kiganjani, ilikuwa imezimwa.

Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, alitumia Saa 1:17 kuzungumza na wafanyakazi hao na kufafanua kwamba Serikali imechoka kutoa fedha za kuliendesha shirika hilo, akihoji iweje mashirika mengine ya ndege yaweze kusimama yenyewe, lakini ATCL iishindwe.

"Tunaipenda ATCL iendelee na tunachukua hatua za kila aina ila tukiona tunashindwa tutaachana nalo ili, fedha zinazotumika hivi sasa zipelekwe kufanyia mambo mengine ya maendeleo," alisema Dk Mwakyembe.

Tuhuma
Akichambua tuhuma moja hadi nyingine za ukiukwaji wa sheria na taratibu, Dk Mwakyembe alianza kwa kutolea mfano mkataba tata baina ya shirika hilo na Air Bus ambao umeifanya nchi kudaiwa Sh69 bilioni na kusisitiza kuwa, kutokana na hali hiyo Serikali haikuwa tayari kufumbia macho mambo mengine ya ovyo yaendelea katika shirika hilo.

Alisema wafanyakazi wote wa ATCL ambao wananung'unika baada ya kutengua uteuzi wa Chizi wako huru kuondoka katika shirika hilo, huku akionya atawatimua wengi watakaofanya mambo kinyume.

"Nilipoteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi siku chache baadaye nilisikia ATCL wanaleta ndege mpya, nilimwita Katibu Mkuu wa wizara anipe ufafanuzi wa jambo hilo, lakini, akaniambia hafahamu lolote," alisema Dk Mwakyembe.

Aliongeza, "Ndege hiyo ilikodishwa na kutua nchini kwa mara ya kwanza mwezi uliopita kutokana na iliyokuwapo kuanguka mkoani Kigoma. Ndege hiyo aina ya Boeing 737-500 imekodishwa kutoka Kampuni ya Aero Vista ya Dubai."

Dk Mwakyembe kwa sauti ya ukali alisema, "Niliamua kuwaita wakurugenzi wa ATCL ofisini kwangu saa 3 asubuhi, lakini wakaja saa nne na nusu, pamoja na hayo walinieleza kuwa jambo hilo liko safi na limeshafika kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali."

Alisema baada ya siku moja, alipata taarifa kutoka ofisi ya AG ikieleza kwamba hawana mkataba huo.

"Nikaona jambo zito kidogo, nikaamua kukutana na wale wawekezaji ambao walinionyesha mkataba ule ambao ulipitishwa bila wizara kujua, jambo hilo nililihoji pia&#8230;, nawambia ukweli mkataba huu niliuona upande wa pili sio kwa viongozi wa shirika," alisema Dk Mwakyembe.

Alisema hivi sasa mchakato wa kuchunguza mikataba hiyo umeshaanza na kusisitiza kuwa, hiyo ndio ilikuwa moja ya sababu ya kumng'oa Chizi.

Dk Mwakyembe alisema, "nchi haiwezi kuendelea kwa kukiukwa kwa sheria za ununuzi na ajira. Hata Kapteni Lazaro naye ameponea chupu chupu maana kabla ya kuwang'oa wakurugenzi tulipitia mafaili yao."

"Msitegemee kubebwa ndugu zangu, nawaomba mchape kazi, mishahara yenu sio mizuri, lakini mkiweza kusimama mtakuwa na uwezo wa kujipangia hata mishahara," alisema Dk Mwakyembe.

Alisema kwa kutambua mchango wa ATCL, Serikali imepata Sh4.9 bilioni kwa ajili ya matengenezo ya ndege ya shirika hilo na kuwataka kuzitumia kwa ufanisi fedha za shirika hilo."Hivi sasa inatakiwa kila baada ya miezi mitatu tunakutana na kuzungumza," alisema Dk Mwakyembe.

Kapteni Lazaro aahidi ushirikiano
Kwa upande wake, Kapteni Lazaro aliahidi kuyazingatia yote yaliyozungumzwa na waziri huyo, huku akiomba shirika hilo kuongezewa muda zaidi kwa kuwa miezi mitatu ni michache ili liweze kujitegemea.

Kupanda/kushuka ATCL
ATCL ni kampuni iliyoanzishwa baada ya Shirika la Ndege la Tanzania ATC kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mnamo mwaka 2002.

ATCl ni moja ya mashirika ya ndege yaliyoonyesha kukua kwa kasi miaka ya 1980 na 1990, lakini lilianza kuyumba kutokana na uendeshaji mbovu na hali ikawa mbaya zaidi baada ya kuingia ubia na SAA.

Serikali iliingia mkataba wa ubia na SAA mwaka 2002 kwa matumaini kwamba itakua na kuwa moja ya mashirika makubwa ya ndege Afrika, lakini hali ikawa kinyume chake.

Kwenye mkataba huo, Serikali ikibakia na hisa 49 huku SAA ikiwa nazo 51, ambazo zilimfanya mbia huyo kuwa na nguvu ya kuamua mambo mengi.

Serikali ilivunja mkataba na SAA Septemba 2006, baada ya kubaini kuwa ATCL inazidi kudidimia kiuchumi huku madeni yakiwa yanaongezeka kadri muda ulivyokuwa unaenda.
Mwakyembe: Nimemng?oa bosi ATCL kwa ufisadi
 
Kiko wapi??wezi wachomwe moto tu...dawa ya mwizi ni moto pekee.

Wezi wa nazi tu sokoni, au hata wezi wa rasilimali za nchi. Kila ninaposoma wanaochomwa moto naona ni wezi wa magengeni na wadokozo tu. Wanaoiba rasilimali za nchi wanapita huku wakipunga mkono.
 
Tumechoka na siasa za ATCL, bora ife tu ianze kitu ingine.

Nijuavyo mimi ATCL ilijaa mijitu ya system, ikajisahau kazi rasmi ikabobea kwenye siasa,
  • ni shirika mzigo lakini kila siku kwenye media
  • mleta mada ni mtu wa ATCL na ni "walewale"
  • either waziri kakosea au hajakosea... your time is all over due... if i was in authority ningua tu hilo shirika tuone kama mngeshinda kwenye media badala ya kufanya kazi
  • kuzungumzia bei kini ya market price kuna factors nyingi sana, ubora, au kutuaminisha kwamba mlikua mnababua, wakubwa unao-refer wamekosa ulaji ni walewale wa "system" ambao wanawadanganya na sasa mwakyembe kawageuka ( he has nothing to lose, alishakufa akafufuka... allegedly)
  • Kuhusu kukurupuka... maybe it is the last chance, maana staha hizo za "kiswahili" ndizo zilizofikisha hapo ATCL

SAFI SANA, SAFI SANA, SAFI SANA........... NINGEKUA MIMI NINGEVUNJILIA MBALI KABISA ATCL... MZIGO MKUBWA

BTW, MBONA HAMKUTOKA KWENYE KIKAO?

MLETA MADA, VIPI SUALA LA KUSHONA NGUO? AU NALO JUNGU?
 
Paul Chizi amewachishwa kutokana na utaratibu mbovu wa kumuajiri. Kuna uwezekano mkubwa kabisa akarudishwa kwa kufuata taratibu ili baadae kusiwe na malalamiko.

Sioni ubaya wa kusimamishwa mtu kwa kuwa aliajiriwa bila taratibu kufatwa na ikiwa taratibu zitafatwa na yeye ana qualify kama taratibu zikifatwa sioni sababu kwanini asiajiriwe tena.
tHANKS

tatizo letu kama kawa na uswahili wetu tumeshaanza majungu ya ukabila....... that is where our shallow mind kila siku inatupeleka kwenye hisia na kuacha facts

to me whether mwakyembe is right or wrong, some shake up was needed, ATCL concubine was in such a comfort zone
 
Wadau,

Nasikitika kwamba badala ya mimi kushangilia maamuzi ya waziri, kwa hili naomba nionyeshe masikitiko yangu makubwa hasa kwa mtu muelewa kama Dr Mwakyembe. Alichokifanya mh huyu ndo yale yale ambayo yalilalamikiwa nab w Lowasa wakati ule, maamuzi ambayo hayatokani na utafiti bali mujungu na kutafuta kuonekana kutenda hata kama unafanya madudu.

  1. ATCL kwa mara ya kwanza mefanikiwa kupata ndege ya kukodi kwa bei chini ya wastani wa bei ya soko (block hour rate below market standard) ambayo kama nakumbuka vema ni USD 1,700 wakati soko liko USD 2,400
  2. Kwenye mkataba huu ambao wakubwa wanasikitika kupigwa chenga ya mkataba ambayo kwa kawaida ndiyo sehemu ya ulaji wa wakubwa wetu, umeondoa yale mazoea ya kulipa kishika uchumba (down/advance payment) ambayo nayo huwa inachakachuliwa na wakubwa. Badala yake hii ya sasa ni kulipa kutokana na matumizi based on block hour usage
  3. Market penetration yao ambayo return ticket ya KIA ni tzs 199k (against 340k ya PW) na Mwanza tzs 199k (tzs 420 ya PW) ambayo kwa wale wanaotumiwa na wazito wa PW, wameona ATCL ni threat at least kwa hizo routes mbili.
  4. Majungu kwamba ATCL management amepokea hela nyingi na kuzifuja during month of May ambapo mpaka waziri na naibu wake walinitembelea hapa J3 asubuhi na kuwapa ukweli bayana (as we are the only banker of ATCL) and yet wamekwenda kufanyia kazi fitna na mujungu
  5. Paul Chizi ambaye alikuwa sourced from Community Air, being of less than 5 Tanzanians who pocess an MBA in Aviation, leo mnasema vifungu vilikiukwa na ukweli unafahamika mtendaji mkuu wa wizara ni katibu mkuu&#8230;So, wa kuwajibika ni Eng Chambo ambaye ndiye alikuwepo Aug last year wakati Paul Chizi anapewa nafasi ya kukaimu u-CEO wa ATCL.
  6. ATCL kulaumiwa kulipa deni la Ultimate Security above $0.9m wakati kesi iliamuliwa na mahakama ya biashara Mar 2011 ambapo uongozi huu haukuwepo madarakani, ATCL hakuwa na pesa na hivyo serikali kupitia barua ya Eng Chambo kucommit kulipa deni ambalo hata hivyo kila wakiandikiwa barua wanapotezea kwa zaidi ya mwaka. Matokeo last week ATCL amepata mpunga wa malipo ya bima ya ndege iliyotembelea tumbo Kigoma, mdeni akawahi mahakamani na kuleta zuio la hela benki (garnishee nisi) na tumezuia pesa ambapo ATCL amerejea mahakamani kuomba kesi itizamwe upya na kukubaliana payment plan, yet wanasemwa kuwa wametumbua pesa.
Tunabaki tunakurupuka kama kawaida yetu na kuishia kuwaonyesha watanzania kwamba kukosoa kumbe ni rahisi kuliko kuongoza. Tunaishi kwa majungu na utafutaji wa njia za mkato wa kupata umaarufu kwa wananchi.

Natamani kama ningeyasema haya ana kwa ana badala ya kuyaandika. Lakini naona mazingira hayaruhusu. Binafsi nimefuatilia hili sakata toka early last week, nimeketi na watendaji wakuu wa ATCL, Wizara na mpaka juzi waziri na naibu wake. Ajabu sana, narudia tena ajabu sana uvumi kwamba nia ni kumg'oa Chizi ili awekwe ndugu wa mh toka nyumbani kwetu Mbeya nilikuwa nayo toka 28 May 2012. Mwisho wa siku ndicho kilichotokea.

Stanbic ndo sole banker wa ATCL, sasa mtu anaposema kuna fedha zimefunjwa wakati ATCL hajawahi kuwa na hela ndani ukiachilia ka-OD kadogo ambako tuliwapa ili waweze kuwa wanalipia mafuta PUMA Energy, maelekezo ya kulipa tumekuwa tunafanya wenyewe hapa ndani, pesa pekee walopata mwezi May ni ya mshahara toka serikalini few millions. Then mtu anasema wamefuja?!?

Unless mtu anambie kuna pesa ATCL alikuwa anapelekewa cash na serikali pale ofisini kwao, kitu ambacho ni non sense.Wadau,

==> Si maneno yangu wana jamvi, bali ni maneno ya mdau wa karibu wa Stanbic<===
Samahani mkuu wangu nauliza tu out of curiosity, Wewe ni Banker wa ATCL umewahi kupitia vitabu vya ATCL kutazama jinsi walivyotumia fedha zao na umejuaje kama nyie tu ndio mnazo account za ATCL hata wakitaka kununua vifaa nje kupitia mikopo ya serikali ni lazima ipitie kwenu?
Na pili, mtu yeyote anayeiba au kugushi fedha za wizara au shirika mara nyingi haziwezi kuwa ktk Account ya benki isipokuwa ktk account zenu kuna vitu ambavyo havionekani japokuwa fedha imetolewa.. Labda nikwambie kivipi. Kwa mfano kuna Cheque ya ATCL inaingia kwa mamillioni mtu anaweza ibadilisha cheki hiyo kwa jina tofauti na isiingie kwenu ikaenda ktk account yake na record ikarudi kwa mlipaji kuonyesha fedha imelipwa. Kwenu hamtaiona hiyo fedha lakini ATCL records zake inaonyesha wamelipwa.. Upo? Hivyo ni vizuri kama unatueleza kwamba unajua toka pande zote mbili kilichotokea na nani mhusika ama wahusika ktk scandal nzima.
 
Mwakyembe: Nimemng’oa bosi ATCL kwa ufisadi Send to a friend
Thursday, 07 June 2012 19:54
0digg

atcl-mwakyembe.jpg
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza katika mkutano na na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) uliofanyika Dar es Salaam jana. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi mpya wa ATCL, Milton Lazaro na Mkurugenzi Rasilimali Watu, Judith Ndaba. Picha na Rafael Lubava

ASEMA WANAOUNUNG’UNIKA WAKO HURU KUJIONDOKA
Fidelis Butahe
SIKU nne baada ya kung’olewa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameamua kuanika tuhuma za ufisadi zinazodaiwa kufanywa na kigogo huyo.Miongoni mwa tuhuma hizo ni kuingia mkataba wa kununua ndege bila kumhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na kununua sare 15 za watumishi wa ndege kwa dola 50,000 za Marekani.

Juni 5, Dk Mwakyembe alitengua uteuzi wa Chizi na kumteua rubani wa muda mrefu, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi hiyo, akisema uteuzi ulikiuka Sheria za Utumishi wa Umma.

Mbali na kutengua uteuzi huo, pia alitangaza kuwasimamisha kazi vigogo wengine wanne wa shirika hilo, hatua ambayo ilianza kuibua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi kwamba hatua hiyo ilitokana na majungu na ukabila.

Waliosimamishwa kazi na Dk Mwakyembe ni Kaimu Mkurungenzi wa Uhandisi, Jonh Ringo, Mwanasheria ,Amini Mziray, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Justus Bashara na Josephat Kagirwa ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Biashara.

Jana, waziri huyo wa uchukuzi aliamua kufafanua tuhuma moja hadi nyingine zinazomhusu kigogo huyo na wenzake na kusema, mbali ya tuhuma za Chizi, wakurugenzi wawili wa shirika hilo walikwenda kushonesha sare 15 za wahudumu wa ndege nchini China kwa gharama ya dola 50,000 za Marekani (karibu Sh80 milioni).

Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika Uwanja wa Ndege wa zamani (Terminal One) jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe alisema kutokana na hali hiyo, ameagiza kujazwa kwa nafasi zilizo wazi na kuwaonya watakaozichukua, kuhakikisha wanachapa kazi ili ATCL ipige hatua na kama wakishindwa watakuwa wamejiondoa wenyewe.

Dk Mwakyembe alitoa miezi mitatu kwa shirika hilo kuanza kujiendesha kwa faida, ikiwa ni pamoja na kupata fedha za kuwalipa wafanyakazi wake.

“Kwa kasi niliyoanza nayo watu kama Chizi ni lazima wakae pembeni, ni mtaalam katika masuala haya, lakini tatizo lake hakuwa muwazi,” alisema Dk Mwakyembe.Chizi hakupatikana jana kuzungumzia tuhuma hizo, wakati wote Mwananchi ilipompigia simu yake ya kiganjani, ilikuwa imezimwa.

Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, alitumia Saa 1:17 kuzungumza na wafanyakazi hao na kufafanua kwamba Serikali imechoka kutoa fedha za kuliendesha shirika hilo, akihoji iweje mashirika mengine ya ndege yaweze kusimama yenyewe, lakini ATCL iishindwe.

“Tunaipenda ATCL iendelee na tunachukua hatua za kila aina ila tukiona tunashindwa tutaachana nalo ili, fedha zinazotumika hivi sasa zipelekwe kufanyia mambo mengine ya maendeleo,” alisema Dk Mwakyembe.

Tuhuma
Akichambua tuhuma moja hadi nyingine za ukiukwaji wa sheria na taratibu, Dk Mwakyembe alianza kwa kutolea mfano mkataba tata baina ya shirika hilo na Air Bus ambao umeifanya nchi kudaiwa Sh69 bilioni na kusisitiza kuwa, kutokana na hali hiyo Serikali haikuwa tayari kufumbia macho mambo mengine ya ovyo yaendelea katika shirika hilo.

Alisema wafanyakazi wote wa ATCL ambao wananung’unika baada ya kutengua uteuzi wa Chizi wako huru kuondoka katika shirika hilo, huku akionya atawatimua wengi watakaofanya mambo kinyume.

“Nilipoteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi siku chache baadaye nilisikia ATCL wanaleta ndege mpya, nilimwita Katibu Mkuu wa wizara anipe ufafanuzi wa jambo hilo, lakini, akaniambia hafahamu lolote,” alisema Dk Mwakyembe.

Aliongeza, “Ndege hiyo ilikodishwa na kutua nchini kwa mara ya kwanza mwezi uliopita kutokana na iliyokuwapo kuanguka mkoani Kigoma. Ndege hiyo aina ya Boeing 737-500 imekodishwa kutoka Kampuni ya Aero Vista ya Dubai.”

Dk Mwakyembe kwa sauti ya ukali alisema, “Niliamua kuwaita wakurugenzi wa ATCL ofisini kwangu saa 3 asubuhi, lakini wakaja saa nne na nusu, pamoja na hayo walinieleza kuwa jambo hilo liko safi na limeshafika kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.”

Alisema baada ya siku moja, alipata taarifa kutoka ofisi ya AG ikieleza kwamba hawana mkataba huo.

“Nikaona jambo zito kidogo, nikaamua kukutana na wale wawekezaji ambao walinionyesha mkataba ule ambao ulipitishwa bila wizara kujua, jambo hilo nililihoji pia…, nawambia ukweli mkataba huu niliuona upande wa pili sio kwa viongozi wa shirika,” alisema Dk Mwakyembe.

Alisema hivi sasa mchakato wa kuchunguza mikataba hiyo umeshaanza na kusisitiza kuwa, hiyo ndio ilikuwa moja ya sababu ya kumng’oa Chizi.

Dk Mwakyembe alisema, “nchi haiwezi kuendelea kwa kukiukwa kwa sheria za ununuzi na ajira. Hata Kapteni Lazaro naye ameponea chupu chupu maana kabla ya kuwang’oa wakurugenzi tulipitia mafaili yao.”

“Msitegemee kubebwa ndugu zangu, nawaomba mchape kazi, mishahara yenu sio mizuri, lakini mkiweza kusimama mtakuwa na uwezo wa kujipangia hata mishahara,” alisema Dk Mwakyembe.

Alisema kwa kutambua mchango wa ATCL, Serikali imepata Sh4.9 bilioni kwa ajili ya matengenezo ya ndege ya shirika hilo na kuwataka kuzitumia kwa ufanisi fedha za shirika hilo.“Hivi sasa inatakiwa kila baada ya miezi mitatu tunakutana na kuzungumza,” alisema Dk Mwakyembe.

Kapteni Lazaro aahidi ushirikiano
Kwa upande wake, Kapteni Lazaro aliahidi kuyazingatia yote yaliyozungumzwa na waziri huyo, huku akiomba shirika hilo kuongezewa muda zaidi kwa kuwa miezi mitatu ni michache ili liweze kujitegemea.

Kupanda/kushuka ATCL
ATCL ni kampuni iliyoanzishwa baada ya Shirika la Ndege la Tanzania ATC kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mnamo mwaka 2002.

ATCl ni moja ya mashirika ya ndege yaliyoonyesha kukua kwa kasi miaka ya 1980 na 1990, lakini lilianza kuyumba kutokana na uendeshaji mbovu na hali ikawa mbaya zaidi baada ya kuingia ubia na SAA.

Serikali iliingia mkataba wa ubia na SAA mwaka 2002 kwa matumaini kwamba itakua na kuwa moja ya mashirika makubwa ya ndege Afrika, lakini hali ikawa kinyume chake.

Kwenye mkataba huo, Serikali ikibakia na hisa 49 huku SAA ikiwa nazo 51, ambazo zilimfanya mbia huyo kuwa na nguvu ya kuamua mambo mengi.

Serikali ilivunja mkataba na SAA Septemba 2006, baada ya kubaini kuwa ATCL inazidi kudidimia kiuchumi huku madeni yakiwa yanaongezeka kadri muda ulivyokuwa unaenda.
Mwakyembe: Nimemng?oa bosi ATCL kwa ufisadi

Asante kwa hii article....at least imeeleza sababu za upande mmoja , tusubiri Mr. Chizi nae aote upande wake , Haya mambo yakuja na speculations na personal attacks hayasaidii.

Ikiwezekana MODs wake hii article kwenye post ya kwanza.ie watu wa follow vizuri.
 
aetcl_300_186.jpg
atcl-mwakyembe.jpg
airtzzzz_300_179.jpg

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza katika mkutano na na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) uliofanyika Dar es Salaam jana. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi mpya wa ATCL, Milton Lazaro na Mkurugenzi Rasilimali Watu, Judith Ndaba.

Mwakyembe: Nimemng'oa bosi ATCL kwa ufisadi

ASEMA WANAOUNUNG'UNIKA WAKO HURU KUJIONDOKA

SIKU nne baada ya kung'olewa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameamua kuanika tuhuma za ufisadi zinazodaiwa kufanywa na kigogo huyo.Miongoni mwa tuhuma hizo ni kuingia mkataba wa kununua ndege bila kumhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na kununua sare 15 za watumishi wa ndege kwa dola 50,000 za Marekani.

Juni 5, Dk Mwakyembe alitengua uteuzi wa Chizi na kumteua rubani wa muda mrefu, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi hiyo, akisema uteuzi ulikiuka Sheria za Utumishi wa Umma. Mbali na kutengua uteuzi huo, pia alitangaza kuwasimamisha kazi vigogo wengine wanne wa shirika hilo, hatua ambayo ilianza kuibua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi kwamba hatua hiyo ilitokana na majungu na ukabila. Waliosimamishwa kazi na Dk Mwakyembe ni Kaimu Mkurungenzi wa Uhandisi, Jonh Ringo, Mwanasheria ,Amini Mziray, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Justus Bashara na Josephat Kagirwa ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Biashara.

Jana, waziri huyo wa uchukuzi aliamua kufafanua tuhuma moja hadi nyingine zinazomhusu kigogo huyo na wenzake na kusema, mbali ya tuhuma za Chizi, wakurugenzi wawili wa shirika hilo walikwenda kushonesha sare 15 za wahudumu wa ndege nchini China kwa gharama ya dola 50,000 za Marekani (karibu Sh80 milioni). Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika Uwanja wa Ndege wa zamani (Terminal One) jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe alisema kutokana na hali hiyo, ameagiza kujazwa kwa nafasi zilizo wazi na kuwaonya watakaozichukua, kuhakikisha wanachapa kazi ili ATCL ipige hatua na kama wakishindwa watakuwa wamejiondoa wenyewe.

Dk Mwakyembe alitoa miezi mitatu kwa shirika hilo kuanza kujiendesha kwa faida, ikiwa ni pamoja na kupata fedha za kuwalipa wafanyakazi wake "Kwa kasi niliyoanza nayo watu kama Chizi ni lazima wakae pembeni, ni mtaalam katika masuala haya, lakini tatizo lake hakuwa muwazi," alisema Dk Mwakyembe.Chizi hakupatikana jana kuzungumzia tuhuma hizo, wakati wote Mwananchi ilipompigia simu yake ya kiganjani, ilikuwa imezimwa.

Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, alitumia Saa 1:17 kuzungumza na wafanyakazi hao na kufafanua kwamba Serikali imechoka kutoa fedha za kuliendesha shirika hilo, akihoji iweje mashirika mengine ya ndege yaweze kusimama yenyewe, lakini ATCL iishindwe. "Tunaipenda ATCL iendelee na tunachukua hatua za kila aina ila tukiona tunashindwa tutaachana nalo ili, fedha zinazotumika hivi sasa zipelekwe kufanyia mambo mengine ya maendeleo," alisema Dk Mwakyembe.

Tuhuma
Akichambua tuhuma moja hadi nyingine za ukiukwaji wa sheria na taratibu, Dk Mwakyembe alianza kwa kutolea mfano mkataba tata baina ya shirika hilo na Air Bus ambao umeifanya nchi kudaiwa Sh69 bilioni na kusisitiza kuwa, kutokana na hali hiyo Serikali haikuwa tayari kufumbia macho mambo mengine ya ovyo yaendelea katika shirika hilo. Alisema wafanyakazi wote wa ATCL ambao wananung'unika baada ya kutengua uteuzi wa Chizi wako huru kuondoka katika shirika hilo, huku akionya atawatimua wengi watakaofanya mambo kinyume. "Nilipoteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi siku chache baadaye nilisikia ATCL wanaleta ndege mpya, nilimwita Katibu Mkuu wa wizara anipe ufafanuzi wa jambo hilo, lakini, akaniambia hafahamu lolote," alisema Dk Mwakyembe.

Aliongeza, "Ndege hiyo ilikodishwa na kutua nchini kwa mara ya kwanza mwezi uliopita kutokana na iliyokuwapo kuanguka mkoani Kigoma. Ndege hiyo aina ya Boeing 737-500 imekodishwa kutoka Kampuni ya Aero Vista ya Dubai." Dk Mwakyembe kwa sauti ya ukali alisema, "Niliamua kuwaita wakurugenzi wa ATCL ofisini kwangu saa 3 asubuhi, lakini wakaja saa nne na nusu, pamoja na hayo walinieleza kuwa jambo hilo liko safi na limeshafika kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali."

Alisema baada ya siku moja, alipata taarifa kutoka ofisi ya AG ikieleza kwamba hawana mkataba huo. "Nikaona jambo zito kidogo, nikaamua kukutana na wale wawekezaji ambao walinionyesha mkataba ule ambao ulipitishwa bila wizara kujua, jambo hilo nililihoji pia&#8230;, nawambia ukweli mkataba huu niliuona upande wa pili sio kwa viongozi wa shirika," alisema Dk Mwakyembe. Alisema hivi sasa mchakato wa kuchunguza mikataba hiyo umeshaanza na kusisitiza kuwa, hiyo ndio ilikuwa moja ya sababu ya kumng'oa Chizi.

Dk Mwakyembe alisema, "nchi haiwezi kuendelea kwa kukiukwa kwa sheria za ununuzi na ajira. Hata Kapteni Lazaro naye ameponea chupu chupu maana kabla ya kuwang'oa wakurugenzi tulipitia mafaili yao." "Msitegemee kubebwa ndugu zangu, nawaomba mchape kazi, mishahara yenu sio mizuri, lakini mkiweza kusimama mtakuwa na uwezo wa kujipangia hata mishahara," alisema Dk Mwakyembe. Alisema kwa kutambua mchango wa ATCL, Serikali imepata Sh4.9 bilioni kwa ajili ya matengenezo ya ndege ya shirika hilo na kuwataka kuzitumia kwa ufanisi fedha za shirika hilo."Hivi sasa inatakiwa kila baada ya miezi mitatu tunakutana na kuzungumza," alisema Dk Mwakyembe.​

Kapteni Lazaro aahidi ushirikiano
Kwa upande wake, Kapteni Lazaro aliahidi kuyazingatia yote yaliyozungumzwa na waziri huyo, huku akiomba shirika hilo kuongezewa muda zaidi kwa kuwa miezi mitatu ni michache ili liweze kujitegemea.​

Kupanda/kushuka ATCL
ATCL ni kampuni iliyoanzishwa baada ya Shirika la Ndege la Tanzania ATC kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mnamo mwaka 2002. ATCl ni moja ya mashirika ya ndege yaliyoonyesha kukua kwa kasi miaka ya 1980 na 1990, lakini lilianza kuyumba kutokana na uendeshaji mbovu na hali ikawa mbaya zaidi baada ya kuingia ubia na SAA. Serikali iliingia mkataba wa ubia na SAA mwaka 2002 kwa matumaini kwamba itakua na kuwa moja ya mashirika makubwa ya ndege Afrika, lakini hali ikawa kinyume chake.

Kwenye mkataba huo, Serikali ikibakia na hisa 49 huku SAA ikiwa nazo 51, ambazo zilimfanya mbia huyo kuwa na nguvu ya kuamua mambo mengi. Serikali ilivunja mkataba na SAA Septemba 2006, baada ya kubaini kuwa ATCL inazidi kudidimia kiuchumi huku madeni yakiwa yanaongezeka kadri muda ulivyokuwa unaenda.
 
In between lines= ngome ya Lowas yaondolewa ATCL. Haya tutasikia mengi. Fikiria kama mbayuwayu, chakachua na zako.
 
effectiveness ndugu yangu ndiyo cha msingi kwenye kazi...mimi nafanya kazi na mtu ana digrii tatu za field tofauti zenye maana tu..lakini ukikaa naye unatamani umpige vibao kwa reasoning yake ilivyo hovyo..effectiveness mkuu..haya ya kusema unamjua fulani toka lini..watu tulikuwa tunamjua kikwete toka akiwa waziri wa mambo ya nje,ccm,daruso..halafu ametufikisha wapi.

Post yangu ilibase katika effectiveness. Na kama waziri angejali effectiveness na si ukabila, asingemtoa Chizi.
 
Ma bankers wa bongo hao. Upande mmoja nakuwa kama siwezi kuamini kwamba banker anayeijua kazi yake anaweza kuandika hivi.

Upande mwingine bongo anything is possible, why, Kikwete kawa rais.

Alichaguliwa na Ma bankers! kwi kwi kwi teh teh teh. Tanzania imekuwa Switzerland.
 
Mleta hoja hukufanya utafiti kwanza naamini Chizi hajatolewa kwa kukurupuka sababu zimetajwa na ziko wazi.
 
Back
Top Bottom