ATCL kurejea angani Ijumaa!!!

Shirika la ndege tanzania (ATCL) linatarajia kuanza safari zake za ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya shirika hilo Mkurugenzi mkuu alisema wamepania kurudisha heshima iliyopotea kwa muda mrefu.
Aliainisha ya kuwa safari yao ya kwanza itaanza Ijumaa ya wiki hii na itakuwa ni kutoka Dar- Mza- kilimanjaro. Ikifuatiwa na safari za dar-zanz- Arusha kisha katikati ya mwezi novemba wataanza safari za dar- mtwara.
Akizungumzia safari za nje ya nchi alisema wataanza na safari za dar- Moroni hiyo ni kwa mwezi Nov.
Pia alisema wanatarajia kununua ndege mbili kubwa kwa ajili ya safari za ULAYA DUBAI NA CHINA IFIKAPO mwishoni mwa Desemba au mwanzoni mwa january.
Jamani tufunge na kuomba kwa imani zote yasije yakawa maneno matupu.
Kuelekea mageuzi ya kisiasa na kiuchumi tufufue vya nyumbani kwanza.
 
Mkuu mtotowamjini, hawa jamaa(ATCL) ndege zao sio safi kama PA, lakini tatizo ni kwamba PA hawajali kabisa muda, yaani ni kero mkuu, plus upotevu wa vitu...kama kweli ATCL watakuwa wamejipanga inawezekana tikaikimbia kabisa hii PA.

Hapo muujiza unangojewa - as long as linabaki shirika la umma halitakwepa athari mbaya za watawala. Hakuna kitu hapo.
 
Hata siku ile ndege ya kukodi kutoka DUBAI ilivyo wasili story zilikuwa hizo hizo. HILI SHIRIKA ILI LIFUFUKE NI LAZIMA WAFANYAKAZI WOTE WAPIGWE CHINI NA WAANZE KUAJILI UPYA. Haiwezekani shirika liwe na ndege moja then wafanyakazi zaidi ya mia.
 
Ni ushauri tu, kama wakitaka ATCL iendelee, ile board of directors isiwe na watu wenye comflict of interests? Yaani utakuta members baadhi ni members wa 540, Precision Air na hata KQ, unategemea hilo shirika litaendelea? Si ni kuliua tu? Na wafanyakazi kibao kwenye ndege moja wala siyo tija wala sifa. Hata kama Precision Air ni private enterprise, niliwadiscredit nilipoona ndege moja (Hata kama ni Boeing 737) ina wafanyakazi kama nane au kumi hivi. Watatu au wanne wanagawa refreshments, watatu wanatoa maelekezo na wawili marubani na yule binti mmoja anatangaza na kuwahudumia marubani, WA NINI WOTE HAWA? watatu wangetosha tu including marubani, air hostess mmoja afanye yote. Route ndefu kuliko zote hapa Tz ni Dar- Mz direct, muda ni saa moja na nusu maximum. Wafanyakazi wengi wa nini wakati hawaongezi efficiency?

No wonder nauli inakuwa juu ili kufidia mzigo wa wafanyakazi. Na hii nadhani inatokana na "yule ni mtoto wa mjomba, yule ni mpwa, yule ni shemeji yake na bibi yake na mama yangu". Full of corruption!!!! Kama itaendelea kuwa kama ilivyokuwa, wala msitegemee mabadiliko. Itakuwa ni ku pump in money kwenye shirika uselessly!!!!

jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. namba ya wahudumu inategemea na uwezo wa kubeba abiria wa ndege husika. hili limekaa kisheria zaidi. maelezo haya nimeyapata kwa mdau mmoja hapa Mwanza ambaye alianzisha shirika ambalo halikudumu sana. anasema sheria zenyewe zinalazimisha uwe na wahudumu wengi japo anasema Europe aliona wawili tu kwenye ndege kama yake.
 
Ili mbegu iote lazima ioze kwanza
 
ATCL wana challenges kama tatu hivi:
1. wanaweza vipi kupata management isiyofungamana na wanasiasa
2. kujua internal weaknesses (maana hakuna strength pale)
3. kufikiria substitutes za kibiashara kama connections huku wakiangalia competitors wao kama precision, KQ, Rwandair, Air Uganda, 540 nk.

Kwa vile ni vigumu kupangua hayo matatizo ni bora wangejipambanua kama kampuni ndogo tu ya domestic charter na maeneo ya jirani (aina ya TANZANAIR) kwa miaka mitano hivi then watakuwa wamejua how to fly further and beyond boarders

koma kq imakufanyaje
 
jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. namba ya wahudumu inategemea na uwezo wa kubeba abiria wa ndege husika. hili limekaa kisheria zaidi. maelezo haya nimeyapata kwa mdau mmoja hapa Mwanza ambaye alianzisha shirika ambalo halikudumu sana. anasema sheria zenyewe zinalazimisha uwe na wahudumu wengi japo anasema Europe aliona wawili tu kwenye ndege kama yake.

Mkuu sheria za aviation ni za kimataifa (IAAL) na SIDHANI kama zinatemea sheria mahalia, well inawezekana. Nasema hivi hivi kwasababu kama ulivyosema kule kwa wenzetu utakuta dege linasafiri fourteen to sixteen hours pengine nonstop (Transcontinental airlines/ Zile zinazovuka mabara) Kuna wahudumu wanne, wawili hostesses na wawili marubani, na mbaya zaidi ndege nyingi za saa moja na mawili kama hapa kwetu wahudumu ni watatu tu, mmoja hostess na wawili ni marubani. Kama sheria za nchini kwetu zinabana idadi ya wafanyakazi basi ujue wakuu wetu wameziweka hizo sheria ili ziwasaidie wao na familia zao.

Kwenye business enterprise watu wanatafuta efficiency ya hali ya juu kwa kupunguza labor power. Kama watu wawili wanaweza kufanya kazi ya watu nane au kumi kwa ufanisi uleule au zaidi, why not go for that? na hii inapunguza gharama za uendeshaji hence nauli ya msafiri inakwenda chini sana! Fuatilia community airlines ilikuwa na wahudumu wangapi? Pengine waliwekewa vikwazo ili vigogo waendeleze ukiritimba wao
icon4.png
 
Ni ushauri tu, kama wakitaka ATCL iendelee, ile board of directors isiwe na watu wenye comflict of interests? Yaani utakuta members baadhi ni members wa 540, Precision Air na hata KQ, unategemea hilo shirika litaendelea? Si ni kuliua tu? Na wafanyakazi kibao kwenye ndege moja wala siyo tija wala sifa. Hata kama Precision Air ni private enterprise, niliwadiscredit nilipoona ndege moja (Hata kama ni Boeing 737) ina wafanyakazi kama nane au kumi hivi. Watatu au wanne wanagawa refreshments, watatu wanatoa maelekezo na wawili marubani na yule binti mmoja anatangaza na kuwahudumia marubani, WA NINI WOTE HAWA? watatu wangetosha tu including marubani, air hostess mmoja afanye yote. Route ndefu kuliko zote hapa Tz ni Dar- Mz direct, muda ni saa moja na nusu maximum. Wafanyakazi wengi wa nini wakati hawaongezi efficiency?

No wonder nauli inakuwa juu ili kufidia mzigo wa wafanyakazi. Na hii nadhani inatokana na "yule ni mtoto wa mjomba, yule ni mpwa, yule ni shemeji yake na bibi yake na mama yangu". Full of corruption!!!! Kama itaendelea kuwa kama ilivyokuwa, wala msitegemee mabadiliko. Itakuwa ni ku pump in money kwenye shirika uselessly!!!!

Mkuu kuna taratibu zinazoongoza huduma za ndege,mfano idadi ya wafanyakazi wanaotakiwa kuruka na ndege. Idadi ya wafanyakazi 9 ktk ndege ya boeing kama hizi za Precisionair ni standard kabisa. Biashara ya ndege ni ngumu sana inayohitaji weledi. Kinyume chake wanasiasa wetu wanadhani ni kama biashara ya daladala!
 
Shirika la ndege tanzania (ATCL) linatarajia kuanza safari zake za ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya shirika hilo Mkurugenzi mkuu alisema wamepania kurudisha heshima iliyopotea kwa muda mrefu.
Aliainisha ya kuwa safari yao ya kwanza itaanza Ijumaa ya wiki hii na itakuwa ni kutoka Dar- Mza- kilimanjaro. Ikifuatiwa na safari za dar-zanz- Arusha kisha katikati ya mwezi novemba wataanza safari za dar- mtwara.
Akizungumzia safari za nje ya nchi alisema wataanza na safari za dar- Moroni hiyo ni kwa mwezi Nov.
Pia alisema wanatarajia kununua ndege mbili kubwa kwa ajili ya safari za ULAYA DUBAI NA CHINA IFIKAPO mwishoni mwa Desemba au mwanzoni mwa january.
Jamani tufunge na kuomba kwa imani zote yasije yakawa maneno matupu.
Kuelekea mageuzi ya kisiasa na kiuchumi tufufue vya nyumbani kwanza.

Afadhali wakatuchukulie ndugu zetu waliopo Ugiriki waepukane na kuadhirika nchi za watu.
 
jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. namba ya wahudumu inategemea na uwezo wa kubeba abiria wa ndege husika. hili limekaa kisheria zaidi. maelezo haya nimeyapata kwa mdau mmoja hapa Mwanza ambaye alianzisha shirika ambalo halikudumu sana. anasema sheria zenyewe zinalazimisha uwe na wahudumu wengi japo anasema Europe aliona wawili tu kwenye ndege kama yake.

hiyo ya idadi kidogo ya wafanyakazi ni kwa budget airlines. zinakuwa kama daladala hivi,hata nauli yake ni ndogo.
 
Mkuu kuna taratibu zinazoongoza huduma za ndege,mfano idadi ya wafanyakazi wanaotakiwa kuruka na ndege. Idadi ya wafanyakazi 9 ktk ndege ya boeing kama hizi za Precisionair
Wala sikatai ila believe me, hapa kwatu sheria za aviation zimekuwa regulated just to fit in our Politicians' interests. Kuhusu idadi niseme tu kuwa hili ni locally instituted manake kuna nchi nyingine za wenzetu idadi ya wafanyakazi katika ndege kama hizo za nyumbani kwetu ni ndogo sana!
 
At long last mnataka kuonesha dalili za kurudi angani. Kikubwa zaidi ya kutoa huduma uwepo wenu angani huwa unasaidia sana ku-adjust bei za usafiri wa ndege za haya mashirika binafsi. Hii ni fursa yako Bw Lussajo kumsafisha binamu yako Mwakyembe maana wengine tuliamini kuwa amekuweka kishkaji, shutuma ambazo utaweza kuziondoa kwa kufanya kazi nzuri..

Ila kuendesha shirika la ndege ni gharama kubwa na inahitaji mtaji wa uhakika ambao kwa hii serikali DHAIFU kamwe haitakuja kuupata. Ushauri wangu mjaribu kuunganisha mtaji na local investors in ku boost mtaji na mkishaanza kupata faida mje kwenye public tuingize vihela vyetu hapo kulipa mtaji shirika. Wenzenu KQ wana ndege zaidi ya 70 lakini hata watu binafsi wana hisa pale
acha uongo KQ haina ndege sabini! hata nusu yake hawajafikia KQ ina ndege 34 angalia hapa
 
koma kq imakufanyaje
mkuu Pdidy, naongeloea ninachokiona angani na si vinginevyo maana hawa ndio wanafuatilia kila 'endeleo' tunalofanya. Pia kuna Air Mozambique, Air Malawi japo Zambia na Congo sijaziona ndege zao kama threat hapa, au sijakuelewa??

SHRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL), limejipanga kurudisha safari zake kuanzia Ijumaa hii na kuahidi kujikita katika safari za ndani na kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro, alisema shirika lake limeanza kutekeleza mpango wa maendeleo utakaosaidia kuboresha utoaji huduma pamoja na upanuzi wa safari zake.
“Tumejipanga kurejesha huduma zetu Ijumaa hii huku tukiwa tumepanga kuongeza safari nyingine katika mkakati wetu wa kuhakikisha kuwa tunafika maeneo mengi nchini.
“Tutaanza na safari ya Dar es Salaam-Mwanza-Kilimanjaro kabla ya kuanzisha safari ya Dar es Salaam-Arusha-Zanzibar itakayozinduliwa Novemba 2.
“Tunawashukuru wateja wetu kwa kuwa nasi katika kipindi hiki kigumu tuliposimamisha huduma zetu na tunaahidi kuwapatia huduma bora na za kipekee kipindi tutakapoanza safari,” alisema Lazaro.
Lazaro aliongeza kuwa, shirika hilo lina mpango wa kuzindua safari ya Dar es Salaam-Mtwara itakayoanza Novemba 16, kwa kutumia ndege ya Dash 8-300 iliyokuwa katika matengenezo baada ya kuhusika kwenye ajali kipindi kifupi kilichopita.
“Changamoto kubwa sasa ni kujikita katika urejeshaji wa heshima ya shirika. Tumejipanga kununua ndege mbili mpya, ili kupanua huduma zetu na wakati mwingine tutaingia ubia na mashirika makubwa ya ndege, ili kuongeza safari zetu,” aliongeza.
Akizungumzia usitishwaji wa mkataba kati ya Kampuni ya ATCL na kampuni ya Aero Vista Agosti ambayo iliwakodisha ndege aina ya Boeing 737-500, Lusajo alisema mazungumzo kati ya kampuni hizo mbili yanaendelea na kusema wanategemea kufikia makubaliano muda si mrefu.

SAA nasikia wanamatatizo, kuna cha kujifunza kutoka na hasara na matatizo yao?
 
linco mkuu
unasubiri matatizo ya wenizio utokee hapo ..toolate
biblia inasema imani ni kuwa na uhakika wa mambo ytarajiwayo embu tuwape last chance kama movie inavyosema tuangalie
kuhusu idadi ya wafanyakazi nimeona comments nyingi nzuri za kuhimiza idadi ipungue sijaona wanaosema inatakiwa wawe wangapi..kama unashaurio ipungue angalia na ndege iliopo then shauri wawe wangapi usaidie management......

Kuhuusu hili la interest no comments maana Mramba anawezaa kuteleza zaidi atcl ilipokuwa then tukaendelea na hawa wengine kwa kweli...hili ni tatizo kubwa kama uamini soma raia mwema leo na uchunguzi wa mkurugenzi wa tanesco
kila la kheri wanasema mwombee adui yako aone mafanikiao naamini atcl itaongeza maombi zaidi this time wengine waone mafa ...yao
 
lakini hayo mandege wanayoleta ni ya kizamani mno.Boeing 737-200 ADV ? kibaya zaidi ni wet lease manake macrew wa ATCL currently hawako rated kuruka aircraft hiyo au model nyingine kwani hawajaenda training.Hili nalo linaongeza gharama za kulipa mishahara ya mapilot na crew members.Serikali isomeshe marubani na engineers ili wawe rated na kupunguza gharama
 
Back
Top Bottom